Na Faki Mjaka-Maelezo 
Zanzibar  29/12/2011

Wananchi wa Zanzibar wameombwa kushiriki katika Dua maalum ya Mkesha wa kuliombea taifa la Zanzibar ilioandaliwa na Umoja wa Makanisa Zanzibar ambapo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Add anatarajiwa kuwa Mgeni.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha huo Mchungaji Simon Mputa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo uliopo Raha leo Mjini Zanzibar.

Amesema dua hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia majira ya usiku wa kuamkia Mwaka 2012 katika Uwanja wa Mao tse Tung lengo lake kuu ni kuliombea taifa kuepukana na majanga mbali mbali ambayo yanaweza kulikumba Taifa hilo.

Mchungaji Simon amesema sambamba na kuliombea taifa pia kutafanyika maombi maalum ya shukrani kwa Mungu juu ya kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar pamoja na kuwaombea viongozi wake hekima na busara katika uongozi wao

Aidha ameongeza kuwa kuna haja ya wananchi kukaa kwa pamoja na kuweza kumuomba Mungu ili kuyaepusha majanga yaliyoikumba Tanzania mwaka 2011 yasiweze kutokea tena katika Mwaka mpya wa 2012

Ameyataja majanga hayo kuwa ni pamoja na ajali ya kuzama kwa Mv. Spice Islanders Zanzibar na Mafuriko yaliyoikumba mikoa ambali mbali ya Tanzania Bara ikiwemo Dar es Salaam na kusababisha vifo vya wananchi wengi.

Kwa upande wake Katibu wa Mkesha huo Mchungaji Edward Mashimba amesema maandalizi ya Mkesha huo yamekamilika na kuwataka wananchi wa Zanzibar kushiriki kwa wingi bila kujali itikadi za dini wala siasa zao.

Mchungaji Saimon amesema Maombi hayo ni maombi shirikishi ambayo hapo awali yalikuwa yakifanywa na watu wachache lakini kutokana na mwamko wa watanzania kumesababisha maombi hayo kufanyika katika viwanja ili kukidhi haja ya wageni wanaoshiriki

Naye Mraribu wa Tamasha hilo hapa Zanzibar Allen Mbaga amesema Mkesha wa Maombi wa kuliombea Taifa utafanyika katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na Visiwani ambapo washiriki wa Zanziabar watapata burudani mbali mbali kutoka kwa vikundi vya Kwaya huku huduma ya za vitafunwa na vinywaji vikiwa vinapatikana Uwanjani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mukiwa kwenu BARA munasema ZNZ si TAIFA ,huu ni unafiki na Mungu anawachukia WANAFIKI ndio maana adabu yao itakuwa kubwa zaidi.

    ReplyDelete
  2. haya tena zanzibar inazidi kupanuka kwa umoja wa makanisa kesho utasikia hamduni john

    hatutaki mikesha kama hiyo huku visiwani kama mnataka kaunganeni na wenzenu wa bara

    ReplyDelete
  3. Huyu mchungaji na mratibu wa tamasha wanasema maombi hayo hayalengi itikadi mbona wanajichanganya mwenyewe kwa kusema kwamba kutakuwa na burudani kama vile kwaya. Nijuavyo mimi kwaya ni kwa dini za kikristo lakini hakuna kitu hicho kwa dini za kiislamu. Waislamu kuweni makini msije mkakumbwa na mkumbo hatari msioujua, mtapotea bila kujitambua.

    ReplyDelete
  4. Mambo kama haya ndi yanayozalisha Al-shabab..mtakuja kukumbuka comment hii.
    Ninachotaka kusema hapa ni kwamba siku zote migogoro na misimamo mikali ya Dini huanza pale ambapo moja kati ya kundi hilo la Dini linapoona linadhulumiwa haki yake,so hapa Wazanzibar ambao kwa asilimia kubwa ni waislam watahisi wanavamiwa nchi yao na wagalatia so hapo ndipo hisia zakuwafukuza zitakapoanza na hatimae Al-qaeda na Shabab kuchukua nafasi za kutraine na kuongoza mapambano.

    ReplyDelete
  5. ZNZ zuieni kama mlivyozuia amizio la arusha huo mkutano wa maombi waambieni wakaufanyie Chumbe

    ReplyDelete
  6. Nawe Balozi uwe makini, tafadhali mtafute Johni awe ndie mgeni rasmi kwani muda wako wa kuishi ni mfupi mno hivyo usikubal kuingia katika hasara!!

    ReplyDelete
  7. Nawe Balozi uwe makini, tafadhali mtafute Johni awe ndie mgeni rasmi kwani muda wako wa kuishi ni mfupi mno hivyo usikubal kuingia katika hasara!!

    ReplyDelete
  8. Msituletee, hizo!! subirini vyama nyenu vya CUF na CHADEMA vipate madaraka(jambo ambalo ni ndoto)ndio mlete udini kama mtaweza.

    Kumbe kila mkiambiwa mna 'dizaini' hizo hapo, mnazidi..eeh?

    Basi mjue kadiri ambavyo 'Chama dume' litaendelea kubaki madarakani, Mtanzania ataishi popote ktk jamhuri hii na Kuabudu dini yoyote anayoitaka ilimradi tu, havunji sheria.

    ....Kazi kwetu watanzania!!!!

    ReplyDelete
  9. Mambo mapya haya Zenj niijuayo. yanachukua hatua kwa hatua,bila shaka wenywe wamevamiwa sasa.

    ReplyDelete
  10. HATUTAKI MAOMBI YA KIKRISTO KWENYE NCHI YETU YA ZANZIBAR FULL STOP!!!
    WATAKAOSHIRIKI WATAKUJA JUTA YATAKAYOWAKUTA.

    ReplyDelete
  11. HATUTAKI MAKANISA KATIKA VISIWA VYETU HIIIIIII KILA TUKIYACHOMA MOTO NDIO MUNAZIDI KUJA NA SPEED NYENGINE.............
    WAZANZIBARI 99% NI WAISLAM
    TUMEWACHIA KANISA LA MKUNAZINI,SHANGANI AMBAYO NI MAKUBWA SANA KULIKO KANISA LOLOTE KULE TANGANYIKA.
    KAMA MUNATAKA ALSHABAB WAANZE KAZI NDANI YA ZENJI BASI SUBIRINI TU MTAONA FAIDA YAKE?

    ReplyDelete
  12. Mie ni mbara na muislam. Nawaunga mkono 100% ndugu zangu wa visiwani, hawa watu ni hatari msikubali kabisa hayo maombi yao ya kinafiki, kama siyo ya kidini mbona masheikh hawakushirikishwa? Hizi ni mbinu zao, ona makanisa yalivyo shamiri znz. njoo bagamoyo, njoo dar, ni makanisa makanisa msikubali hawa watu ni wabaya mno..............yaani ni ule mkataba walioingia na serikali ndio umewapa power, kazi ya lowasa.

    ReplyDelete
  13. Mie ni mbara na muislam. Nawaunga mkono 100% ndugu zangu wa visiwani, hawa watu ni hatari msikubali kabisa hayo maombi yao ya kinafiki, kama siyo ya kidini mbona masheikh hawakushirikishwa? Hizi ni mbinu zao, ona makanisa yalivyo shamiri znz. njoo bagamoyo, njoo dar, ni makanisa makanisa msikubali hawa watu ni wabaya mno..............yaani ni ule mkataba walioingia na serikali ndio umewapa power, kazi ya lowasa.

    ReplyDelete
  14. Wenye hekima wanasema "do not argue with a fool people might not notice a difference" mtu yeyote mwenye akili atajua kabisa ni haki ya kila mtanzania kukaa popote pale na kuabudu chochote anochoabudu, wengine hapo juu wanaongelea kushamiri kwa makanisa, mbona hamjaongelea misikiti inayoshamiri kila kona ya nchi yetu. kanisa likijengwa kosa msikiti ukijengwa sio tatizo. mpaka mtu mwenye akili atajua watoa maoni hapo juu mna matatizo

    ReplyDelete
  15. mdau wa 2:59 na 3:00 nakupa big up usiangalie mbara au mznz uislam ndio muhimu we love u bro/sis jamaa hawa wanajifanya wajanja sana

    ReplyDelete
  16. Haya maombi ya ndani ya nyumba za Ibada,,,KHAAA ,sasa tuna lazimishana kuingia dini zingine!

    KILA MTU MKESHA WA SALA ATAFANYA KTK NYUMBA YA IBADA KULINGANA NA DINI YAKE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...