Waziri wa Nishati na Madini,Mh. William Ngeleja akihutubia wakati wa Kongamano la Uwekezaji (Tanzania Investment Forum 2011) hoteli bab kubwa ya May Fair jijini London jana
Waziri Ngeleja akiwa na Mh Naibu Balozi Chabaka wakiongea na mwananchi.
Bw. David Tarimo akiwa katika mazungumzo na Wadau wa Kongamano hio mara baada ya kumalizika.
Waziri wa Nishati na Madini, Mh. William Ngeleja (katikati),Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa ubalozi na wajumbe wa jumuiya ya Watanzania London.

Na Freddy Macha.

Wawekezaji, wataalam na wafanyabiashara toka kona mbalimbali ulimwenguni wamekaribishwa kwa mkono wa kheri kuendeleza uchumi na maendeleo ya nchi yetu katika kipindi kinachofuatilia miaka 50 ya Uhuru.

Akiongea wakati wa Kongamano la Uwekezaji (Tanzania Investment Forum 2011) hoteli bab kubwa ya May Fair jijini London jana Ijumaa, Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngeleja alisema tuko katika kipindi kipya cha maendeleo ya uchumi chenye manufaa kwa wafanyabiashara.

Waziri huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria aliuambia mkutano kwa Kiingereza fasaha: “Miaka mitatu iliyopita Bongo imebadilika toka mnunuzi wa bidhaa kuwa muuzaji wake. Mathalan siku hizi tunaiuzia Kenya chakula. Ukilinganisha nchi yetu na nyinginezo Afrika , tumekuwa makini shauri ya amani na utulivu miaka 50 iliyopita.”

Hotuba yake mheshimiwa ilikuwa miongoni mwa hoja nyingi zilizochambuliwa na washiriki wazawa wa Uingereza, Norway, Afrika Kusini, Kenya, Marekani, Uholanzi na Tanzania.

Soma habari zaidi :

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hivi ina maana hamna Watanzania wenye uwezo wa kufikiri na kuwekeza nchini mpaka kwenda nje kutafuta wawekezaji..? Ina maana wote wana akili za kivivu za kufikiri..? Na mpaka lini wanaume Watanzania watakoma kusimama na kubisha hodi katika milango ya wanaume wenzao..??!! Hivi kwa nini kila wakati na mara mwanamme unakaa unasimama kwenye mlango wa mwanamme mwenzio unaomba omba..?! Kulikoni?! Kama uko kilema sema..

    ReplyDelete
  2. lakini mbona viongozi wetu nchini ni wanasheria?alafu mambo hayaendi vizuri?tatizo ni nn?ukweli inauma sana wanapenda uongozi kwa nguvu zote mwisho wasiku wakipata wanatupeleka kusiko eleweka waachie wengine waiongoze nchi hiyo maana watu wa HGL NA HGK sasa tumeanza kuwachoka kilele nyingi kazi hakuna kuongea tuuu da

    ReplyDelete
  3. Ngeleje jifunza uwajibikaji, jiuzulu, wizara yako imechangisha fedha haramu.

    ReplyDelete
  4. Unalozi poa siku hizi mh chabaka mtu wa watu, mh Ngeleja unazidi kung'ara na Kua kijana .

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani hapa ingeandikwa hivi: MKUTANO WA WAWEKEZAJI VITEGA UCHUMI WAWASHA MOTO LONDONI. SIO WAWASHA KIBIRITI. Maana kibiriti ni chimbo tunachokitumia kupata au kuwasha moto. Lengo kuu hapa ni moto sio kiberiti.

    Mdau.

    ReplyDelete
  6. mbona hamkuzima hiyo luninga inayotuma mionzi ukutani kabla hamjapiga picha wajameni?

    ReplyDelete
  7. WAMESHAZOEA KUOMBA..HATA WAKIWA NA FIKRA NZURI HAWAZWEZI KUJIKOKOTA MPAKA WAKOKOTWE. PESA YOTE ILIYOKUWEPO AFRICA UNAFIKIRI KUTAFUTA SOKO ULAYA WAKATI WA FINANCIAL CRISIS.!!!!

    ReplyDelete
  8. MBONA WATU HAMNA USTARABU? Kwamana comments walizotia Sarah wingine ni utumbo tu, weye uliyesema MH NGELEJE AJIUZULU, UNA AKILI TIMAMU KWELI? napenda kukubaliana na mdau aluyechangia kwamba UBALOZI WETU UK SASA MAMBO MSWANO, mh CHABAKA KILUMANGA. NI MTU WA WATU KWELIKWELI

    ReplyDelete
  9. Fanya jitihada upate wawekezaji wa uhakika wa umeme na sio wasanii huko UK,,,ingawa umesha chemsha!

    ReplyDelete
  10. kwani wawekezaji huwa wanatokea wapi, kulikoni? sio huwa wanatokea njia za nje? inakuaje comments hapa baazi ni za kukandia? au wabongo hamuelewi swala hili.
    kuhusu ubalozi wetu ni hakika unatembeleka tangu alipokwenda mama ''maajar'' na sasa ''kalage na kilumanga'' wanashirikiana vizuri.

    ReplyDelete
  11. poa poa sana, maajar aliwaunganisha wabongo wote vizuri. lakini kuna wachache ubalozini wapo poa, wengine bado wana nyodo, lakini hata tukienda twajisikia tupo nyumbani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...