Shikamoo Kaka michuzi,
pole kwa kazi Kaka mkubwa. Jamani nina tatizo kidogo
ambalo nazani globu ya jamii na wadau wa IT wanaweza wakanitatulia.
Kama unavyojua sisi vijana siku hizi ni wajasiriamali kwa namna yeyote ile
kuipiga vita umaskini na hivyo basi mimi na Kaka yangu tumeungana mkono
tukaamua kuanzisha internet cafe maeneo ya Kilwa Road hapa jijini Dar es salaam kabla ya kufika Mbagala.
Hutaamini kaka mwezi mzima wa maandalizi,matengenezo na manunuzi ya vifaa lakini paka sasa hatujapata internet Service provider anayefaa.
Sio eti hawapo ila tunatafuta huduma kwa computer 5 na budget ya 'kikawaida' sana si unaelewa kaka ndio mwanzo.
Tulimtarajia TTCL akiwa yeye ndiye mama yao wote lakini tumeambiwa huduma mwisho ni Misheni(ingawa kwa kweli tunashangaa kama hii ni kweli). wengine wote hawa wanasema 'unlimited internet'.
Hivi kwa kweli hamna kampuni au ISP(Internet Service Provider) yeyote ambaye ana huduma ambayo kibiashara tutaweza kuitumia tukatoa huduma nzuri kwa kasi inayofaa????Jamani natoa hilichangamoto kwa yeyote aliye na uelewa na swala hili awasiliane nami tuchukue huduma. email yangu ni msakig@gmail.com
Ndugu sijakuelewa unaposema TTCl huduma mwisho ni misheni!! kwa ufupi si kwamba nawapigia debe TTCl ila kuna wajasiliamali kama wewe ambao wanatumia huduma za internet za ttcl na wanaendelea kupeta kama kawaida mfano jaribu kumuuliza huyu jamaaa 0684 007920 atakupa maelezo kamili alianza lini kutumia huduma za ttcl na mpaka sasa amepata faida kiasi gani
ReplyDeleteSimbanet ndio wanaongoza Tanzania kwa huduma nzuri. Pesa yako tu ya kuwekeza. Unapata unlimited service.
ReplyDeleteKaka,tatizo ni kwamba haifiki Misheni anapoiataka huku kaka.TTCL wanatoa huduma yao mwisho ni Mtongani na hivyo kwa yeye anayetaka kukianzisha Misheni hawezi kupata huduma. nazani hilo ndio tatizo la TTCL anavyoelezea.
ReplyDeleteISP wengi mdau wa kwanza hapo ju wapo ki maslahi tu!, kama ni tahafifu inakuwa ni ya muda tu ili kuvuta wateja halafu wakijaa wanakamua!
ReplyDelete