Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC
Lawrence Mafuru
Na Mwandishi Wetu

IMEELEZWA kuwa Tanzania bado inakabiliwa na uhaba wa huduma za kibenki na kukabiliwana changamoto kadhaa licha ya kuwepo mafanikio katika miaka 50 ya uhuru.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Lawrence Mafuru alisema kuwa wakati wa uhuru Tanganyika ilikuwa na benki moja tu ambayo ni Benki ya Taifa ya Biashara lakini baadaye kulijitokeza benki kadhaa ambazo zilichangia kwa kiwango kikubwa kukuza maendeleo ya taifa hili.

Alisema NBC kwa kiwango kikubwa ilichangia kukuza maendeleo ya taifa hili kwani ilishiriki kwa kiwango kikubwa katiuka ujenzi wa barabara na viwanda jambo ambalo lilichangia kwa kiwango kikubwa sana ukuaji wa maendeleo ya Tanzania.

Mafuru alisema kuwa nchi inaadhimisha miaka ya 50 ya uhuru lakini benki ya NBC itakuwa ikiadhimisha miaka 45 ya uwepo wake mapema mwakani jambo ambalo inaonesha ukomavu na ukongwe wa benki hii.

“Kuna mafanikio mengi sana ya kifedha ambayo tunajivunia licha ya nchi yetu kuendelea kutajwa katika kundi la nchi masikini kwa takwimu za kimataifa lakini ukweli ni kwamba tumeweza kusonga mbele kwa kiwango kikubwa sana katika masuala ya kifedha ukilinganisha nia miaka 50 iliyopita” alisema.

Alisema kuwa NBC imeweza kupiga hatua kubwa kwani mpaka hivi sasa ina matawi 53 nchini yaliyounganishwa katika mtandao wa teknolojia ya kisasa ya kibenki na kutoa huduma za kisasa zinazokidhi mahitaji kwa wateja yanayoendana na wakati.

NBC imeweza kutoa ajira za kudumu kwa wafanyakazi zaidi ya 1500 jambo ambalo limechangia ongezeko la kipato kwa watanzania na kupunguza tatizo la ajira nchini.

Pia Mafuru alisema kuwa NBC imekuwa mdau mkubwa wa huduma za kijamii hasa katika huduma za Afya, Elimu na uwekezaji katika makundi ya wasio na uwezo wa kumudu kupata huduma hizo muhimu nchini huku sulala la elimu peke yake NBC ikitumia kiasi cha shs Bilioni tatu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Halikadhalika Mafuru alisema kuwa NBC bado inaendelea kuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya taifa kwani kwa sasa inachangia upatikanaji wa makazi bora kwa watanzania kwani hivi karibuni imeingia mkataba na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kuweza kujenga makazi bora na ya bei rahisi kwa ajili ya watanzania.

Akizungumzia changamoto zilizopo nchini Mafuru alisema Tanzania bado inahitaji huduma za kibenki kwa kiwango kikubwa licha ya fikra ya kuwepo kwa changamoto baada ya kampuni za simu kujihusisha na utoaji wa huduma za kifedha, jambo ambalo alisema bado mahitaji ni makubwa sana. “Kwa sasa tuna benki 45 tu nchini ambazo zinatoa huduma kwa asilimia 10 tu ya watanzania hali hii inaonesha bado kuna mahitaji makubwa sana ya benki nchini hapa” alisema Mafuru.

Pia alisema hapa nchini kumekuwa na tatizo la kutokuwa na utamaduni wa uwajibikaji licha ya kuwepo wasomi wengi lakini bado taifa linahitaji watu wa kujitoa na kujituma zaidi katika utendaji wa kazi na kukuza weledi ili kuendana na wakati huu wa utandawazi, jambo ambalo limekuwa likitia hofu wengi kuwa nchi itakapoingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki watanzania wengi wanaweza kupoteza ajira hoja si kutokuwepo kwa wasomi ila suala lipo katika uwajibikaji.

Alisema ikiwa watanzania watajituma na kufanya kazi kwa bidii hakuna haja ya kuogopa kwani watakuwa na uwezo wa kushindana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunataka mikopo ya kujenga nyumba za kilala hoi, Kibaha nje na mji.

    ReplyDelete
  2. Huyu Mafuru ana umri gani? Very confusing!

    ReplyDelete
  3. Bora na hao wanaoshukuru, wengine hawashukuru kabisa. Hata ukimuuliza ulipata mchango hasemi. Urafiki na undugu wakati wa shida haufai. Watanzania tubadilike.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili (2) hapo juu unaeuliza muonekano wa Mafuru, ukiona mtu ana grow while look youth ni dalili za kuwa mtu huyo anaishi kwa discipline ya hali ya juu.

    Elewa kuwa kuwa vile ulivyo ndio mwenendo wako ulivyo:

    Kwamba: STAREHE IKIZIDI INAZEESHA! NA INACHANGIA KUPUNGUZA UMRI(LIFE EXPECTANCE).

    1.Huwezi kuonekana young wakati unatumia muda mwingi kwa ulevi!.

    2.Huwezi kuonekana young wakati unaendekeza ngono zembe!.

    3.Huwezi kuonekana young wakati unalala masaa machache!.

    4.Huwezi kuonekana young wakati uanjitwisha migogoro na kutokuelewana ,huku unaishi bila ya mpangilio wa mambo!.

    Kumbuka mambo manne (4) hapo juu ndio moja ya sababu zinazochangia watu ,KUZEEKA HARAKA, KUISHI MAISHA YASIYO NA RAHA YENYE TABU NA KUFA HARAKA!

    ReplyDelete
  5. Hehhhh,

    Mtoa maoni wa pili 2 na wa nne 4 hapo juu.

    kuwa na mwonekano uliokuwa very confusing kama ni Mzee au Mtu wa Makamo au Kijana,

    Mtoa maoni wa nne amejibu vizuri sana,

    hebu tuangalie mwenendo wa mtu ktk tasnia hizi nne alizotaja:

    1.ULEVI,
    -hebu tuangalie energy anayopoteza mtu akiwa amelewa, ndio mara nyingi mtu anaamka mchovu baada ya ulevi siku iliyopita(HANG OVER-sasa hii inaleta uzee)
    ndio mana mtu mwenye hulka ya ulevi daima huonekana mzee

    2.NGONO ZEMBE,(ngono isiyo na mpangilio)
    -hebu tuangalie mtu wa ngono zembe energy anayotoa baada ya mabao kadhaa ni kuwa ana bomoa sehemu ya mwili wake aliyoijenga kwa jitihada na kwa muda fulani, sio rahisi kurejesha kwa haraka kilichopotea ktk ngono zembe.

    3.KUWA NA MUDA MDOGO WA KULALA/ MAPUMZIKO
    -hebu tuangalie mtu akikosa mapumziko atakuwaje siku ya pili anachoka sana, uchovu na kukosa usingizi wa kutosha kunazeesha.

    4.MSONGO WA MAWAZO NA MIGOGORO YA MAISHA
    -hebu tuangalie vitu kama mikwaruzano,ghadhabu,kuchukia,kukasirika, vinaleta shinikizo la damu na magonjwa mengine ambayo licha ya kuua mapema yanamweka mtu ktk maisha yasiyo na raha na mara nyingi mtu anaonekana amezeeka wakati angali kijana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...