Na Woinde Shizza,Marangu

Serekali kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya wanyamapori Tanzania (TANAPA)wameombwa kuboresha mazingira ya mlima kilimanjaro ili watalii pamoja na wazawa wanaoenda kupanda mlima huo wasipate shida.

Hayo yalibainishwa na mtoto wa aliyekuwa brigedia wa kwanza kupandisha mwenge wa uhuru katika mlima kilimanjaro Nyirenda Alex wakati alipokuwa akiongea na Ripota wa Globu hii ya Jamii baada ya kushuka mlimani.

Alisema kuwa hali ya mlima ni nzuri lakini kuna vitu ambavyo vinapaswa kuboreshwa zaidi ili kuweza kuongeza wageni wanaotembelea mliama wetu .

Alibainisha kuwa moja ya vitu ambavyo serekali na Tanapa inatakiwa kujenga ni pamoja na sehemu ambayo watalii watatumia kupata chakula kwani wamekuwa wakipata tabu sana wakati wakila.

"unajua kiukweli mlima wetu ni mzuri vyoo ni vizuri ila kunatatizo moja hamna sehemu nzuri ya kula chakula na ukiangali huko juu mlimani kunanyesha mvua kila siku sisi juzi tulivyopanda ilifika mahali tukashindwa kula ata chakula cha mchana maana mvua inavyesha hamna sehemu ya kujifiicha ili tupate chakula kwakweli ni jambo lakusikitisha sana na ukilinganisha na hela ambayo serekali inapata kupitia mlima huu"alisema Alex.

Alibainisha kuwa katika miaka 20 iliyopita ambayo walipanda mlima huo kulikuwa na sehemu ambazo kipindi hicho watu walikuwa wanakoka moto ule mda wa kula au wakukutana kupata chakula wanaota lakini kwa sasa hamna,hivyo aliiomba serekali ijaribu japo kurudisha mfumo wa zamani wa kukoka moto ili angalau wageni wanaopanda mlima huo waweze kupunguza baridi kupitia njia hiyo na pia alisema iwapo watafanya hivyo watawaongezea wageni kwani kuna wageni ambao hawajawai kuona moto kama huo unawashwa msituni hivyo itakuwa ni kama miujiza kwao.

Alitoa wito kwa watanzania kujijengea tabia ya kutembelea mlima huo kwani upo kwao na nikitu cha maajabu sana kinachofanya adi wageni wanakuja kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuuona mlima huo tu.

"mimi kwakweli napenda kuwasihi watanzania wawena moyo wa kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini kwani na vya kwao wenyewe ,kwanini watu wanatoka nje ya nchi wanakuja kuangalia wao wenyewe wapo hapa hawataki kuja kuangalia kwakweli wawe na moyo wa kutembelea"alisema Alex

Kwa upande wa dadake Tima Nyirenda alisema kuwa anashukuru mungu wa sana kwa kupanda mliama huo ambao wao kwao ni historia kubwa na kumbukumbu kubwa ya baba yao mzazi ambaye alipandisha mwenge wa uhuru katika mliama huo.

Alisema kuwa wao walipanda mliama huo lakini hawakuweza kufika katika kilele ambacho ambacho baba yao alifika kwani kutokana na hali ya hewa iliwakwamisha ila aliaidi kuwa kwa kuwa huu ni mwanzo wanaamini kabisa katika kipindi kijacho cha mwaka ujao watafika kileleni .

"kwakweli tulikuwa tunahamu sana ya kufika katika kilele ambacho baba alifikisha mwenge wa uhuru enzi izo katika miaka ya 1961 lakini hatukufika tuliishia kibo ambapo tuliweza kutembea kilometa 4750 na katika mlima kilimanjaro mfano tungefika kileleni tungetakiwa tutembee kilometa 5685 kwa iyo tumebakiza kilometa 935 tu hivyo nathani mwaka ujao tutamaliza maana hii tumeanzisha mpango wa watoto wa Gwebe Nyirenda kupanda mlima kila mwaka"alisema Tima

Aliwataja watu ambao walikuwa nao katika kikundi chao cha kupand amlima huo waliomaliza kuwa ni rafiki wa babake Ameen Kashimiri,Rahimu Kashimir ,Paul Mason pamoja na Lorly Lavilla.

Alitoa wito kwa watanzani kujenga tabia ya kupanda mlima huo ambao ni kivutiio kikubwa duniania .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni vizuri kwa familia hii ya Nyirenda kumuenzi mzazi wao kwa njia hii na tunashukuru kwa ushauri wa kutuhimiza kutembelea vivutio vyetu.
    Kwa bahati mbaya sana mlima Kilimanjaro si mrefu kama ulivyosema na hakuna mlima mrefu hivyo dunian.
    Mlima Kilimanjaro una mita 5685 na si kilometa 5685,huwezi tembea kilometa 4750 kwa siku mbili unless wewe si binadamu halisi.
    Ni hayo to.

    ReplyDelete
  2. YangoringoriDecember 08, 2011

    Natumani ni vizuri walivyofanya watoto wa Nyirenda (Mmalawi) pamoja na huyo rafiki wa baba yao kashimir (Mhindi) yote hayo ni katika kuhitimisha shamrashamra za miaka 50 ya kutokuwa chini ya mtu mweupe. kitu ambacho ningetofautiana na mtoto wa kiume wa nyirenda ni wazo lake la kukoka moto holela holela juu ya mlima huo kwa watalii watakaokuwa wanaupanda.
    Nafikiri muda uliopita huenda kama alivyosema ilikuwa inaruhusiwa kukoka moto, na baadaye TANAPA na Serikali wakaona madhara makubwa ambayo yanaweza kutokea kama mlima ukishika MOTO.
    Mlima huo ni chanzo cha maji yanayotumiwa na wakazi wengi wa Kitanzania, na ni kivutio cha watalii si kwa urefu wake tu ila na kwa mandhari yake ya mimea tofauti tofauti kila unavyomaliza kilometa kadhaa. Sasa kama tukaruhusu kiholela ukokwaji wa moto, naamini iko siku tutalilia chooni, maana hatutaweza kuzima huo moto kwa mtindo wowote ule. hivyo tutaachwa na mlima usio na mandhari, na utakuwa mwanzo wa ukosaji maji na mvuto wa mvua.
    Kwa maoni yangu ningeiomba TANAPA na Serikali ishikilie Policy au taratibu iliyopo ya kutokuruhusu ukokwaji wa moto holela holela milimani humo.
    na kwa kumalizia ningeishauri TANAPA na Serikali ibuni utaratibu wa kujenga "Resting Posts". sehemu hizi za kupumzikia zitawawezesha wapandaji mlima wetu kuota moto or warming themselves huku wakijipatia chakula chao na vinywaji. DONT EVER ALLOW ANYONE TO MAKE FIRE AROUND AND ALONG THE WAY-UP TO THE TOP OF OUR MOUNTAIN. THAT SHOULD REMAIN AS "PROHIBITED". Hili limeeleweka na sila kujadili, maana madhara yake ni makubwa. nimewakilisha.

    ReplyDelete
  3. Mlima hatukuutumia vizuri hapo kabla,,,sasa ni muda muafaka kuanza kuvuna mapato yake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...