Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (wa pili kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Christopher Sayi (wa pili kutoka kulia) wakati wakielekea katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa wizara na waandishi wa habari ili kutoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia hali yake na kumwombea kupona kwa haraka wakati alipokuwa nchini India kwa Matibabu.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bashir Mrindoko na kushoto ni mtoto wa Maziri Mwandosya, Emmanuel Mwadosya.

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (kulia ) akizungumza na viongozi watendaji wakuu wa wizara hiyo na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia hali yake na kumwombea kupona kwa haraka wakati alipokuwa nchini India kwa Matibabu, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, viongozi wa dini na wa kisiasa ambao ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad , na Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi Watanzania kwa ujumla bila kujali Itikadi za kisiasa. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Gerson Lwenge .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hicho kichwa cha habari"Profesa Mwandosya akuzungumza na wafanyakazi....." hebu rekekebisheni

    ReplyDelete
  2. akuzungumza....duh!

    ReplyDelete
  3. hongera kwa kurud salama.

    ReplyDelete
  4. Ila safari hii Mzee uwe makini na madishi utakayo andaliwa,,jamaa hawataki watu wakweli wasije wakakungóa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...