Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin Goetzsche (kushoto), akiwawashia mishumaa wafanyakazi wa kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Makao Makuu ya TBL,jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kevin O'Flaherty (kulia) akiwasaidia wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwawashia mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika Makao Makuu ya TBL, jijini Dar es Salaam juzi.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani,katika Makao Makuu ya kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.
Meneja wa Kiwanda wa TBL, Bw. Rweyemamu (kulia) akimpatia Ofisa Usalama mahali pa Kazi TBL,Ismail Kalembo zawadi ya simu aina ya BlackBerry, baada ya kuwa mmoja wa wafanyakazi wa waliopima kwa hiari virusi vya Ukimwi.
Meneja Mauzo wa TBL, John Mgega (kushoto) akimpatia zawadi mfanyakazi Khadija Maulid ambaye ni mmoja wa wafanyakazi walioamua kwa hiari yao kupima virusi vya ukimwi.
Mama mhamasishaji vita dhidi ya UKIMWI,akimpatia zawadi ya bia mmoja wa wafanyakazi wa TBL.
Wanakamati ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwa upande wa TBL,wafanyakazi wa TBL,WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WAATHIRIKA WA UKIMWI
Bia si ndiyo kichocheo chenyewe haswaaaa.
ReplyDeleteMtu akishaujaza kichwani hapo sketi itakayopita mbele basi haitakuwa na salama.