Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea akimkabidhi sukari Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye mahitaji maalum iliyopo Masiwani Jijini Tanga, Bw. Omari Masukuzi, wakati mkurugenzi huyo alipotembelea shule hiyo kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya stadi za kazi na vyakula.
Vifaa ambavyo vimetolewa na TAKUKURU kwa shule ya watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo viziwi, wenye mtindio wa ubongo na walemavu iliyopo eneo la Masiwani Jijini Tanga, vifaa ambavyo vyote nina thamani ya shilingi 500,000 (Laki tano).
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea akiwa amepiga picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa shule yenye mahitaji maalumu iliyopo eneo la Masiwani Jijini Tanga, (kulia) ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Lilian Mashaka. (Picha na Mdau Mashaka Mhando).

 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya watoto wenye mahitaji maalum iliyopo eneo la masiwani Jijini Tanga, wakiwa wamehudhuria hafla fupi ya kukabidhiwa zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt Edward Hosea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. WATOO badala ya WATOTO. AJALI VIDOLENI¬¬¬¬¬¬¬¬

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...