Ndugu zangu watanzania, chuo cha Westminster kilichopo katikati ya jiji la london, UK, kila mwaka kinatoa scholarship kwa watanzania kusoma degree ya kwanza na ya pili bure (unalipiwa ndege kwenda london na kurudi Tanzania, malazi, chakula, ada yote na kila mwezi hela ya matumizi). 

Tatizo hizi habari tukipata hatupeani, mwisho nafasi kama hizi zinafutwa chuoni maana hamna wanaoziomba. Mi nilifanikiwa kuipata kupitia rafiki yangu, nami nimekuwa naitangaza na ntaendelea. Hii nafasi itasaidia kubadilisha maendeleo ya watanzania na Maisha yao kiujumla. Link hiyo chini inamaelezo yoote. 

Deadline ni mwakani April, so kama upo interested, tumia mda huu kudownload form za kuomba chuo, ukipata chuo, then unaomba scholarship, maelezo yapo kwenye website yao www.westminster.ac.uk link ni http://2009.westminster.ac.uk/study/international/country-pages/africa/tanzania
Goodluck
Evelyn Kaijage

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Hongera Evelyn kwa kumaliza na kuwa na moyo mzuri.

    ReplyDelete
  2. ukapata na mume pia..Hongera..Eve hivi ile blog yako mbona siioni siku hizi?embu iweke basi.

    ReplyDelete
  3. Thnx Dada Evelyn. Wewe ni Mtu katiaka Watu. n' you gonna be blessed for that...
    Tutaishughulikiaaaa

    ReplyDelete
  4. Mambo ya scholarship ni bahati tu, unaweza ukawa na matokeo mazuri usipate kitu. Ikiwa zipo nafasi mbili unategemea sote tuombe si itakuwa tunapotezeana wakati. Ingawa huwezi kushinda bahati nasibu kama hukucheza!!

    ReplyDelete
  5. Asante sana Evelyn kwa habari nzuri, wewe ni mzalendo wa kweli. wengine wanauchuna tu wanaambia ndugu zao only, keep it up, na hongera sana, naona umevaa joho hapo.
    adii

    ReplyDelete
  6. Asante kwa taarifa mdau! Ila jamani watanzania tujifunze kiswahili Fasaha. Neno likiandikwa tofauti linaleta maana nyingine kabisa. Mdaua badala ya kutuambia MALAZI, ameandika MARADHI. Maradhi ni magonjwa. Nani atapenda kupewa magonjwa?

    ReplyDelete
  7. That is great....Evelyne to think bout others! plz my appreciation!..I had not logging in by the way before some1 from Germany insisted for the same, I did and found so impressing, myself we look for Investment & Risk Finace MSc. Will try to contact you for further proceedures made you successfull...Thanks MICHUZI tooo!
    by hprincesaid@yahoo.com
    hashim.

    ReplyDelete
  8. lol...congratuation for you achievements Evelyne

    ReplyDelete
  9. That is great....Evelyne to think bout others! plz my appreciation!..I had not logging in by the way before some1 from Germany insisted for the same, I did and found so impressing, myself we look for Investment & Risk Finace MSc. Will try to contact you for further proceedures made you successfull...Thanks MICHUZI tooo!
    by hprincesaid@yahoo.com
    hashim.

    ReplyDelete
  10. Asante kwa habari nzuri, nimejaribu kuangalia application form yao siioni wanataka ni apply kwa njia ya UCAS amabayo nafikiri kwa Huku kwetu ni TCU ila wana mlolongo mrefu

    Application form nitaipataje?

    Asante

    ReplyDelete
  11. dahh we dada mungu akujaalie uwe na maendeleo zaidi.na uwe na moyo huo huo.

    ReplyDelete
  12. Asante sana Evelyn kwa taarifa hii muhimu

    ReplyDelete
  13. Safi sana dada coz wabongo wengi wanaroho za korosho huwa hawatoi habar km hizi..
    Ushauri kwa wale wenye malengo yakusoma nje..
    1.Jaribuni kufanya English test b4 km vile TOELF au IELTS coz vyuo vingi vinahitaji hio wakati wa appctn.
    2.jaribuni kutengeneza passport pia kabla,japo ni mara chache bt huwa baadhi ya vyuo wanataka kupi ya pass na co birth certificates.
    3.Andaeni motive lettes au statement of purpose coz almost scholarships zote huwa zinahitaji hii kitu,so nibora kua na draft yako kabisa ili hata km ukipata info.late unaweza kuwahi fasta kwavile kila kitu unacho tayari.
    4.Arrange kabisa referree wako km3 hivi coz kibongo bongo inaweza kuwa issue kupata hawa watu 7bu ni ile ile roho za korosho.

    Mdau wa Ubatani Nawakilisha.

    ReplyDelete
  14. asante sana Evelyn ni watu wachache sana wenye moyo kama wako. Ubarikiwe sana

    ReplyDelete
  15. Hiyo ni advertisement tu. Mimi ni graduate wa Westminster na hiyo scholarship niliomba sikuipata mpaka nikamaliza chuo. Jaribuni, mtaniambia. Hawa waingereza hawana hela kwa sasa.

    ReplyDelete
  16. It such a good idea.thanks a lot we will work out on this.

    ReplyDelete
  17. huu ni upotoshwaji -as far as I Know Scholarship ni kwa Master tu sio kama alivosema au degree ya 1 kiswahili ni master? na tena sio hao tu ulaya yote na bila scholarship ukiomba tu unakubaliwa bahati yako hasa scandinavia,lakini je mume amepata kweli? mi namtaka

    ReplyDelete
  18. uTANI PEMBENI...kWA MARA YA KWANZA KABISA NAKUTAKA NA MTOTO MZURI, TABIA NZURI, ROHO NZURIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII. Dada nimekuzimia ile mbaya. I WISH you were my wifyiiiiiiiie.
    Thank you.

    ReplyDelete
  19. Hii scholarship haipo kwenye yale masharti ya misaada ya Cameron?unaweza ukakuta sharti lakwanza iliusome ndiyo vile tena!!

    ReplyDelete
  20. Hapa hamna kitu ,Si rahisi mTZ wa leo kuwa na roho nzuri kiasi hicho

    ReplyDelete
  21. Mdau unayeulizia kama eveliyne ana mume? Ni kweli akiwa chuoni amepata mume na wameshafunga ndoa na kijana wa kitaliano. Pole yako na jaribu kutafuta mwingine. Hongera sana mtoto wa kihaya na endelea na moyo wako wa kujali na wengine.

    ReplyDelete
  22. Ni kweli, scholarships ni kwa MSc na PhD, undergraduate hawatoi. We jaribu tu, siwakatishi tamaa.

    ReplyDelete
  23. Mdau wa 17 kutoka juu : huu ni upotoshwaji-as far I know Scholarship...
    Mdau wa 2 kutoka juu ametubainishia kuwa tumeshampata Shemeji yetu (Mume) kwa Evelyne Kaijage, sasa na wewe unaesema unamtaka utakuwa Mume wa ngapi?

    Au unataka mambo ya kona?..Mnhh mimi hapo sipo!

    ReplyDelete
  24. thanx..bblsd

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...