Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) inakupa nafasi ya kuangalia kipindi cha Kipima Joto kilichorushwa na kituo cha ITV tarehe 11/11/2011 ambapo Mkurugenzi mkuu wa NHC Ndugu Nehemiah Kyando Mchechu kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC na benki ya Azania pamoja na mtaalamu wa masuala ya mikopo ya nyumba wakieleza kiundani mpango wa kuuza nyumba kwa wananchi kupitia mkopo wa Bank. 

kuangalia kipindi hicho tembelea mtandao wetu  www.nhctz.com na bonyeza kwenye alama ya youtube. Au tembelea moja kwa moja kwenye ukurasa wetu wa Youtube kupitia http://www.youtube.com/user/NHCTZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kama tutaweza kuona live online tafadhari mtuambie itakuwa ni saa ngapi muda wa huko Tanzania

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru,ingekuwa rahisi kama unavyoelezea ninanini asiyependa kuja kusoma uk.wewe siumeamua kujionyesha hapo ili watu wajue kwamba uko majuu?

    ReplyDelete
  3. mjomba komenti zangu zimeingia kapuni.

    ukisikia rushwa ndo hiyo manake ukisema ukweli, mwenye gazti hachapishi kuogopa kumtibua gulamali au kassim dewji.

    bongo media imejaa rushwa kupita kiasi. watu wengi huvamia fani hii ili wale rushwa na siyo kuhabarisha umma au kuelimisha jamii.

    ukijaribu kueleza hali halisi inayomsumbua mlalahoi, mhariri hutia kapuni kisa utmzibia kula yake.

    nd'o maana viongozi wengi huweka kando itikadi za uongozi na kujinufaisha wao wenyewe kwa sababu hakuna chombo wala mtu yeyote ataeweza kujaribu kuzungumzia vitendo vibaya atendavyo.

    vyombo pekee vingeweza kutokomeza usaliti huu ni vya habari. lakini hivyo ndiyo viko mstari wa mbele kuendeleza maovu hayo huku wananchi ambao nd'o tegemeo lao wakifa njaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...