Habari Ankal pamoja na Watanzania wote,
kwa mujibu wa takwimu ya jumuia ya kuangalia mambo ya Rushwa duniani, Tanzania tume-score 3 tu ambayo 0 ni mbaya na 10 ni nchi safi kabisa http://cpi.transparency.org/cpi2011/results/.

Tanzania tupo nchi ya 100 na tumescore 3 wakati kwa Africa Botswana ni ya 49 na imescore 5 imeshinda nchi zote za Africa,na pia nchi nyingi za Ulaya ikiwemo Greece ikiwa ya 80 hatujaachana nayo sana, na kwa Afrika nchi ya Rwanda inafuatiwa na Visiwa vya Seychelles ya 50 imescore 4.8. na Somalia ni ya mwisho kabisa.

Napenda kuwakilisha hili hata hivyo Kwa Africa tupo mbali sana tumejitahidi.

Ahsanteni

Mzee wa statistic na
Quantitative method
U.K

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. mijitu mingine, yaani kwa sababu nchi za ulaya kadhaa zimejaa rushwa kama sisi kwa hiyo we are doing good?

    ReplyDelete
  2. kichwa cha hapari kinapotosha. kinaonyesha tanzania ni nchi ya 100 ikimaanisha iko mbali na rushwa wakati iko karibu na rushwa kamili.

    ReplyDelete
  3. inamaanisha ni wa 100 kati ya 180 kwa usafi.

    hii inaonyesha sisi mafisadi mno, rushwa za fedha, ngono, n.k.

    ReplyDelete
  4. tusijidanganye hata kidogo kwa kupenda kusifiwa,wakati wa uchaguzi watu walijipanga kwa foleni usiku kwenda kuchukua rushwa,bara barani,hospitalini,vyuoni,mashuleni mpaka makazi hali haitamaniki,
    mi sioni nini cha kushangilia humu wakati ukweli tunaujua wabongo wenyewe.

    ReplyDelete
  5. Terrible lakini kila kitu ni relative.Hao wanaotuambia kuwa nchi yetu ni rushwa kama nini, wao pia wana matatizo ya rushwa. Jee unakumbuka nchi iliyotoa rushwa ili bongo inunue radar, jee umesoma magazeti kuwa polisi UKerewe walikuwa walipwa kutoa habari, jee wasikia rushwa huko Afghanistani?Hii yote ni nyani kumcheka tumbili.

    ReplyDelete
  6. Lijitu lingine bwana, linashindwa kuelewa kuwa mto amada analinganisha africa?

    ReplyDelete
  7. bongo tambarareeeee...

    ReplyDelete
  8. Kuna tofauti kati ya rushwa na ufisadi.. Hizi statistics ni za uzushi.. North Korea hakuna rushwa kabisa nashangaa iko karibu ya mwisho.. kwa nchi za Afrika Tanzania inafanya vizuri sana nenda tu kwa watani wetu hapo wakenya mkajionee.. ndiyo rushwa ni adui wa haki ila siyo lazima rushwa ni adui wa maendeleo.

    ReplyDelete
  9. Nilikuwa nikijaribu kutafuta 100 inamaana gani lakini niliposoma hiyo website inasema "Corruption perception index". Hapo haimaanishi chochote cha maana. Pia nani aliyeulizwa, wangapi walioulizwa? Kwa uzoefu wangu tafiti kama hizi kwa Tanzania huwezi kupata majibu sahihi maana waTZ wengi wana itikadi za vyama, ukabila, umajimbo na sifa zenginezo.

    ReplyDelete
  10. wee ni sifuri kabisa umeona nayo hii ni habari ya kuleta humu lengo lako ni ili mafisadi wazidi kutafuna hadi tuwe namba moja. ovyo sana!

    ReplyDelete
  11. bongo !

    laki na nusu net pay , watoto wanne , mdogo wa mkewe na nyumba ni ya kupanga , basi mbili kufika kibaruwani kwenda na kurudi , hela ya mitihani kwa watoto wa shule kila j'mosi achilia mbali tuition fee pia , - watoto hawajala , yeye mwenyewe mlo wa mchana kila siku awapo kibaruwani ...!!! ???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...