Wakati wa kuadhimisha Miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza wakishirikiana na Chuo kikuu cha mji Coventry wanapenda kuwatangazia wadau wote wa elimu kuwepo kwa Scholarship sita maalum za masomo kwa watanzania ambazo zimetolewa kutoka katika Chuo kikuu cha Coventry katika nyanja zifuatazo:
1. MSc Oil & Gas Management
Coventry Campus
Kuanzia Septemba 2012
2. MBA Oil & Gas Management
London Campus
Kuanzia April, July, Septemba 2012
3. MSc Finance & Investment
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba 2012
4. MBA Logistics
IAA Dar Campus
Kuanzia Septemba
5. MSc Finance & Investment
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012
6. MBA Logistics
IAA Arusha Campus
Kuanzia Septemba 2012
Jinsi ya kujiandikisha, tembelea tovuti ifuatayo hapo chini:
Mbali na hapo Ubalozi wetu ukiwakilishwa na Balozi Mh Peter kallaghe, Chabaka Kilumanga na Allen Kuzilwa walipata fursa pekee ya kukutana na kumpongeza afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ndg. Semu Mwakyanjala ambaye pia ni mwanafunzi wa shahada ya Pili( Masters Degree in Communication, culture & Media) katika chuo kikuu cha Coventry alieshinda tuzo ya kuandika insha kuelezea jinsi gani nchi ya Ujerumani itakavyokua mwaka 2051.
Aidha Mh. Balozi Kallaghe alimpongeza sana Afisa Semu kwa juhudi zake kwa kufanikiwa kushinda tuzo hii na kuiletea heshima Tanzania Ughaibuni na kuwahamisisha watanzania wote kusoma na kufanya kazi kwa bidii zaidi. Wakati akiongea na waandishi wa Habari afisa Semu alianza kwa kutoa shukrani kwa familia yake, wafanyakazi wenzake kutoka TCRA na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kumwezesha kufikia hatua aliyopiga leo.
kwa maelezo zaidi wasiliana na ubalozi wetu hapa London 00 44 20 7569 1470
Tafadhalini watanzania wote chukueni hii nafasi mapema iwezekanavyo kwa wale wote mnaopenda kujiendeleza kimasomo.
Asanteni Sana,
URBAN PULSE CREATIVE
Tunashukuru Ubalozi wa Tanzania Uk kwa habari njema ingekua sehemu nyingine ishu ingepita kimya kimya juu kwa juu kwa baadhi ya watu. Lakini ubalozi wa Uingereza kitu wazi wazi kwenye meza. Safi sana Mh Balozi Kallaghe, Chabaka na timu yote ya Ubalozi. Haya sasa wadau kazi Kwetu tuchangamkie dili.
ReplyDeletehaya ndio mambo tunayotaka kusikia Hongera sana Mh Balozi Kallaghe, Chabaka na timu yote ya Ubalozi wa Uingereza . Jamani Balozi za nchi zingine na nyinyi muige mfano huu mzuri ili mtusaidie walala hoi
ReplyDeleteHongera sana Mtanzania mwenzetu. Tatizo tulilokuwanalo watanzania huwa hatujiamini-lakini kuna mambo mengi sana tunaweza.
ReplyDeleteMabalozi wawili Huyu wa UK Peter Kallaghe na Mzee Ombeni Sefue wa UN-TANZANIA kule Marekani kweli wanajituma BIG UP!
ReplyDeleteWENGINE MFUATE NYAYO HIZI!!!!!!!