Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la Hai, Mh.Freeman Mbowe akimkaribisha mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mh. Godbles Lema kuchangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa KKKT usharika wa Nshara Moshi.
Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi akichangia katika harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Bw. Reginard Mengi akimueleza jambo Mh Mbowe kabla ya kuanza kwa harambee.
Mh Mbowe akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Rambo uliopo Machame wilayani Hai.
Wabunge wa viti maalumu Chadema pia walikuwepo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Wadau, naomba kuuliza hili vazi la kanzu na barkashia inaweza kuvaliwa na mtu yeyote ambaye sio mwislam? nilipenda tu kujua ndugu zangu

    ReplyDelete
  2. wamechanga bei gani bei gani mbna hatuambiwi au laki laki

    ReplyDelete
  3. kwani kuna ubaya gani?

    ReplyDelete
  4. nijuacho mie ni kuwa vazi hili si la kiislamu, bali ni utamaduni wa kiarabu. Pia kuna baadhi ya makabila hapa nchini huwa yanatumia vazi hili katika shughuli maalum, kama vile Wahehe na Wahaya

    ReplyDelete
  5. hilo ni vazi tu kama mavazi mengine isipokuwa waislam wamelichagua vazi hilo kuwa ndio vazi rasmi lakini haimaanishi kuwa haliwezi kuvaliwa na watu wa madhehebu mengine

    ni wengi wasiofahamu kuwa hilo ni vazi kama mavazi mengine

    ukiangalia hata kule nchi za warabu kuna baadhi ya nchi zina madhehebu ya kikristo na kiislam lakini wote wanatumia vazi la kanzu na kofia bila kujali madhehebu yao

    ni vazi zuri sana na nchi za warabu walilichagua kutokana na joto jingi la nchi zao
    unapovaa nguo kama kanzu sehemu za joto hukupunguzia kuchomeka na juwa kali na hata hupunguza joto mwilini ni tofauti na mavazi mengine.

    mdau ulieuliza swali itakuwa umenifahamu vyema

    ReplyDelete
  6. ndio inawezekana

    ReplyDelete
  7. kama sio vema kuvaliwa na mtu wa dini nyingine vazii lenyewe hukataa kumuingia ninamkataa kabisa kama si vema kulivaa. ila kama halina shida aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaamtu anachichana kama kawa

    ReplyDelete
  8. Vazi la kanzu mtu yoyote anaeza vaa. Sasa mwarabu mkiristo anavaa nini?

    ReplyDelete
  9. Ndio hilo ni wazi .....ila mara nyingi wanaolivaa huwa waislam ila hukatazwi utapovaa hili vazi zaid ya kukuweka wewe kuwa mzuri na kupendeza

    ReplyDelete
  10. KIASI AVAE KANZU KILA SIKU,MASHALLAH!!

    ReplyDelete
  11. Ndugu yangu sio lazima uwe muislam ndio uvae kanzu,mbona maaskofu na mapadre wanavaa kanzu na kibandiko kichwani?Kanzu ni vazi la awali(kale)la watu wa katikati ya dunia

    ReplyDelete
  12. Jibu la kanzu ni vazi tu kama vazi lingine ingawaje waisilamu ndio vazi muhimu kwetu.Kwani tukiangalia nchi za kiarabu baadhi yao kuna wakiristo vilevile lakini unaweza kumkuta kavaa kanzu.Nimeshawahi kuishi mji mmoja huku UK na Mzanzibari mkristo na mara nyingi hasa siku akiwa haendi kazini na siowakati wa baridi huvaa kanzu na kwamba amezoea na anajisikia "confortable".Lakini tukija kisiasa hapo mzee Mbowe utakuwa unadanganya Umma.Na ningewaomba waisilamu wawe waangalifu na wasije fanya makosa mengine kama walio fanya wazee wetu kwa kudanganyika na mwisho kutawaliwa na kunyang'anywa mpaka jumuia za kiisilamu.Kwani siasa leo hii ni kuvutia watu leo na kesho tukiwapa kura unapigwa na butwaa.Kuna mbunge mmoja wa Mwanza jina nimelisahau tena wa CDM alienda kuwaomba waisilamu kura na akawaahidi kuwasaidia kurudishiwa shule za kiisilamu zilizotaifishwa na Mwalimu Nyerere,na amini usiamini alivoshinda akawatangazia Umma kwamba atahakikisha shule zote zinabakia kwa serikali na zitumeke kawaida na zisirudi kwa waisilamu.Sasa kazi kwenu tumeumbwa na akili na tuzitumie.

    ReplyDelete
  13. Kwani kulivaa kuna shida gani? Nani anakataza kuvaa kanzu au kofia? hayo ni mavazi kama mavazi mengine. Acha udini wewe mdau hapo juu.

    ReplyDelete
  14. Hawa jmaa wasanii tuu wanaiga staili ya mchonga (NYERERE) alipokuwa anataka kuwachota WAISLAM hanatofauti na KINYONGA, Kinyonga akikuona umevaa bleu na yeye anageuka BLEU akitokea mtu amevaa nyekundu anbadilika haraka na kuwa mwekundu wameona staili ya maandamano si nzuri kuingia IKULU sasa wanakuja na staili ya AINA YAKE wakiingia IKULU UTAONA MATOKEO yake(SHANGARORO-USA).

    ReplyDelete
  15. Mdau hapo juu...vazi la kanzu si kwa waislam na wala utakapoona mtu kavaa kanzu usimdhanie kuwa ni muislam.

    Oneni tofauti mandugu, harambee ya kanisa inafanyika wapi na harambee ya msikiti inafanyika wapi. Kiuhalisia upande mmoja katika jamii yetu umeachwa nyuma sana, ni jukumu letu watanzania wote kuhakikisha wote tunakwenda sawa pasi na kuangalia itikadi za kidini,siasa nk.

    ReplyDelete
  16. Hehehe, kweli waisilamu tunajizalilisha wenyewe; Embu checki tofauti ya harambe ya wakristo na ya waislamu - wako chini ya mti na mahema eti..

    ReplyDelete
  17. NINYI wABONGO HIO NI NGUO TU, KAMA SUTI AU BaZEE sio UISLAM.

    temeeni duniani acheni ushamba yote hio nio sababu ya kukjua tanzania tu hata maputo mtu nhajafika .

    ReplyDelete
  18. Anonymous wa kwa kwanza, tuna wasiwasi na uraia wako! For any true tanzanian who was born and grew up here, where Christians and Mslims are making the majority and share lots of things in common must have at least an idea that what so called 'kanzu and barahashia' and even suits have nothing to do with any of these two religions, it's among the effects of colonialism in our culture!...Ukijisikia kuvaa mkuu vaa sana!..wasikutishe!

    ReplyDelete
  19. ISINGEKUWA MTU WA MWANZO KUULIZA SWALI ALILOULIZA ILI KUDIVERT MAWAZO YETU PANGEKUWA PATAAMU. KUCHANGIA WAACHE WACHANGIE KWANI YOTE NI PUBLICITY. PILI HII NAONYESHA WAISLAM TUKO WEAK. KAMA KUCHANGISHA WAACHE ILA SIASA YA CHUKI WAMUMINI WADiNI ZOTE MBILI WATAHADHARI NAZO.

    ReplyDelete
  20. eti vazi la kanzu ni vazi tuu...hovyoo..someni maandiko kwenye biblia yenu..HILO NDILO VAZI TAKATIFU..!

    ReplyDelete
  21. Ndiyo, eeeh bwana, bra, bra, kanzu bra, kibandiko bra, bra! bra! udini,bra, mchonga bra braaaa,br! br! eeh.

    ReplyDelete
  22. Mwacheni Freeman Mbowe avae kanzu, yeye ni Mwana Siasa na Kiongozi wa watu, ktk Chadema wapo Waislamu amefanya Ustaarabu na Uungwana wa hali ya juu kuwajali Waislamu kwa kuvaa mavazi kama wao!

    UNAONA WAKRISTO WALIVYOKUWA WAKOROFI?

    ReplyDelete
  23. Mmeona Wakristo ktk Chadema walivyokuwa Wadini?

    Viongozi wenu waelewa sana ila ninyi wanachama mgongo wazi, ndara mkononi mnaichukulia Chadema kama Kanisa!

    Kwani ktk CHADEMA hakuna Waislamu?

    Ahhh Mbowe kuvaa kanzu imekuwa mgogoro!

    ReplyDelete
  24. Chadema mmeona Kiongozi wenu alivyo pevuka kisiasa na kujaa busara sasa?

    Unapoenda Iringa au Arusha kuongea na wenyeji utavaa mgolole ili kuwaheshimu wakazi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...