TAASISI ya Unit in Diversity Foundation (UDF), imekabidhi Msaada wa baiskeli za walemavu 30 zenye thamani ya sh. milioni tisa kusaidia waathirika wa mafuriko mkoani Dar es Salaam. Msaada huo umelanga kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kambi za waathirika wakaoshi. Akikabidhi msaada huo jana kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Eliya Utandu, Mratibu wa UDF Enock Bigaye, alisema baiskeli hizo zitagawiwa kwa walemavu wenye mahitaji katika halmashauri zote tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala. Alisema UDF ambao ni mdau mkubwa wa walemavu nchini, imeguswa na maafa hayo na kwamba, baiskeli hizo zitawawezesha kuwasaidia kutoka eneo moja kwenda jingine. “Ni maafa makubwa kwa taifa na walemavu wengine wanaishi kwenye maeneo yaliyoathirika. UDF tumetoa msaada huu ili uwasaidie na tutaendelea kuwawezesha ili kuhakikisha wanakuwa salama daima,” alisema Bigaye. Akipokea msaada huo Ntandu, aliishukuru UDF kwa kuwajali walemavu kwa kuwapatia misaada mara kwa mara na kwamba, huu wa baiskeli umekuja kwa wakati muafaka. Alisema serikali itahakikisha msaada huo unawafikia walengwa na kutumikakama ilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa taasisi hiyo. Kwa upande wake Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan ambaye amesaidia kufikishwa kwa msaada huo, alisema jamii na serikali kwa ujumla haina budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na UDF. Alisema katika jimbo lake kuna walemavu wengi walioathirika na mafuriko huku wengine wakiwa na mahitaji mbalimbali na kwamba, msaada huo utakuwa mkombozi. “Kwangu kuna walemavu wengi wameathiriwa na mafuriko, msaada huu utawapa nafuu ya kuishi kwenye kambi ambako serikali imewahifadhi kwa sasa,” alisema Azzan. Pia, alisema atakuwa bega kwa bega na UDF katika kuhakikisha walemavu nchini wanawezeshwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili. Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA), Nicholaus Kihwelo, alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka wakati walemavu wengi wakihangaika kwenye kambi za waathirika. “Walemavu ndiyo wenye nchi, vikitokea vita, mafuriko na maafa mengine hawawezi kujiokoa na wala hutawaona wakikimbia. Tunaendelea kuishukuru UDF kwa kutusaidia,” alisema. |
Home
Unlabelled
UDF YAkabidhi msaada wa baiskeli za walemavu WALIOKUMBWA NA MAFURIKO DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...