Rais Dkt. Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa maadhimisho ya SIKU YA UKIMWI Duniani ambnapo yeye na Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush (aliekaa kushoto) walishiriki katika mkutano kwa njia ya mtandao (Tele-Conference) na mkutano mwingine katika Chuo Kikuu cha Washington huko Marekani. Hii ilifanyika katika Taasisi ya Saratani katika Hospitali ya Ocean Road,jijini Dar es Salaam akiambatana na Mwenyeji wake
Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush akihutubia wakati wa hafla  huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete akisikiliza 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) akiteta jambo na Mgeni wake Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush wakati wa hafla hiyo
Rais Mstaafu wa Marekani,Mh. George W. Bush akiwa na Mwenyeji wake Rais Dkt. Jakaya Kikwete wakati wakiiingia katika  Hospitali ya Ocean Road walikotembelea Taasisi ya Saratani.
Baadhi ya wadau wakipata Taswira wakati wa hafla hiyo.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na aliyekuwa Rais wa Marekani Mh. George W. Bush na mkewe Laura Bush wakizungumza na mmoja wa wagonjwa wa kansa ya funganyonga pindi walipofika kwenye wodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road,Jijini Dar es Salaam.
Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete na aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush na mkewe Mama Laura Bush wakiwa pamoja na wagonjwa wenye VVU / UKIMWI Sara Daudi, Amina Assenga na Freddy Mwasongola.Picha na Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Jamani Watanzania wote na Raisi wetu JK tafadhali sana...George W. Bush asipewe Kigamboni kama ilivyosemwa kipindi cha nyuma, TUTAKUWA TUME KAIDI sera yetu ya ARDHI!

    ReplyDelete
  2. Uranium inatupa umaarufu!

    ReplyDelete
  3. Vp Al-shabab hawapo tena Tz?
    Hahaha..wabaongo bwana..yani kwakukuza mambo rafiki yangu dah..sasa Al-shabab wanavichaa waalipue Bongo wakati hawana interest yoyote.
    Hapa naongelea issue ya kamanda Kova kusingizia Shabab ktk issue ya maandamano wakati hamna uhusiano wowote.

    ReplyDelete
  4. Pamoja na watu kumsema sana Bush lakini amesaidia sana Afrika.

    ReplyDelete
  5. Bush is the man. Mtu powa sana huyu.Bongo unafiki tu kusema watu vibaya. Jamaa alikuja akaacha million mia saba....sasa katuweka LIVE CNN, FOX N.K. Mnasema mtu mbaya..."majungu si mtaji" Banza stone.

    ReplyDelete
  6. UZA UZA UZA NA BAKABURI YA KINONDONI YAHAMISHE SEHEMU ILE IUZWE.

    hahahahahahah Tz TAMBARARE

    ReplyDelete
  7. Mtu anaweza akawa mwema sana na ni mtoaji mchango mkubwa akiwa ktk nyumba za ibada...halafu mtu huyo huyo akatuhumiwa ujambazi!,,,mpo hapo?

    ReplyDelete
  8. Enhee Repulbican ndio CCM ya Marekani?...naona mama Laura Bush amepiga rangi za JEMBE NA NYUNDO!

    ReplyDelete
  9. Inaonekana mgeni wetu amevutiwa na hapa kwetu kwa safari yake ya mara ya pili,,,kama atatoa ushahidi au tamko kujitetea dhidi ya anavyotuhumiwa, yuko huru aje tuishi naye anakaribishwa!

    ReplyDelete
  10. Ni vigumu sisi Wananchi wa Tanzania ki maadili kumkubali kirahisi au kuwa na ukaribu na mtu anaesemwa vibaya!

    ReplyDelete
  11. Mdau wa nne kutoka juu Bush amesaidia Afrika!...hizi ndio zile mtu ktk maeneo ya ibada anakuwa mstari wa mbele, lakini mtu huyo huyo ana tuhumiwa ,ana lalamikiwa ,ana utitiri wa RB na Samazi za kuitwa mbele ya sheria!

    ReplyDelete
  12. Unaweza ukawa Sheikh mzuri au Padre Mzuri lakini ukawa mtu wa misala kibao!

    Nakumbuka palikuwa na Askofu mmoja ambaye jina lake likaendana na wasifu wake,,,alikula hela za asasi kibao ikiwemo Nyerere Foundation,,,aliishia kufungwa na jina lake anaitwa MUTAFUNGWA!!!.

    ReplyDelete
  13. Mangi wa KiboshoDecember 03, 2011

    Hivi Bush ni mjomba wetu? tujiulize anataka nini Tz!!!! wallah! kuna kitu anataka !

    ReplyDelete
  14. mhmmm no comment

    meggie

    ReplyDelete
  15. Wajinga hapa wanyamaze; hivi Bush alivyoweza kuongoza Marekani kuwa mstari wa kwanza kusaidia wagonjwa wetu wa ukimwi na maisha ambayo kutokana na jitihada hiyo yameokolewa hatulioni? Mbona sisi wepesi wa kulaumu tu! Barabara za Millenium Challenge Account vyote unadhani vingejengwa kwa maneno tu? Maneno na matusi yangekuwa gurudumu la maendeleo wachangiaji hapa wangekuwa dunia nyingine! Mungu ibariki Tz na watu wake!!!

    ReplyDelete
  16. Hivi bush mtamfananisha na Obama? Obama ni hopeless kabisa yaani hata si kutegemea

    ReplyDelete
  17. hahaha AMNEST WANAMTAFUTA MUUAJI WA WAIRAQ WASIO NA HATIA
    ACHENI KUMPA SIFA SHETANI KWENYE NYUMBA YA IBADAA.

    ReplyDelete
  18. Mkulu fanya fanya hima tubadilishe Nyerere International Air port iwe Kichaka International Air Port.

    ReplyDelete
  19. Hapa wadau lazima muelewe. Nasisitiza kuwa LAZIMA. Kuna Viongozi wawili hapa. Mmoja mwenye nguvu sana na mmoja mnyonge sana, lakini mwenye haki. Mwenye nguvu akiomba kitu myonge lazima akubali haraka sana, maana akileta ubishi basi mwenye nguvu ata-export demokrasi kwenye nchi ya mnyonge. Je, tutaweza kusimama? tutakuwa salama?
    JK anaplay smart!
    Hawa watu ndivyo walivyo, ukijifunza historia ya dunia hii utagundua kuwa wao wanakwenda nchi yeyote duniani wakati wowote, na wanakaa kwa muda wanaotaka, wanasema wanachotaka, na wanachukuwa chochote wanachotaka. Ukilalamika wanakuzulia jambo. Je, nyinyi/sisi tunaoandika-andika hapa bila kufikili kwa kina tunaweza kumtetea JK? au TZ? au yatakuwa yaleyale ya Libya?
    Fikilini sana ndugu zanguni, wenzetu wana umoja, sisi tumeparaganyika, kila taifa linakwenda kivyake.
    Ukifanya kazi yoyote ya kukusanya pesa muajili mwenye busara atakushauri wazi kuwa siku yoyote akija mtu na silaha na akakwambia umpe pesa, mpe. Usibishane wala usianzishe kurupushani. Maana uhai ni bora kuliko vyote. Kwa hiyo basi huyu mheshimiwa mwenye nguvu muache ajipatie anachotaka kutoka hapa kwetu kwa sasa. Kwa kuwa kila jambo ni wakati, basi atakachokichukuwa leo hii muda utafika atakirudisha.
    MUNGU UIBARIKI TANZANIA NA AFRIKA.
    bloger usibanie maoni yangu, asante.

    Asanteni wadau.

    ReplyDelete
  20. Anony wa kumi na saba toka juu, umegonga nyudo kwenye kichwa cha msumali. Huyu jamaa, kwa sasa hivi hawezi kwenda nchi yoyote ulaya, Watakamata! Ila TZ oooh karibu muheshimiwa.

    ReplyDelete
  21. ahhh! uranium weee! Bush kaja kuichota kiulaiiinii, kama anchota mchele wa kuonja sokoni mbeya!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...