Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akiongea na waandishi wa habari hapo pichani wakati wa kumkabidhi rasmi Vodacom Miss Tanzania Salha Israel gari aina ya Jeep Patriot yenye thamani ya shilingi 72 Milioni,kulia Meneja Masoko wa CFAO Alfred Minja ambao ni wadhamini wenza.
Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa akimuelekeza jambo Vodacom Miss Tanzania Salha Israel wakati wa kumkabidhi rasmi gari aina ya Jeep Patriot yenye thamani ya shilingi 72 Milioni.
Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akipokea funguo ya gari aina ya Jeep Patriot kutoka kwa Meneja Matukio na Udhamini wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw. Alfred Minja. Gari hiyo ina thamani ya shilingi 72 Milioni.
Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akionyesha funguo ya gari aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi milioni 72mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Udhamni na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa wa pili toka kulia kama ishara ya makabidhinao ya zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.Kulia ni Mkurugenzi wa Lino Agency waratibu wa shindano hilo la Vodacom Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga na mwengine anaeshuhudia ni Meneja Masoko wa CFAO wadhamini wenza wa shindano Bw. Alfred Minja.
Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akifungua mlango wa gari lake aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi 72 milioni tayari kwa kuondoka nalo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa hayupo pichani,Ikiwa ni zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.
Vodacom Miss Tanzania Salha Isarel akiondoka na gari lake aina ya Jeep Patriot lenye thamani ya shilingi 72 milioni mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa hayupo pichani,Ikiwa ni zawadi ya ushindi kwa kutwaa taji la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika shindano lililofanyika Septemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera sana kwa Miss Tanzania kukabidhiwa zawadi yake.Kwa kamati ya Miss Tanzania natoa ushauri kuwa Miss atumikie kwanza taji lake na kisha aende kushiriki Miss World.Sababu ni kuwa akienda kule ataweza kueleza shughuli za kijamii alizozifanya wakati akiwa na taji la Miss Tanzania tofauti na sasa ambapo anaenda muda mfupi baada ya kuchaguliwa.

    ReplyDelete
  2. ndugu wewe uko wapi? ameshakwenda mashindano miss world.

    ReplyDelete
  3. Watu wengine kwa kukurupuka. Sasa wewe anony wapili hapo juu umetafakari kabla ya kujibu au ulikuwa unajisikia tu kushushua mtu.?!Matokeo yake wewe ndio kituko.

    ReplyDelete
  4. anin wa kwanza ni kweli kabisa usemayo.. hawa Miss Tz nasikia wamekwisha sahuriwa sana kuhusu hilo lakini wanajidai wanajua sana hawataki ushauri wa mtu eti wana uzoefu..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...