Katibu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi amewataka wahitimu na wale wote wanaopeleka maombi ya nafasi za kazi katika Sekretarieti ya Ajira kuwasilisha vyeti vyao halali na kuachana na tabia ya kutumia vyeti vya kugushi maana pindi watakapobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Daudi amesema hayo leo, ofisini kwake jijini Dar es Salaam alipokuwa akihojiwa na baadhi ya Waandishi wa habari.

Amesema ameamua kutoa tahadhari hiyo hivi sasa baada ya ofisi yake kukamilisha utaratibu madhubuti wa kuweza kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote watakaobainika kugushi vyeti katika kupeleka maombi ya kazi.

“Napenda wananchi wajue kuwa kutokana na njia tunazozitumia katika mchakato mzima tangu kutoa matangazo, kufanya usaili hadi kufikia hatua ya kuwapangia vituo vya kazi wale waliofaulu katika usaili kuwa za kisasa ni rahisi kuwabaini wale wote watakaotumia vyeti vya kugushi katika kuomba nafasi za kazi” alisema Daudi.

Aidha, amesema kuwa kazi ya kukagua vyeti vya kugushi ni ya kudumu kwa mujibu wa mfumo na taratibu zilizopo na litaendelea kufanyika kwa fani zote na ngazi zote za nafasi za kazi zinazotangazwa ili kuweza kutoa fursa za ajira kwa wale wanaostahili tu.

Amehitimisha, kwa kuwataka wale wote wanaopeleka maombi ya kazi katika Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira kuwa wakweli kwa kuwasilisha vyeti vyao halisi maana Ofisi yake haitasita kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria mtu yeyote atakayebainika kutumia vyeti vya kugushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. muanze kuwatahazarisha/kuwaelewesha viongozi kwanza maana likipita gwaride leo la kukagua vyeti maofisini/wizarani mbona watabaki wafagizi tuu

    ReplyDelete
  2. Baada ya maandalizi hayo onyesheni ukweli na uwazi kwa wale waiokwisha ajiriwa. Sio siri kazi itakuwepo kwelikweli.

    ReplyDelete
  3. ahhhhaa apo itabidi waje hata huku uk kwenye balozi yetu kwani ni aibutupuu kukutana na wafanyakazi ambao hawana confidence ya kuweza kuendeleza mazungumzo ya zaidi ya dakika tano!!!

    ReplyDelete
  4. Duhh imekaa vizuri ila zoezi limechelewa sana,,,serikalini ndio kuna upukupuku wa watumishi Vilaza na Vihiyo!

    Zoezi hili lisiwe kwa wanaoomba kazi sasa bali lifike hata kwa wale waliopo makazini wahakikiwe upya!

    Wengi wamepita kwa njia za kufoji foji tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...