viongozi wa Serikali na wananchi wa kijiji cha Nduu,Mombo mkoani Tanga wakitafuta namna ya kuwatoa askari wa kikiso cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Tanga mara baada ya gari lao lenye namba za usajiri PT 2000 aina ya Toyota Landcrusser kuacha njia na kupinduka bondeni wakati wakiwa kwenye ziara ya Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal iliyotokea jana eneo la Nduu Mombo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani Tanga wakipata msaada wa kuvutwa kutoka kwenye bonde baada ya gari yao kuacha njia na kuelekea bondeni wakiwa kwenye msafara wa ziara ya makamu wa Rais Dkt. Mohamed Balil eneo la Nduu Mombo lililo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe jana na kusababisha vifo vya kwa askari wawili wa kikosi cha hicho.
Mmoja wa Majeruhi wa katika ajali hiyo akipata matibabu katika hospital ya Magunga wilayani Muheza.
Wananchi wa Mombo na viongozi wa Serikali wakiangalia ajali hiyo mbaya iliyotokea eneo la Nduu Mombo na kupoteza maisha kwa askari wawili na kujeruhi wanne wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) Mkoa wa Tanga wakati wakitokea Lushoto kwenye ziara ya makamu wa Rais Dkt. Mohamed Bilal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Pole kwa wanafamilia waliopoteza vijana hao,pole kwa majeruhi.Ila tuseme ukweli hii misafari ya viongozi wakubwa wa nchi gari huwa 'zinatembea' ni balaa.Kuanzia gari la kwanza hadi la mwisho;

    David V

    ReplyDelete
  2. Mimi siju kama Tanzania tuna maadui wengi kiasi hichi.Msafara inakuwa na magari mengi na askari wengi sana.Ila raia akipiga simu kuomba msaada ahata wa imeregency tu kama wizi na nakadahlika hawaonekanai.Sasa mimi sielewi wako kwa ajili ya wananchi au kwa watu wote?
    Poleni waliofiwa na askari mjifunze kwa makosa.

    ReplyDelete
  3. muschi b.c.January 28, 2012

    sumatra je mlikagua magari kabla ya safari!!
    Ajali hutokea popote na si mabasi ya abiria tu. poleni Familia za wafiwa poleni na ndugu zetu majeruhi.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana wafiwa.
    Africa hivi ni kwanini misafara hii huenda kasi hata kama nchi zenye amani kama Tanzania?
    Nini wanakimbia???? Je wanaogopa kukamatwa na wananchi?? kwani wao ni wezi??? au ufisadi???
    Hizo nchi mfano za ulaya wakati mwingine hata huwezi kujua kuna kiongozi anapita, hakuna kukimbizana, mwembwe wala nini.
    Nafikiri hawa viongozi wana lao jambo, wanajishuku ndio maana mbio zito hizo.

    ReplyDelete
  5. Hii ni matokeo ya mwendo kasi mkubwa.


    Usalama ni umakini na kuchukua tahadhari zaidi.

    Usalama wa Msafara wa Kiongozi hauwezi kuhakikishwa kwa mwendo kasi!

    ReplyDelete
  6. Hivi mantiki ya kukimbiza hii misafara ya wakubwa ni nini? Misafara hii huenda kasi ya kutisha hata katika barabara za mjini. Inapotokea ajali madhara yake huwa ni makubwa kama ilivyotokea kwa msafara wa Bilal.

    ReplyDelete
  7. Jamani nisaidieni. Hivi misafara ikikimbizwa kama magari yako mashindanoni ndio viongozi wetu watukufu wanakuwa salama?

    ReplyDelete
  8. Vipi Polisi mna maoni gani hapo mnapomlipisha faini ya shilingi 30,000.00 mtu aliyetembea 55kph mahali palipo andikwa 50kph hali ya kuwa hakuna tatizo wala gari lolote mbele kisha mkasahau mbio mnazokimbia nyinyi wenyewe! Nadhani hii ni sawa tu na hasa ikimtokea bingwa wa kupiga faini watu barabarani kwa mwendo kasi!

    ReplyDelete
  9. akina Ras makunja poleni sana sana na maafa haya,unajua ajali haina kinga si mnaona wenyewe msaada mnaopewa kiasi raia wema wanavuta magitaa yenu kuwatoa bondeni,Poleni sana akina ras makunja

    ReplyDelete
  10. Poleni sana wafiwa,

    Kwanini msafara ya wakubwa, wanakimbia sana? Mwendo wa kasi unaua jamani, huwa naona misafara hii ikipita mpaka unaogopa kasi yake sio ya kawaida.

    Ila basi ajali ni ajali tu....bahati mbaya, poleni sana!

    ReplyDelete
  11. there is no one good reason of doing 120kph along bagamoyo road at anytime of the day / night. but this is what i have witnessing for almost all the 6 years that i have been working here. nobody thinks of any mishap that can kill in high speed but can be controlled in low speed.
    Ajali ina kinga.
    Kuwa mwangalifu.
    Usiwe mpumbavu.

    ReplyDelete
  12. poleni sana kwa wafiwa,ila ninachokiona hapo,kwanini hii misafara inakuwa na magari mengi na ina inakuwa kasi ya ajabu,atuna maadui,kwanini wasipunguze misafara ya magari mengi,pia magari yawe kwenye hali nzuri,na pia kitu kimoja najuiliza hivi magari ya polisi ni kwaajili ya misafara ya viongozi tuu?

    ReplyDelete
  13. I cant believe a police using a gun as an aid to be pulled out of a ditch!
    Someone help us........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...