Asalam Aleykum Ustadh Issa,

Pole na baridi linalokupiga huko Davos, Uswisi..

Hakuna tunachokunyima Dar zaidi ya joto tu..Nadhani joto hili la hapa kwetu ndo limesababisha mpaka gari hili kuungua...

Hii imetokea just now...hapa kwenye parking za jengo la Amani Place. Upande wa nyumba karibu na Citibank.

Zimamoto walifanikiwa kuisukuma na kuitoa eneo la parking ili isisababishe madhara kwa magari mingine..lakini almanusura wasababishe ajali nyingine baada ya kuiachia gari hiyo kwenda yenyewe hadi upande wa pili wa barabara na kumkosakosa jamaa aliyekuwa amepaki pikipiki akiangalia uokoaji wa gari hilo.

Chanzo cha gari hilo aina ya Toyota Surf kushika moto halijafahamika hadi sasa..na mwenye mali yake hajaonekana wala kujitambulisha.

Injini ya gari imeungua yote.

Mdau wa Globu ya Jamii alieshuhudia Tukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. bongo inshu kidogo watu wanajazana

    ReplyDelete
  2. Yaani watu wamesimama kibao kuangalia gari lakini akidondoka mtu hapo. haji mtu kuangalia kwa sababu ni gari lazima iwe issue mpaka mwenyewe ajulikane ni nani


    WORLD UP!

    ReplyDelete
  3. SIE WA-TANZANIA KITU KIDOGO MTU YUPO TAYARI ACHELEWE ANAPOKWENDA AU MKUTANONI AU KAZINI ATIZAME TU NINI KIMETOKEA, MAMBO KAMA HAYA WATU WA NJE WAKIJA WANATUONA WATANZANIA MATAJIRI KWELI SEHEMU UTAONA WATU WA-SIMU WANAFANYA YALE MATANGAZO YAO YA NJIANI K BASI WATU KIBAO WANAPAZUNGUKA WANAWACHA KAZI ZAO, KAMA HAPO NDIO MFANO ILA TUTAFIKA TU. TUWE MAKINI WENZETU NCHI ZA NJE WANAANZA KUFUKUZWA MAKAZI KUWA HAWANA MAKAZI SASA NGOJA WAJE HUKU WABEBE KAZI. MZ

    ReplyDelete
  4. dah yaani hata ningekuwa mimi ndio mwenye gari nisingejitokeza maana jinsi wanavyolitrit hilo gari ni noma je owner ingekuwaje?

    ReplyDelete
  5. Bongo ni uvivu na udaku tu ndio tatizo la watu. Watu wameridhika na umasikini hawataki kujiweka busy kujishughulisha wanasubiri dili na wizi, ujanja ujanja tu, la sivyo wasingekuwa na muda huo kupoteza kusimama mabarabarani.

    ReplyDelete
  6. vya wizi tu hivyooo

    ReplyDelete
  7. Kwendeni zenu mnajifanya nyinyi mpo busy na kazi wakati mnaonyesha kabisa hamana kazi hata aliyebandika habari hii ni moja wapo wa waliokuwepo hilo eneo akishangaa kama asingeweka hiyo habari mnaonekana mngekuwa wagonjwa kwani inaonekana ninyi ni mabingwa wa kuosha vinywa binafsi nilipita eneo hilo na kengele za hatari za jengo zima la Amani zilikuwa zikipiga kelele sasa mnadhani watu wangekuwa wanapita na kuona jambo lakawaida? hao unaodhani wanalitreat gari vibaya walikuwa wanajitahidi lisisababishe madhara kwani likikuwa juu parking ya jengo la Amanina gari lenyewe lilikuwa lina hitilafu ya umeme so halina brake system ilikuwa imekufa. waoshavinywa msiokuwa na deal kazi kuangalia wenzenu wanafanya nini moshe vinywa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...