Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) limemvua uanachama Mbunge wa Wawi na Mjumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, Mh Hamad Rashid Mohamed (pichani), kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama na hivyo kupoteza sifa za uanachama. 

Akitangaza uamuzi huo katika Hoteli ya Manson Mji Mkongwe jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema mbali na Hamad Rashid, pia baraza hilo limewavua uanachama wajumbe wengine watatu wa Baraza Kuu. 

Wajumbe hao ni Doyo Hassan Doyo kutoka katika Mkoa wa Tanga, Juma Sanani ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi na Shoka Khamis Juma, aliyewahi kuwa Mbunge wa Micheweni kwa tiketi ya CUF. 

“Baraza Kuu la CUF limewafukuza viongozi hao baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili kutoka wajumbe wa Tanzania Bara na theluthi mbili kutoka wajumbe Zanzibar,” alisema 
Mtatiro. 

Mjumbe mwingine: Yasin Mrotwa amepewa onyo kali na karipio huku na kwa mujibu wa Mtatiro, anaendelea kuchunguzwa na Baraza Kuu. 


Baada ya kuvuliwa uanachama, Hamad Rashid alizungumza na waandishi wa habari na kumuita Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, dikteta na kiongozi asiyeheshimu uamuzi wa Mahakama. 

“Sisi tumeweka pingamizi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa mkutano wa Baraza Kuu na hati ya Mahakama ipo wanayo...sasa nawashangaa wanakiuka sijui kwa nini?” Alihoji Hamad Rashid. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. HALAFU NDIO TUWAPE NCHI HAWA LABDA CCM IMELALA,TULIWAJUA ZAMANI HAO SI WALIKUWAMO HUMU TULIMO WAKASHINDWA WOTE NA HUYO SEIF WAO NDIO KABISA

    ReplyDelete
  2. Hakuna upinzani Tanzania. Wote walewale tu mamluki...

    ReplyDelete
  3. Sasa huyu mbunge wa CUF na yule wa NCCR ambao wanafukuzwa uanachama kikatiba ni lazima wavuliwe ubunge. Kwahiyo serikali inabidi iingie gharama za uchaguzi mdogo kwenye majimbo yayoachwa wazi kwa kutumia kodi za wananchi. Nafikiri hizo pesa za kampeni za helkopters zingesaidia waathirika wa mafuriko kuliko kugharamia chaguzi ndogo. Kwanini msiwafukuze mwaka wa uchaguzi 2015?

    ReplyDelete
  4. we mdau acha upuuzi. tatizo hili lisiwe kisingizio cha kusema eti ccm ndio bora, wote sawa. na mbaya zaidi ccm in kirusi cha umasikini kwani imekuwa madarakani miaka kibao hakuna kitu.
    upuuzi mtupu.
    tunahitaji revolution!!!ndio dawa pekee.

    ReplyDelete
  5. yaani upuuzi tu watu wazima badala ya kukaa na kuelekezana unafukuza nyie wenyewe wapinzani ndio nini?

    ReplyDelete
  6. yaani hata sielewi siasa za nchi hii.kwa mtindo wa timua timua huu nina mashaka na nia ya dhati ya ujenzi wa taifa letu.

    ReplyDelete
  7. way to go..hongeteni sana cuf, mtu mmoja anachafua hali ya hewa ya nchi nzima kisa uroho na tamaa tu ya madaraka!

    Bure kabisa!

    ReplyDelete
  8. KUDADADEKI....KAMA SEMINARY VILE.

    ReplyDelete
  9. Seif ,hataki upinzani kamili ndani ya Chama bali upinzani wa Ki maslahi, anajaribu kuinusuru 'NDOA' yake binafsi ya jinsia moja na Serikali!

    ReplyDelete
  10. Staihili yake Bwana HR
    Latuf

    ReplyDelete
  11. Safi sana CUF, kama NCCR na Chadema vile. Kama watu wanaokiuka katiba iliyowaweka madarakani basi lazima wawajibike kwayo kwa kupatilizwa! Lazima nidhamu katika chama iwepo, hakuna mtu aliye maarufu kuliko chama chake, mara nyingi anakuwa maarufu ndani ya chama. Sisiemu hadi leo wanashindwa kuvuana magamba, wanabaki kukashfiana katika magazeti na TV tu, hawana ubavu wa kufukuza hata mwenyekiti wa nyumba kumi kumi anayekula rushwa za kuku kijijini.

    ReplyDelete
  12. Tatizo la huyu bwana ana uchu sana wa madaraka! kumbukeni alipokuwa Mwenyekiti wa upinzani ubungeni na uliporudi kwa CHADEMA alihangaika sana kwa kutaka bado kuung'ang'ania!

    Amevuna alichopanda na nawasifu sana CUF kwa 'kumpiga chini' pambaf

    ReplyDelete
  13. wapinzani jasiri kutimuana,hawataki unafiki, ccm hasubutu kutimuana maana wamejaa woga na unafiki.walisema wanatimua mafisadi,wakaogopa,maana mafisadi ndo wamebeba chama.wapinzani hawaogopi kitu.bora wakutane mahakamani.

    ReplyDelete
  14. Hawa wanadai wanataka kuleta demokrasia ya kweli na nini halafu wao wenyewe hawako kidemokrasia. Mtu yupo uongozini hataki kukosolewa na wa chin yake je hapo kuna demokrasia kweli? Halafu ugomvi mkubwa wa Hamad ni dhidi ya Seif lakini cha ajabu Seif ndo mwenyekiti wa kikao kilomfukuza Hamad, sasa hapo kuna haki kweli? Hivi Lipumba ana kazi gani CUF?

    ReplyDelete
  15. Seif anakuwa kama Hirizi katika CUF akikukataa itabidi uondoke tu!

    ReplyDelete
  16. Walewale waliosifia madiwani wa Arusha kutimuliwa wanalalama wabunge mbunge wa CUF, NCCR kutimuliwa, Hongereni kwa vigegeu!

    ReplyDelete
  17. huyu na kafulila ndio waliotibua sheria ya kiongozi wa upinzani ndani ya bunge. Leo wanaonja dhambi zao.

    ReplyDelete
  18. Katiba ibadilishwe. Wabunge wamechaguliwa na wananchi then why wanapoteza ubunge wao wanapofukuzwa uanachama?

    ReplyDelete
  19. 1. Hamad rudi CCM
    2. Lipumba achana na siasa, kaongeze ujuzi USA, Uwe mshauri wa raisi 2015.
    3. Seif hatukupi nchi hata kwa hongo.

    ReplyDelete
  20. muschi b.c.January 05, 2012

    Huku ni kuoneana tu
    mbona viongozi wa serekali wanavunja katiba ya nchi wanabebwa CUF/NCCR katiba zenu ni za wapi kufukuzana ovyo chama lazima kiwe na wajanja na viraka bwana! Hamuoni za jamaa zetu wa Igunga! wimbo ni wa uchwara lakini tulicheza wote! Tuige wana kidumu bwana

    ReplyDelete
  21. CUF IPO JUU MIMI NI CCM LAKINI KWA KITENDO CHA KUFUKUZA NIMEPENDA SANA KWANI CHAMA AMRI MOJA TU UMEPEWA UBUNGE KUPITIA CHAMA HIVYO CHAMA HUNA UBUNGE HUNA SASA SISI CHAMA CHETU KIBOVU MTU HAWEZI VUA GAMBA ANA VULIWA TUU HATA KAMA ATATOA SIRI ZOTE ANAZO ZIJUA MWACHE ATOE TUSIMUOGOPE KWAMBA ATATOA SIRI ZA CHAMA AU DHAMBI ZA BWANA MKUBWA FUKUZA TUU POTELEA MBALI WACHA CHAMA KISAMBARATIKE NA MTU ASIPATE URAISI 2015 MFUKUZENI TU HUYO NDIO AMELETA MAFUNGU YA KUMLA KISOGO BOSI WAKE JAPO KUA AMEMUWEKA MADARAKANI SASA MWACHE ATOE SIRI MSIOGOPE NA URAISI HAPATI AKITOA SIRI ZA WENZIE FUKUZA FUATA CUF UAMUZI WAO SEIF BABUKUBWA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...