Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea seti ya vyombo vya nyumbani na taa inayotumia nguvu za jua toka kwa Mkurugenzi wa Home Shopping Centre Bw Gharib Saidi Mohamed ambaye kampuni yake imejitolea kugawa seti kama hizo pamoja na taa kwa kila familia 655 zilizohamishiwa Mabwepande baada ya kuathirika na Mafuriko katika bonge la Msimbazi. Bw Gharib pia ameahidi kujenga shule ya msingi ya eneo hilo pamoja na kituo cha polisi.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakioneshwa maeneo ya makazi mapya ya walioathirika na mafuriko katika bonde la Msimbazi walipotembelea eneo hilo leo.
Na Mwandishi Maalumu
Kampuni ya Home Shopping Centre (HSC) imeahidi kujenga kituo cha polisi, vyumba 14 vya madarasa ofisi za walimu na chumba cha kulia chakula kwa ajili ya waathirika wa mafuriko watakaohamia Mabwepande nje ya jiji la Dar es Salaam.
Mbali na ahadi hiyo HSC imetoa mifuko 2,000 ya saruji, vyombo vya ndani na taa za sola kwa familia zote 653 zitakazopatiwa makazi kwenye eneo hilo.
Hayo yalisemma leo na Mkurugenzi wa HSC Gharib Said Mohamed muda mfupi kabla Kamati ya maafa mkoani hapa kumkabidhi rais Jakaya Kikwete mahema 203 yaliyojengwa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS).
Bw Gharib amesema kwamba shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi na jengo la kulia chakula vitakamilika katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa.
“Kwa kweli mpaka sasa kwenye saruji, vyombo vya ndani na taa za sola tumetumia zaidi ya sh milioni 70 kuhusu ahadi ya ujenzi wa kituo cha polisi na shule mpaka sasa gharama yake hatujaijua hadi vitakapokamilika,” alisema Bw. Gharib.
Aliwaomba pia wadau wengine wenye nia ya kuwasaidia wananchi hao kujitokeza kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye maeneo mengine huku akisisitiza kwamba jukumu la kusaidua utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa wananchi linawahusu wote.
Awali rais Kikwete aliitaka kamati ya Maafa inayoshughulikia waathirika hao kufikiria namna ya kuwapatia viwanja waliokua wapangaji kwenye nyumba zote zilizobomelewa kwa mafuriko huku akiitaka kamati hiyo kuwa makini katika ugawaji wa viwanja hivyo.
“Msipokua makini zoezi hili haliishi… mtaendelea kufanya hivi kila siku watajitokeza pia wasiostahili watakuja kudai viwanja,” alisema rais Kikwete muda mfupi kabla ya kukabidhiwa na kukagua mahema hayo.
Aidha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) watafanya usafi wa maeneo na kujenga mahema kabla ya waathirika hao kuhamia Mabwepande.
Shukurani JK kwa kutuibulia Mstahiki Meya maana ishu yote hii hatukumuona na tangu achaguliwe sioni umuhimu wake, better scrap the post so we can use the funds for other issues.
ReplyDeleteMstahiki Meya, huu ulikuwa ni msiba wake kabisa!.
ReplyDeleteTena eneo la Jangwani kabisaaaaa nyumbani.
Jamani mmeona Uongozi wa vijana huo?
AMA KWELI UTU UZIMA DAWA!
Masikini Mzee wa watu amefitiniwa bureee, kipindi chake suala kama hili kwa vile anakaa Mtaa wa Tiwga na Sikukuu angewapa hata hifadhi kwake baadhi wa Waathirika!
Ninavyoamini Ankali Michuzi ni kwamba Mkuu wa nchi akisema kitu ni agizo na sio tena kubembelezana na agizo alilotoa ni kwamba nyumba zote ambazo zimeathirika na mafuriko zibomolewe na wenye nyumba wapatiwe viwanja.
ReplyDeleteLakini cha kustaajabisha ni kwamba kuna maeneo wamechagua nyumba chache tu kwa ajili ya kubomolewa na kupewa viwanja huku wakisema wamewapa wale tu walio kambini sasa wengine ambao hawakuwa kambini na ni waathirika waendelee kukaa tu mabondeni? halafu kesho na keshokutwa tutasema watu wa mabondeni ni wabishi kuhama, watu watahama vipi wakati viwanja walivyoahidiwa hawakupewa? na kumbuka hakuna mtu anayependa kukaa sehemu ya matatizo.Lakini Kutokana na uhuni kama huu ndio maana watu wanajichokea na kuamua kukaa mabondeni.