NAIBU WAZIRI WA MAJI, MHANDISI GERSON LWENGE AKIPOKEA MAELEZO YA UWINGI WA MAJI KATIKA CHOTEO LA MAJI LA RUVU CHINI KUTOKA KWA MTENDAJI MKUU WA DAWASCO MHANDISI JACKSON MIDALA.
NAIBU WAZIRI WA MAJI (WA TATU KULIA),MHANDISI GERSON LWENGE AKIPOKEA MAELEZO YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UPANUZI WA MTAMBO WA KUSAFISHA NA KUSAFIRISHA MAJI WA RUVU CHINI KUTOKA KWA MUWAKILISHI WA MFUKO WA FEDHA ZA CHANGAMOTO ZA MILINIA NCHINI TANZANIA (MCA-T), MHANDISI WILLIAM CHRISTIAN.
HII NI BAADHI YA MITAMBO INAYOTUMIWA NA KAMPUNI ZA DEGREMONT YA UFARASA NA SPENCON CONSOTIUM YA KENYA KATIKA UTEKELEZAJI WA UPANUZI WA MTAMBO WA KUSAFISHA NA KUSAFIRISHA MAJI WA RUVU CHINI.
HII NI MIONGONI MWA SEHEMU ALIZOZIKAGUA NAIBU WAZIRI WA MAJI MHANDISI GERSON LWENGE. SEHEMU HIYO INAHUSISHA UJENZI WA TENKI LA KUPOKELEA MAJIGHAFI KUTOKA KWENYE CHOTEO, CHUJIO LA KUONDOA TOPE KWENYE MAJI, SEHEMU YA KUSAFISHA MAJI NA KUTIA DAWA AINA YA KRORINI ILI KUUA BACTERIA PAMOJA NA PAMPU YA KUSUKUMA MAJI YALIYOSAFISHWA KUELEKEA JIJINI DAR ES SALAAM (PICHA NA PAINETO MAKWEBA, KITENGO CHA HABARI WIZARA YA MAJI).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimetafakari sana, ila nikajiuliza hakukuwa na kampuni ya kitanzania kwa ajii ya hii kazi??? wakenya wana uwezo zaidi yetu??? ama nikutopendana watanzania kwa watanzania???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...