Kwa viwalo vya kisasa kwa kinamama na kinababa pamoja na watoto kutoka USA, Spain na Italy tembelea J&M Virgo Boutique iliyopo katika jengo jipya ya C&G Mikocheni kwa Warioba jijini Dar es salaam ambako utawakuta James Shan'ga na Da'Mishi Marshall wakikukuhudumia kwa weledi.
Watembelee katika libeneke lao: 
 Hapa ushindwe wewe tu....
 Mashati ya uhakika na suti za kileo
 Viatu toka Italy
Da'Mishi Marshall akiwa ofisini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hawa jamaa wanauza vitu ghali sana wakati ni vitu vya kawaida kabisa ambavyo unaweza kuvipata sehemu zingine nyingi kwa bei nafuu sana tu.I don't recommend shopping here at all!

    ReplyDelete
  2. Kwani si uende tu kwenye bei nafuu? Tunaojua na kutakata viwango na utofauti tukiwa nazo tutaenda virago tu.

    ReplyDelete
  3. mdau nakubaliana nawe. lakini kila duka linauza kulingana na mahali lilipo, kodi wanayolipa ya pango, tra wakiiingiza mzigo na ubora wa vitu/bidhaa.
    unaweza kununua shati congo st bei nafuu lakini huna uhakika kama ni genuine au limefyatuliwa china. kitu ghali ujue kina uhakiki na ubora wake. kwa hiyo ukiuziwa ghali, juwa kimegharamiwa na ni bora.

    ReplyDelete
  4. WEWE MDAU MFUNGUA KINYWA WA KWANZA, ACHA NONGWA YAKO KAMA HUNA HELA YA KUNUNUA NENDA KANUNUE MTUMBANI HUO NI USWAHILI KUJALAZIMISHWA KWENDA NUNUA PALE.HILO NI TANGAZO LA BIASHARA KAMA UNATAKA KANUNUE HUTAKI SINUNUE FALA MKUBWA WEE! CHIPS KINONDONI KWA MANYANYA NI SHS 2000, UKINUNUA CHIPS HIO HIO WHITE SAND NI SHS 10,000/= WAAMBIE NA HAO WALA CHIPS WASINUNUE HOTELINI HAPO WHITE SAND, KWANI NI BEI KUBWA . MSHAMBA HUJAENDA SHULE ,KANAWE KWANZA USO, UTOE TONGO TONGO NDIO UENDE INTERNET CAFE UKALIPE SHS 250 ROBO SAA.

    KUMBUKA HILO DUKA HALIKO VINGUNGUTI ! LIKO MIKOCHENI KWA WATU WANAOWEZA NUNUA KWA THAMANI INAYOSTAHILI. WEWE UNA FIKIRI HILO DUKA KAPANGISHA BURE?UTAMLIPIA WEWE RENT?, SWAINI MSWAHILI WA HEDI.

    MDAU LONDON

    ReplyDelete
  5. VERY NICE. JAMANI MISHY UMEENDELEA HIVYO DADA ANGU. HONGERA SHOGA MJASIRIMALI WA NGUVU DUKA NDANI SHOPPING PLAZA SI MCHEZO. VIWALO PIA SI MCHEZO. NIKIPATA KITABU CHANGU NTAKUJA KUTEMBELEA DUKA LAKO.

    MDAU USA.

    ReplyDelete
  6. Mdau Fri Jan 20, 03:46:00 PM 2012 nina wasiwasi una uhusiano na duka hilo.

    ReplyDelete
  7. Hii ni BLOG.Sawa, ila mimi nitarudia kusema Matangazo ya biashara tuyaheshimu jamani..Mtu anapoweka biashara yake si vizuri kutoa maoni ambayo ni hasi hata kama yana ukweli ndani yake.Waweza kusoma tu na 'kukata kona'.Fikiria wewe unayesoma comment hii umeweka biashara yako sehemu fulani halafu kuna mtu pembeni anapiga kelele..hee msinunue hiyo...hiyo mbovu hiyoooo...anawadanganya huyo......!

    David V

    ReplyDelete
  8. VIRGO MBONA MNAKUJA KASI HIVYO. JAMANI DUKA KUBWA, VIWALO VYA NGUVU DUKA JAMANI KAMA LIPO NDANI YA SHOPPING MALL MAJUU. LIMEPENDEZA KWELI HOPE NAMI NINGEKUWA NA NJULUKU NIKAFUNGUA MDUKA MKUBWA KAMA HUO. DUKA LA LAAAAANA.

    ReplyDelete
  9. kwa maelezo na picha zaidi bofya hapa :- j&m virgo blogspot.com

    ReplyDelete
  10. Huyo mdau wa kwanza anachuki binafsi au ni mtu ambaye hajatembea

    ReplyDelete
  11. michuzi mtoa mada last but one hapo juu amechafua hali ya hewa! amututukana sisi wa vingunguti, na usifikiri anaekaa vingunguti kapenda, nae anajitahidi na maisha na utakuta walio nazo ni vigumu sana hata kutoa hela zao japo kuchangia wasio nacho hata kama ni kuhusiana na suala la elimu. sisemi ni hao wenye duka but kumbuka nchi hii kuna ukiukaji haki wa kila aina ili wachache wajirajirishe. usiseme for the sake of kusema, usiandike for the sake of kuandika. TAFAKARI!

    ReplyDelete
  12. Freedom of speech lets them talk what ever they want.

    ReplyDelete
  13. jamani hizi picha ni nyanya tu. ingia j&m virgo blogspot utazimia. kuna vitu vya nguvu kama ukifa utataka uzikwe navyo. nime google j&m virgo ikafunguka link yako. kubonyeza hivyo vitu vyilivyomo humo ndani, anajua mwenyewe mwenye duka. nimefurahisha macho tu hata kama sina hela lakini siku moja ntajipinda. life is too short!

    ReplyDelete
  14. Vitu J$M Virgo ni vikali,,,usipime!

    Mwenye hela zake na anaetaka viwango atanunua!

    Anaetaka kwa bei ya chini aende sagula sagula Mchikichini, Congo Kariakoo au Manzese akaokote za kurundikwa chini!

    ReplyDelete
  15. uza mlivyozalisha = maendeleo kwenu, nyie wa-TZ!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...