NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

MWENYEKITI mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) Jaji Mstaafu, Damian Lubuva amesema kwamba atafanya kazi kwa kuzingatia Katiba ya nchi na Sheria .

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti huyo wa NEC mara baada kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete leo katika halfa fupi iliyofayika Ikulu jijini Dares Salaam.

“Nitaendeleza shughuli za tume pale walipoachia wenzangu . Nitafanya kazi kama wenzangu kwa kuangalia Katiba na Sheria bila kupendelea wadau wowote,” alisema Jaji Lubuva.

Aliongeza kuwa kazi atakayoanza nayo kwa sasa ni kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia uchaguguzi uliopita hadi uchaguzi ujao wa mawaka 2015.

“ Tunaomba wannachi watuamini ,tuppeni muda ili tufanye shughuli za tume tuzimlize kablya ya uchaguzi wa mwaka 2015,” alisisitiza huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa uboreshaji huo utakaofanyika kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Aidha, Rais Kikwete aliwaapisha viongozi wengine wapya wa tume hiyo , ambao ni Makamu Mwenyekiti Jaji mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid na Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba.

Uteuzi wa viongozi hao ulianza Desemba 19, mwaka jana .

Kabla ya uteuzi wake, Lubuva alikuwa Jaji katika Mahakama ya Rufani Tanzania na baada ya kustaafu aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi. Lubuva anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Lewis Makame ambaye mkataba wake wa utumishi wa umma ulifikia mwisho Julai, mwaka huu, 2011.

Wakati Hamid alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kustaafu kwake na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Jaji Omari Makungu. Jaji Makungu aliteuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na baadaye akateuliwa kuwa Jaji Mkuu.

Naye Mallaba, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Mkurugenzi wa Sehemu ya Mikataba (Contracts and Treaties) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mallaba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Rajabu Kiravu ambaye amemaliza mkataba wake wa utumishi Septemba, mwaka huu, 2011.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwani hao waliotangulia walikuwa wanafuata nini?

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu nakuunga mkono, Jaji Lubuva tueleze una maana gani, walikuwa wakifuata mwongozo wa CCM?

    ReplyDelete
  3. ndo misemo yao hao!

    ReplyDelete
  4. Hakuna jipya hapo yale yaleee na mnategemea tume huru hapo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...