Gari la mbele la njano ni maalumu kwa kusomba theluji ambayo inadondoka masaa 24 katika mji wa Davos, Uswisi na wasipofanya hivyo barabara inakuwa haipitiki
 Davos ni mji mdogo wa milimani Alps kaskazini magharibi mwa Uswisi wenye wakaazi 13,000 ukiwa mita 1560 juu ya usawa wa bahari katika  (canton) mkoa wa Graubunden, kiasi cha masaa mawili hivi kwa gari toka jijini Zurich. Ulianza kama kiota cha vekesheni za kiafya na michezo ya thelujini, ila sasa Davos ni maarufu duniani kwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Uchumi  (BOFYA HAPA The Annual Meeting of the world Economy Forum), na mwaka huu kongamano hilo limeanza leo hadi January 29, 2012.

Wastani wa hali ya hewa kwa mwaka ni 2.8C (37.04F) na wakati wa kongamano la mwaka huu kiwinta kitakuwa -4C (24.8F) na 1C (33.8F) hivyo kwa akina sie tunaotoka pwani ya Afrika Mashariki ni balaa tupu.

Kwa majira Uswisi iko mbele kwa saa moja dhidi ya GMT/UTC, na Bongo ni GMT+3 hivyo iko saa moja mbele ya Uswisi.

Fedha yao hadi sasa ni faranga (Swiss Francs) ama CHF ama Sfr, ambapo Euro moja ni sawa na CHF 1.23715 ama Dola moja ya Kimarekani ni sawa na CHF 0.92400. 

Lugha wanayotumia Uswisi zaidi zaidi ni Kijerumani ambacho ndio lugha rasmi hapa Davos, ingawa kimombo, Kifaransa na Kitaliano huzungumzwa sana.
 Theluji kila mahali na kila wakati
 Sheli
 Babu anaenda shopping huku theluji ikimnyeshea
ankal anawasili Davos akivunga kufa kwamba kiwinta hakimsumbui. 
Hapo anatetemeka kama nini sijui...Ze Fulanazzzz kama kawa hahahaa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Ankal karibu kwa wajanja! mambo ya joto la bongo waachie wenye kuliweza..ila hala hala usijepata pneumonia manake kwa pamba ulizopiga,kifua hakikawii kuitikia...kula bata kama huna akili nzuri ankal.

    ReplyDelete
  2. Mkuu karibu sana Ubaridini, a.k.a kwenye Friji.

    ReplyDelete
  3. Ankal, hala hala na nyumonia, pumu na ngiri maji.
    Ninavyokufahamu wewe afya yako ni ya mgogoro hata kule nyumbani, leo iweje kijifulanazzz ukiamini hivyo?

    Massoud Kimim, Cleveland, OHIO

    ReplyDelete
  4. Ankal, tumekuwekea "surveilance Camera" huko uliko, ukichukua blanketi chapa ya mtu tutakusemea kwa mama yake Mamuu.

    Abiola Jr., Mafia kiduka cha juice.

    ReplyDelete
  5. @ Anony 01:57: Nadhani Ankal kavaa fulana aina ya thermal..

    ReplyDelete
  6. Nini Pneumonia Ngiri je? we mwache tu

    ReplyDelete
  7. ankal fulana hii kila ukienda abroad unayo..mh tupe siri yake. Goodluck huko

    ReplyDelete
  8. shauri yako utatoka na gonjwa la ajabu. itakuwa flu si flu, malaria si malaria. baridi haizoeleki ankali vaa masweta mazito na turtlnecks utadedi siku si zako ohooo!!!

    ReplyDelete
  9. Ankal winta mbona mnaisikia tuu, karibu kwenye winta ya kweli canada uone mambo kama hiyo tisheti utaijua, karibu toronto.

    ReplyDelete
  10. bata gani mateso tu labda wazawa ndio wanainjoi kutwa nzima unajifungia ndani ya kuta usidanganye kwa wasiofika huko anonymous Wed Jan 25, 01:57:00 AM 2012

    ReplyDelete
  11. I like the trademark 'Ze Fulanazzz'

    ReplyDelete
  12. Michuzi angalia usipate Hypothemia kaka. Hiyo sio baridi ya mbalizi,makambako.Btw mkuu wa nji hii yupo swisw nini? Enjoy your trip.

    ReplyDelete
  13. Ankal hizo fulanazzz zako, kwa Jokofu la huko U-SWISS angalau ungevaa lile lishati lako la Magwandazzz la mifuko ya kifuani double pocket ulilopiga wiki iliyopita tukakuuliza labda umebadili ITIKADI!

    ReplyDelete
  14. Haya haya Kakaaaaaa! Bakiza faranga hizoooo teheeeeee

    ReplyDelete
  15. oya Michu usifanye mchezo na kiwinta ukarudi na nimonia, piga koti la maana, viatu vya wintana scarf achana na hicho kijasti chako.

    ReplyDelete
  16. Kaka, Salamu zao huko ughaibuni, hala hala usije bakia huko bwana njoo mapema taifa linahitaji wanahabari hili.

    Nelson, mzee wa vyoo.

    ReplyDelete
  17. Hiyo fulanaz ankal iko moja? si ishafubaa! sema tukuchangie! lol!

    ReplyDelete
  18. hahahahah jamn the fulan uliachiwa na babu nin????maana ankal na hiyo fulana eheheheh

    ReplyDelete
  19. Asante sana Bro Michuzi kwa picha na taarifa nyingine za kuelimisha.

    David V

    ReplyDelete
  20. ankali mbona huko ni joto kabisa ukilinganisha na huku russia nilipo. Leo temp ni -21C.Tuna bahati tupo likizo

    ReplyDelete
  21. Ankal, tafadhali tumia kiswahili sanifu. Hiyo syo Sheli - ni Sheli ya Shell.
    Kw2a taarifa tu kwa wale wa ughaibuni. Sheli za BP haziko tena TZ, sasa zitaitwa Sheli za Puma Oil

    ReplyDelete
  22. Jamal ankal alishapiga kikombe cha babu ivo winter haimpi tabu

    ReplyDelete
  23. mbona hapo snow ni ndigo,njoo maeneo fulan fulan utakoma ubishi,muchizi vaa koti kubwa utaumwa!!

    ReplyDelete
  24. snow ikiwa inaanguka wala kunakuwa hamna baridi kivile subiri jua liwake kidogo ndo utajua nini maana ya kiwinter! ankali naapa ukivaa namna hii toronto lazima utalia maana baridi inakata kama kiwembe.

    ReplyDelete
  25. Hivi Q7 kwenye background inaonekana ni modeli mpya. Hivi huko inaweza kuwa inauzwa kama paundi ngapi?

    ReplyDelete
  26. Ankal Nimegundua kumbe wewe unatembea na Rais kumpiga picha. mana naona JK yuko Davos Uswiss na ww uko huko huko. Haya hongera sana tuletee basi habari zaid na usisahau kupitia UK kidogo kutusalimia

    ReplyDelete
  27. UNCLE LAKINI ANGALIA HAKO KA WINTER, NI HATARI KAMA HUVAI VIZURI. NA HUYO WAZRI J4 MAGHEMBE MWAMBIE AFANYE MAZOEZI APUNGUZE TUMBO KUBWA SANA MPAKA NOMA. HUKU ULAYA HAKUNA WAZIRI ALIEKUWA NA UMBO KAMA HILO .HASA ISITOSHE YEYE NI WAZIRI WA ELIOMU JE WASOMI NDIO WAIGE MWILI KAMA HUO AU NI UFISADI TU ? WAZUNGU WANAMUONA KAMA KASHIBA DOLA ZA WIZI, NOMA HIO JAMANI WABONGO WENZANGU TUAMBIANE, HUYO SI ATAKUFA NA PRESHA TU KESHO KESHO KUTWA?

    MDAU LINDUKA,ZURICH

    ReplyDelete
  28. wewe anony wa Wed Jan 25, 06:59:00 AM 2012 acha wivu na kijiba cha roho.wewe kama huna karatasi la kukaa ulaya kaa kimya. au ulienda ulaya kwa hela za kijiji ndo ukashindwa kula bata?? kwa taarifa yako baridi ipo na watu wanaenda clubs kula raha vile vile. kama huna cha kuchangia kaa kimya sio kujidai unajua kujibu comments za watu..
    Ankal kula bata uswiss manake maisha mafupi..

    ReplyDelete
  29. Ankali baridi haina masifa tuulize sisi wenyeji wa ughaibuni tafuta koti la maana la kujizuia na baridi utarudi nyumbani na magonjwa ya mifupa......hapo utajiona unapita mara moja unaingia ndani lakini hiyo mara moja itakufanya ukitoka tena nje ya nyumba utajisikia baridi ya hatari sana ndani ya mifupa.

    ReplyDelete
  30. haha wadanganye wasio ijua europe matesooo kutwa ndani jamaa yupo sahihi
    hahahaaaaaaaaaaa
    hakufanai na hmo home ukiwa nazoo fulll shangweeeeeee
    mimi nipo DERNMARK kaka lakini shwariiii

    ReplyDelete
  31. Nipatanga dili kuiba hiyo fulana itakapoanikwa nyumbani kwako. Nina hakika Ankal utakuwa tayari kutoa mamilioni ili urudishiwe. Hiyo fulana si bure. Nadhani unaichukulia hiyo kama 'talisman' yako, yaani kitu chenye kukuletea mafanikio. Wasalimie wote walio katika hilo friji.

    ReplyDelete
  32. Winter hiyo! Halahala na spin-outs kwenye barafu (black ice) iliyochini ya hiyo theluji!

    ReplyDelete
  33. ankali tunajua KAZI yako....wewe kumbe ni s....... tu

    ReplyDelete
  34. kaka mimi hilo audi tu ukilisafisha lilete hapa bongo ha haa

    ReplyDelete
  35. Ankal umeonaeeee wadau wako tunakupendaga sana hatutaki uugue au ufe na winter la huko.

    ReplyDelete
  36. Ankal niletee zawadi ya chocolate toka Uswizi basi ee si unakuja nayo ee.

    ReplyDelete
  37. Zee fulanaz na kiwinterz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...