![]() |
Gari la mbele la njano ni maalumu kwa kusomba theluji ambayo inadondoka masaa 24 katika mji wa Davos, Uswisi na wasipofanya hivyo barabara inakuwa haipitiki |
Davos ni mji mdogo wa milimani Alps kaskazini magharibi mwa Uswisi wenye wakaazi 13,000 ukiwa mita 1560 juu ya usawa wa bahari katika (canton) mkoa wa Graubunden, kiasi cha masaa mawili hivi kwa gari toka jijini Zurich. Ulianza kama kiota cha vekesheni za kiafya na michezo ya thelujini, ila sasa Davos ni maarufu duniani kwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Uchumi (BOFYA HAPA The Annual Meeting of the world Economy Forum), na mwaka huu kongamano hilo limeanza leo hadi January 29, 2012.
Wastani wa hali ya hewa kwa mwaka ni 2.8C (37.04F) na wakati wa kongamano la mwaka huu kiwinta kitakuwa -4C (24.8F) na 1C (33.8F) hivyo kwa akina sie tunaotoka pwani ya Afrika Mashariki ni balaa tupu.
Kwa majira Uswisi iko mbele kwa saa moja dhidi ya GMT/UTC, na Bongo ni GMT+3 hivyo iko saa moja mbele ya Uswisi.
Fedha yao hadi sasa ni faranga (Swiss Francs) ama CHF ama Sfr, ambapo Euro moja ni sawa na CHF 1.23715 ama Dola moja ya Kimarekani ni sawa na CHF 0.92400.
Lugha wanayotumia Uswisi zaidi zaidi ni Kijerumani ambacho ndio lugha rasmi hapa Davos, ingawa kimombo, Kifaransa na Kitaliano huzungumzwa sana.
Theluji kila mahali na kila wakati
Sheli
Babu anaenda shopping huku theluji ikimnyeshea
ankal anawasili Davos akivunga kufa kwamba kiwinta hakimsumbui.
Hapo anatetemeka kama nini sijui...Ze Fulanazzzz kama kawa hahahaa!
Ankal karibu kwa wajanja! mambo ya joto la bongo waachie wenye kuliweza..ila hala hala usijepata pneumonia manake kwa pamba ulizopiga,kifua hakikawii kuitikia...kula bata kama huna akili nzuri ankal.
ReplyDeleteMkuu karibu sana Ubaridini, a.k.a kwenye Friji.
ReplyDeleteAnkal, hala hala na nyumonia, pumu na ngiri maji.
ReplyDeleteNinavyokufahamu wewe afya yako ni ya mgogoro hata kule nyumbani, leo iweje kijifulanazzz ukiamini hivyo?
Massoud Kimim, Cleveland, OHIO
Ankal, tumekuwekea "surveilance Camera" huko uliko, ukichukua blanketi chapa ya mtu tutakusemea kwa mama yake Mamuu.
ReplyDeleteAbiola Jr., Mafia kiduka cha juice.
@ Anony 01:57: Nadhani Ankal kavaa fulana aina ya thermal..
ReplyDeleteNini Pneumonia Ngiri je? we mwache tu
ReplyDeleteankal fulana hii kila ukienda abroad unayo..mh tupe siri yake. Goodluck huko
ReplyDeleteshauri yako utatoka na gonjwa la ajabu. itakuwa flu si flu, malaria si malaria. baridi haizoeleki ankali vaa masweta mazito na turtlnecks utadedi siku si zako ohooo!!!
ReplyDeleteAnkal winta mbona mnaisikia tuu, karibu kwenye winta ya kweli canada uone mambo kama hiyo tisheti utaijua, karibu toronto.
ReplyDeletebata gani mateso tu labda wazawa ndio wanainjoi kutwa nzima unajifungia ndani ya kuta usidanganye kwa wasiofika huko anonymous Wed Jan 25, 01:57:00 AM 2012
ReplyDeleteI like the trademark 'Ze Fulanazzz'
ReplyDeleteMichuzi angalia usipate Hypothemia kaka. Hiyo sio baridi ya mbalizi,makambako.Btw mkuu wa nji hii yupo swisw nini? Enjoy your trip.
ReplyDeleteAnkal hizo fulanazzz zako, kwa Jokofu la huko U-SWISS angalau ungevaa lile lishati lako la Magwandazzz la mifuko ya kifuani double pocket ulilopiga wiki iliyopita tukakuuliza labda umebadili ITIKADI!
ReplyDeleteHaya haya Kakaaaaaa! Bakiza faranga hizoooo teheeeeee
ReplyDeleteoya Michu usifanye mchezo na kiwinta ukarudi na nimonia, piga koti la maana, viatu vya wintana scarf achana na hicho kijasti chako.
ReplyDeleteKaka, Salamu zao huko ughaibuni, hala hala usije bakia huko bwana njoo mapema taifa linahitaji wanahabari hili.
ReplyDeleteNelson, mzee wa vyoo.
Hiyo fulanaz ankal iko moja? si ishafubaa! sema tukuchangie! lol!
ReplyDeletehahahahah jamn the fulan uliachiwa na babu nin????maana ankal na hiyo fulana eheheheh
ReplyDeleteAsante sana Bro Michuzi kwa picha na taarifa nyingine za kuelimisha.
ReplyDeleteDavid V
ankali mbona huko ni joto kabisa ukilinganisha na huku russia nilipo. Leo temp ni -21C.Tuna bahati tupo likizo
ReplyDeleteAnkal, tafadhali tumia kiswahili sanifu. Hiyo syo Sheli - ni Sheli ya Shell.
ReplyDeleteKw2a taarifa tu kwa wale wa ughaibuni. Sheli za BP haziko tena TZ, sasa zitaitwa Sheli za Puma Oil
Jamal ankal alishapiga kikombe cha babu ivo winter haimpi tabu
ReplyDeletembona hapo snow ni ndigo,njoo maeneo fulan fulan utakoma ubishi,muchizi vaa koti kubwa utaumwa!!
ReplyDeletesnow ikiwa inaanguka wala kunakuwa hamna baridi kivile subiri jua liwake kidogo ndo utajua nini maana ya kiwinter! ankali naapa ukivaa namna hii toronto lazima utalia maana baridi inakata kama kiwembe.
ReplyDeleteHivi Q7 kwenye background inaonekana ni modeli mpya. Hivi huko inaweza kuwa inauzwa kama paundi ngapi?
ReplyDeleteAnkal Nimegundua kumbe wewe unatembea na Rais kumpiga picha. mana naona JK yuko Davos Uswiss na ww uko huko huko. Haya hongera sana tuletee basi habari zaid na usisahau kupitia UK kidogo kutusalimia
ReplyDeleteUNCLE LAKINI ANGALIA HAKO KA WINTER, NI HATARI KAMA HUVAI VIZURI. NA HUYO WAZRI J4 MAGHEMBE MWAMBIE AFANYE MAZOEZI APUNGUZE TUMBO KUBWA SANA MPAKA NOMA. HUKU ULAYA HAKUNA WAZIRI ALIEKUWA NA UMBO KAMA HILO .HASA ISITOSHE YEYE NI WAZIRI WA ELIOMU JE WASOMI NDIO WAIGE MWILI KAMA HUO AU NI UFISADI TU ? WAZUNGU WANAMUONA KAMA KASHIBA DOLA ZA WIZI, NOMA HIO JAMANI WABONGO WENZANGU TUAMBIANE, HUYO SI ATAKUFA NA PRESHA TU KESHO KESHO KUTWA?
ReplyDeleteMDAU LINDUKA,ZURICH
wewe anony wa Wed Jan 25, 06:59:00 AM 2012 acha wivu na kijiba cha roho.wewe kama huna karatasi la kukaa ulaya kaa kimya. au ulienda ulaya kwa hela za kijiji ndo ukashindwa kula bata?? kwa taarifa yako baridi ipo na watu wanaenda clubs kula raha vile vile. kama huna cha kuchangia kaa kimya sio kujidai unajua kujibu comments za watu..
ReplyDeleteAnkal kula bata uswiss manake maisha mafupi..
Ankali baridi haina masifa tuulize sisi wenyeji wa ughaibuni tafuta koti la maana la kujizuia na baridi utarudi nyumbani na magonjwa ya mifupa......hapo utajiona unapita mara moja unaingia ndani lakini hiyo mara moja itakufanya ukitoka tena nje ya nyumba utajisikia baridi ya hatari sana ndani ya mifupa.
ReplyDeletehaha wadanganye wasio ijua europe matesooo kutwa ndani jamaa yupo sahihi
ReplyDeletehahahaaaaaaaaaaa
hakufanai na hmo home ukiwa nazoo fulll shangweeeeeee
mimi nipo DERNMARK kaka lakini shwariiii
Nipatanga dili kuiba hiyo fulana itakapoanikwa nyumbani kwako. Nina hakika Ankal utakuwa tayari kutoa mamilioni ili urudishiwe. Hiyo fulana si bure. Nadhani unaichukulia hiyo kama 'talisman' yako, yaani kitu chenye kukuletea mafanikio. Wasalimie wote walio katika hilo friji.
ReplyDeleteWinter hiyo! Halahala na spin-outs kwenye barafu (black ice) iliyochini ya hiyo theluji!
ReplyDeleteankali tunajua KAZI yako....wewe kumbe ni s....... tu
ReplyDeletekaka mimi hilo audi tu ukilisafisha lilete hapa bongo ha haa
ReplyDeleteAnkal umeonaeeee wadau wako tunakupendaga sana hatutaki uugue au ufe na winter la huko.
ReplyDeleteAnkal niletee zawadi ya chocolate toka Uswizi basi ee si unakuja nayo ee.
ReplyDeleteZee fulanaz na kiwinterz
ReplyDelete