Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. hahahaha, nimeipenda hyo na ntakuwa wa kwanza kununua hyo tshirt

    ReplyDelete
  2. haaahaaa duh... ama kweli insikitisha. I luv my country

    ReplyDelete
  3. Nimtanzanialakini....January 04, 2012

    Kwa kweli kauli za Magufuli ni sawa kabisa, nauli iliokuwepo ni kidogo mno.
    Kudos magufuli.
    Kuna dada mmoja katoa maoni kupitia kwenye blog ya othman Michuzi.
    http://othmanmichuzi.blogspot.com/2012/01/mnalenu-jambosio-bei-mpya-ya-kivuko.html
    Kwamba wabongo tumezoea kuambiwa UONGO, sababu tunapenda kuambiwa uongo.
    Kwa hili naku support Magufuli.

    ReplyDelete
  4. Kipanya, amesahau ile ya Waziri mkuu Msuya enzi zake " kila mtu atauchukua mzigo wake na watoto wake"

    ReplyDelete
  5. Kweli imedhihirika kuwa Sirikali yetu ni wafanya biashara kwa karibu kila kitu!

    KARIBU KILA KITU PESA:
    1.Pasipoti kwa gharama zetu!
    2.Vyeti vya kuzaliwa ,doa na kifo kwa gharama zetu!
    3.Nyingi za huduma za Kiaraia ambazo hata nchi masikini wenzetu zina gharimiwa na Serikali zao chovu hapa kwetu hakunaga bure, kila kitu pesa mbele!

    SIO AJABU:
    4.Utaweza kuja kusikia KUPIGA KURA kwa gharama zenu pia!
    5.Kutaka kumuona Kiongozi kwa PESA!

    Hii bei ni KUBWA MNO kwa vile wacha huko nchi zilizoendelea humu humu nchi jirani kama Likoni Mombasa-Kenya na Nkata Bay-Malawi pana vivuko kwa wale bandugu (TZ 11),,,watumiao usafiri wa miguu yao miwili, yaani waenda kwa miguu ni BUREEE!

    ReplyDelete
  6. Kweli imedhihirika kuwa Sirikali yetu ni wafanya biashara kwa karibu kila kitu!

    KARIBU KILA KITU PESA:
    1.Pasipoti kwa gharama zetu!
    2.Vyeti vya kuzaliwa ,doa na kifo kwa gharama zetu!
    3.Nyingi za huduma za Kiaraia ambazo hata nchi masikini wenzetu zina gharimiwa na Serikali zao chovu hapa kwetu hakunaga bure, kila kitu pesa mbele!

    SIO AJABU:
    4.Utaweza kuja kusikia KUPIGA KURA kwa gharama zenu pia!
    5.Kutaka kumuona Kiongozi kwa PESA!

    Hii bei ni KUBWA MNO kwa vile wacha huko nchi zilizoendelea humu humu nchi jirani kama Likoni Mombasa-Kenya na Nkata Bay-Malawi pana vivuko kwa wale bandugu (TZ 11),,,watumiao usafiri wa miguu yao miwili, yaani waenda kwa miguu ni BUREEE!

    ReplyDelete
  7. SAWA AMRI HIYO (PIGENI MBIZI) SIYO HUKUMU YA KIFO, BAADA YA ADA YA KIVUKO KUPANDA!

    Angalau mngetoa mafunzo ya BURE ya kuogelea kwanza!

    ReplyDelete
  8. Big up KP! Tunataka watu kama wewe ambao mna-dare kusema ukweli kweupeee! Endelea kuwaelimisha wadau bwana, fungu lako liko Mbinguni, usijali. Tunakuombea na tupo pamoja sana tu, zifyatue hizo fulanaz muda muafaka ukifika!

    ReplyDelete
  9. Mi nimefurahi magufuli alivyosema.hao wabunge kwanini wasitututee umeme ukipanda ka sio chuki binafsi.Big Up Magufuli

    ReplyDelete
  10. Nauli kupandishwa haina tatizo hilo ni jambo la kawaida, tatizo hawakuwahusisha wadau na pili maneno ya kupiga mbizi au mrudi kijijini ni ya kihuni. Magufuli amekosea kwa kutoa maneno ya mtaani wakati yeye ni kiongozi hapo ndo tunapopingana, ila kwa kuongeza nauli tuko pamoja kama utaratibu unafuatwa

    ReplyDelete
  11. Mimi nataka pantoni ziwepo na siyo zife kwasababu nauli kidogo..Huko bara vivuko bei mbaya kwanini dar es salaam shs 200 kubwa???

    ReplyDelete
  12. Nimesikitishwa na hayo majibu ya waziri magufuli,kupandisha nauli ni sawa lakini tuwe na namna nzuri ya kuelimesha watu.inawezekana wasikuelewe lakini lugha nzuri ni muhimu.uongozi ni utumishi au sio?

    ReplyDelete
  13. Kipanya itoe hiyo Tshirt kesho asubuhi manake wale wanaojua kukopy na kupaste saa hizi wanatengeneza zao ukishangaashangaa utakuta wenzio kesho jioni wameanza kuuza.

    ReplyDelete
  14. KP ni wazo zuri ila ongeza space kwani mpaka 2015 vitakuja vingi kama vitalu vya uwindaji na midura ya migodini ni kwa wakubwa tu etc, etc

    ReplyDelete
  15. Kuna Watanzania huwa tunawaona kwenye mitandao ya kijamii wanataka ubepari. Kulipia kila kitu ndio ubepari wenyewe huo. Yaani lazima umlipe bepari,na serikali inaruhusu hivyo kwa sababu bepari lazima arutubishwe ili awaajiri makabwela. (kiukweli bepari anaajiri makabwela wachache na anabania mishahara) Lakini kinadharia ndio mpango unavyjulikana.

    ReplyDelete
  16. kipanya fanya haraka ukaweke hati miliki maana hiyo inauzika tena kesho na siyo 2015.wasije wezi wakafyatua T shirt kesho.Mimi ikitoka mteja namba moja.hayo maneno ya wakuu wa nchi yatawageuka 2015 Mungu anawaonyesha watanzania nini cha kufanya.

    ReplyDelete
  17. Kama hujui kupiga mbizi hamia Dodoma. Hakuna cha bure dunia hii.

    ReplyDelete
  18. Tatizo linabaki kwa sisi wenye namba za Usajili wa Magari yetu (TZ 11) yaani tunaotembea kwa miguu!

    Gharama hii Shs. 200/= ni kubwa mno, hata hiyo Shs. 100/= ilikuwa ni nyingi sana ukizingatia sisi wengi ni akina ABA CHOLILE!

    ReplyDelete
  19. Mie namuunga mkono Magufuli kwa 100%! nauli shs 100 tangu 1995 hadi leo? ebo! gharama za uendeshaji mwazijua? acheni uswahili jamani twende na wakati! namsifu kwa ukweli! Pigeni mbizi ndio acheni utoto

    ReplyDelete
  20. Magufuli yuko sawa, kwanza hiyo nauli yenyewe bado ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za uendeshaji. Tatizo ni kuwa tumezoea kudanganywa tukiambiwa ukweli inakuwa tatizo.

    ReplyDelete
  21. Sh. 200/= kwa Mafisadi ni ndogo lakini kwa sisi Wangere mange ni kubwaaa,,,unakuta mtu unaua kenge kwa kutembea kwa mguu huko utokako ukielekea Kigamboni ili mradi unabakisha angalau Sh. 100/= uweze kuvuka tu!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...