Ni miaka 15 sasa tangu ututoke mpendwa kaka yetu Juma Hassan Sanga. Ni vigumu kukubali kwamba hakika mpendwa wetu Juma uliondoka kama utani. Umetuachia majonzi makubwa ndugu zako ambayo hayataisha mioyoni mwetu kamwe. 

 Mama yako mpendwa Mariam Sanga na Baba yako mpendwa Hassan Sanga wanakukumbuka kila kukicha hawachoki kukuongelea Juma wetu. Ulikuwa mcheshi mwenye upendo na haruma kwa familia zote. Ulikuwa Kaka mkubwa katika familia yetu tulikutegemea sana kwa ushauri na busara zako Kaka. 

 Kwetu sisi kama wadogo zako Athumani, Rehema na Aziz hatuishi kukumbuka wenzio na tuna imani kubwa sana Kaka yetu ipo siku tena tutakuwa pamoja. Kwa kweli pengo lako uliloliacha kamwe halitazibika. Wajomba na wakina Mama mdogo, pamoja na jumuiya yote ya Ilala maghorofani, marafiki na majirani wote wanakukumbuka sana Juma kwa ucheshi wako.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi Juma. 

 AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. RIP bro Sanga. Nimeguswa na ujumbe. Ama kweli vizuri havidumu.

    ReplyDelete
  2. siwezi amini Juma amefariki maskini Inna lillah wainna ilayhi raajiun..tulikuwa tukifanya kazi wote katika mambo ya tickets airline na kimjinimjini 17 yrs ago..mwenyezi mungu ailaze pema peponi..Prince

    ReplyDelete
  3. R.I.P Juma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...