Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tano mstari wa mbele kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde, Ikulu, Dar es Salaam, iliyotwaa ubingwa wa Chalenji 1994, Nairobi Kenya. Katika picha hii wamo pia wanahabari walioripoti fainali hizo.Kutoka kushoto mstari wa mbele ni; Mpigapicha Richard Mwaikenda (wa gazeti la Mfanyakazi ambaye kwa sasa ni Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo na Mmiliki wa Blogu ya KAMANDA wa  MATUKIO), Kuwayawaya S. Kuwayawaya, Mbunge wa Dodoma aliyekuwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, aliyekuwa Waziri wa Elimu na Michezo, Profesa Phillemon Sarungi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (TFF), Muhidin Ndolanga, Marehemu Moses Nnauye wa CCM, aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa Daily News mdau Muhidin Issa Michuzi (Sasa ni Mzee wa Libeneke la Michuzi Blog). Mstari wa katikati kutoka kushoto ni; John Hokororo (MAELEZO ), aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makame Rashid, James Nhende (aliyekuwa Mhariri wa Michezo gazeti la Mfanyakazi na sasa ni mhariri wa gazeti la MZAWA, Mwanza),aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo gazeti la Uhuru, Godfrey Lutego (hivi sasa ni Mkuu wa Kitengo cha Matangazo gazeti la Jambo Leo),Japhet Sanga (alikuwa mwandishi wa gazeti la Daily News na sasa ni afisa wa habari wa Tanzania Media Fund), aliyekuwa Meneja Usambazaji wa gazeti la Mfanyakazi, Richard Ndasa (sasa ni Mbunge wa Sumve) aliyekuwa Katibu Mkuu wa FAT, Ali Mwanakatwe, Aliyekuwa Mpigapicha wa Mfanyakazi, Deus Mhagale (sasa ni mpiga picha wa gazeti la Mtanzania), aliyekuwa Mhariri wa Michezo wa Daily News na Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Stephen Rweikiza na aliyekuwa Mpigapicha wa gazeti la Mfanyakazi, Joseph Senga (sasa ni Mpigapicha Mkuu wa Tanzania Daima). Wengine msitari wa nyuma kutoka kushoto ni; Mwandishi wa habari Edmund Msangi na Evarist Mwitumba ambaye ni Mhariri Mkuu wa gazeti la This Day .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. michuzi kweli we ni mfano wa kuigwa maana unatukumbusha mbali sana na hizo picha sio wengine kila kukicha diamond na wema mara uwoya great job mkuu

    ReplyDelete
  2. Kamati ya Saidia Taifa Stars inshinde 1994;

    Tukiacha waliotangulia mbele za Haki kwa Mwenyezi Mungu waliobaki ni muhimu saaana kwa Maendeleo yetu ya Soka Nchini kwa sasa ili watoe SIRI ya mafanikio yale!

    ReplyDelete
  3. Ankal umechakachua kapshen ya picha espeshale maelezo juu yako wewe. Eniwei, hongera ankal kwa nafasi mpya

    ReplyDelete
  4. Katika wote hawa, aliyevunja rekodi alikuwa ni Richard Mwaikenda (wa kwanza kushoto mbele). Maana hata mavazi ya enzi hizo ni kivutio kweli kweli. Mwaikenda wakati huo alikuwa JuA Kali kweli kweli, maana ni yeye aliyevaa raba tu!

    ReplyDelete
  5. watu wanakua na umri unakwenda ila huyu mshikaji wako Richard Mwaikenda na Blog yake ya Mzee wa matukio duh huyu jamaa hakui, ni aibu tupu , anamix habari za ngono humohumo ndo mana haisomwi sana, hana adabu kabisa, ankal toa reference yako pale katika blog yake mana ni aibu na ndege wa rangi moja huruka pamoja, atakuaibisha, hebu angalia anaweka eti maombi ya kazi afu picha za uchi na hamna warning yoyote ukitaka fungua blog yake afu commet zote za matusi aibu sana mru mzima huyu aliwakilisha taifa na heshima ya kukutana na watu waheshimiwa kama hivi, jifute kule ankal HANA ADABU HUYO MWENZAKO sio yule tena nilifungua nikiwa na mwanangu ikabidi nimfukuze

    ReplyDelete
  6. yaani michuzi we kweli uko juu. jamani hiyo picha mi nimeipenda kweli. je naweza kuipata? yaani mzee mengi na afro yake du. yani walikuwa vijana hasa.

    ReplyDelete
  7. Ni kipi cha kukumbukwa na wapenda soka nchini baada ya kuundwa kamati hiyo? Ni mafanikio gani yalipotikana?

    ReplyDelete
  8. Mdau Anyomonous wa Sat Jan 21, 12:05:00 PM 2012

    Unayesema...Ni kipi cha kukumbukwa na wapenda soka nchini baada ya kuundwa kamati hiyo? Ni mafanikio gani yalipatikana?

    SWALI LAKO NI ZURI SANA:

    NI WAZI KUWA KAMATI HIYO HAIKUDUMU!

    UWEPO WA KAMATI HIYO ULIATHIRIWA NA SIASA, HUJUMA NA UBABAISHAJI KITU AMBACHO NDIO MCHAWI MKUBWA KWA MAENDELEO YA SOKA NA MAMBO MENGINE MENGI YA TAIFA LETU TANZANIA!

    ReplyDelete
  9. Mkuu kama nakufananisha hapo, je upo kwenye picha hii?

    ReplyDelete
  10. HII ILIKUA SAIDIA SIMBA ISHINDE. AU HAMNA MACHO WAJAMENIII?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...