Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hapo mheshimiwa anaruka nini, mbona sikioni?

    ReplyDelete
  2. Picha ya mwisho...mkuu anaogopa kutumbukia majini wakati yupo mbali kabisa...yaani anachungulia kimtindo ila kusogea kidogo 'never!' Hahaha!

    ReplyDelete
  3. Wachina tulikuwanao sahani moja miaka 50 iliyopita,wenzetu waliwekeza kwenye elimu Hawakuwategemea wawekezaji kama sisi.
    Sasa wenzetu nasio mabomu kila siku mavyuoni kwa kuzuia vijisenti vichache tu vya ubwabwa, je kuwekeza kenye tafiti za kisayansi na maendeleo si tutaishia kuota tu.
    Sasa hako kajiukuta katatafutiwa mwekezaji au kakijengwa ndo katakua mfano wa maendeleo ktk sehemu hiyo kwa miaka 5 ya uongozi.
    Bila elimu tutaishiWa kuliwa na wawekezaji!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Nilitembelea Pangani mwaka 1992. Watu wa huko walikuwa ni conservative sana. Sijui kama hali imebadilika au la.

    ReplyDelete
  5. kama kawaida yetu mpaka jambo lifikie hali mbaya na wakubwa waje kushuhudia ndio tuanza kulishungulikia. swala la huo ukuta wa mawe kuwa unabomoka ni la siku nyingi sana nashangaa mpaka leo hii bado halijashungulikiwa, tunasubiri wafadhili anyway tutafika tu!!!

    ReplyDelete
  6. Hongera Luten mstaafu mheshimiwa chiku Galawa.Nyota yako inang'aa.Ex katibu Bunda DDH.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...