Mdau Michuzi,
Imekuwa ni jambo la kawaida sana kwa hapa Zanzibar (pamoja na kwengineko Tanzania) kwa madereva kushindwa kutumia vifaa sahihi pindi wanapoharibikiwa na gari zao. Mara nyingi madereva hawa huamua kuweka kati kati ya barabara vitu kama majani, matairi au hata mawe ili eti kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara kwamba mbele kuna gari limeharibika!! Mbaya zaidi ni pale vitu hivi vinapowekwa hata usiku, ni jambo la kushangaza sana!
Leo hii, hapa Zanzibar nimeona jambo geni kwangu ambalo ni zuri sana kuigwa na madereva wote waungwana wanapoharibikiwa na gari zao, jambo hili ni kuona kwangu kwa dereva kutumia kifaa sahihi kinachostahili kutumiwa ili kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara, ni matumizi ya reflexive triangles.
Dereva wa gari hili kama linavyoonekana amefanya wajibu wake alipoharibikiwa na gari kwenye kona ya nyumbani kwa Mheshimiwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi eneo la Maisara Mjini Unguja. Hapa Zanzibar zaidi ya asilimia 98 (98%) ya madereva hawauelewi wajibu huu!!
Naomba kitendo hiki kitiliwe mkazo na Mamlaka husika, kila gari ni lazima liwe na zaidi ya reflexive triangle moja ili iwe ni sheria kutumika kama hakuna sheria ya matumizi yake kwani inaweza kuepusha ajali nyingi zinazotokea hasa baada ya jua kutua (usiku)
Mdau zaidi ya idadi kubwa ya Madereva kushindwa kutumia alama sahihi na kanuni za udereva, mambo haya mawili ni muhimu:
ReplyDelete1.Madereva kuwa wana pimwa afya mara kwa mara ,afya ya maumbile na afya ya akili,,,kwa kuwa ubinaadam mtu anaweza akawa mzima anapopewa leseni na baada ya muda akawa si mzima kiafya.
2.Mafunzo elekezi ya mara kwa mara, hasa kwa wanaopata ajali ili wakumbuke kanuni.
Tanzania hapa mtu kishapewa leseni inakuwa kama zawadi ya milele na milele, inawezekana madereva wetu wengine ni wagonjwa wa kichaa,kifafa cha ukubwani au utaahira!
yeye anajali lakini hao wengine unadhani wanajali,wanaweza hata kuikanyaga hiyo alama,bongo watu vichaa.
ReplyDeleteAnkal Zaidi ya hoja ya Usalama barabarani Zanzibar, ile HISTORIA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR...
ReplyDelete'2012 SHEEP PRODUCTION' ni sanaa tupu hakuna ukweli pale ,ile video imetengenezwa!
DALILI ZA UONGO:
1.Thamani ya picha (quality) kwa mtu mwenye hulka za kijasusi kama mimi ataelewa wazi kuwa ni animated..imechezeshwa kwa komputa au video ni ingine imetiwa mkono ili kufikia lengo.
2.Hapakuwa na utaalamu wa picha kwa kuchua tukio kama vile mwaka 1964.
3.Waliouliwa 10,000 walikuwa wamefungwa kamba za minyororo? ,hadi wanamalizwa hata kama wauaji wana bunduki?
4.Mwarabu alikuwa amejiimarisha ana kwa idara zote, isingekuwa rahisi mauaji ya kiasi hicho kujiri.
5.Idadi ya watu Zanzibar wakati huo ilikuwa ni ndogo sana sio rahisi watu 10,000 kuuawa.
hiyo labda zenji tuu bongo kuna vibaka wataiba
ReplyDeletekwa zenji o.k bongo mmmmmmmmmmmmm vibaka
ReplyDeleteHata hivyo, sheria ya trafiki ni kuweka alama hiyo mita 200 kutoka kwenye gari iliyoharibika na sio mika 15. Gari inakuja nyuma yaek sio baiskeli, inahitaji kuona kibao na baada ya hapo kuanza kuchukua tahadhari ya kupunguza mwendo.
ReplyDeleteMpwa, Kama kibao hicho kingewekwa mita 200 kama inavyotakiwa jamaa wangeki-beba na kushia nacho,ndio maana jamaa akaona ni heri kuweka mita 15 ili aweze kukipigia chabo..
ReplyDeleteWajinga ndio waliwao!
ReplyDeleteMajani ni alama nzuri na yanatambulika kimataifa..wewe hujaendesha 'safari ndefu' huko maporini ndiyo maana unadharau hayo majani..Angalizo..Gari likipona basi na majani yaondolewe..!Majani kwenye safari ndefu yanatoa tahadhari nzuri sana yakiwekwa kwa urefu wa kutosha na hasa kwenye 'blind corners'
ReplyDeleteDavid V