Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akimkabidhi Zawadi iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mwakilishi mkuu wa JICA wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.
Mwakilishi mkuu wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) Bw. Yukihinde Katsuta akitoa maelezo juu ya ukamilishwaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania uliofadhiliwa na serikali ya Japan kwa lengo la kupunguza maambukizi ya VVU sanjari na usambazaji wa vifaa vya kupimia maambukizi hayo na kuahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania katika utoaji wa vifaa vya kutolea huduma za afya.
Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akizungumza watendaji wa Wizara hiyo na wawakilishi wa Shirika la Kimataifa la ushirikiano wa kimaendeleo la Japan (JICA) wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini ulioanza mwaka 2009 chini ya ufaufadhili wa serikali ya Japan, jijini Dar es salaam.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya afya na wawakili kutoka Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya ukamilishaji wa mradi wa kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini uliofadhiliwa na serikali ya Japan jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Eh kwanini umefungwa?VVU vimeisha?

    David V

    ReplyDelete
  2. ILIKUWA DILI ZA ULIMWENGU ULIOKWISHA ENDELEA SASA KILA NCHI WAMEISHA GUNDUA DAWA KWA HIYO HAKUNA WA KUUZIWA KUTOKA DOLLERS 10,000 KWA MWEZI SASA ZINAUZWA SHS 5000/= KWA MWEZI INA MAANA MARKET IMEPUNGUA NA VIFO VIMEPUNGUA KWA ASILI MIA 70% KWA HIO INA MAANA KUNA MAFANIKIO BAADA YA KUPATIKANA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA . MTU ALIYEAMBUKIZWA NA VVU HIVI SASA KAMA ANATUMIA DAWA ANAWEZA KUISHI MPAKA MIAKA 40 MINGENE IJAYO, SASA HIYO INAONYESHA JINSI GANI DUNIA ILIVYO PROGRESS KWA HILO HIVYO VVU SIO TISHIO TENA WEWE TIA TU HATA BILA KONDOM UTAISHI KAMA MTU WA KAWAIDA.

    MDUA ATLANTA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...