Brother Michuzi naomba nipostie tangazo langu katika blog yetu ya jamii kwani kama mmoja wa wanajamii natafuta jiko.

I am a 36 years old Tanzanian gentlemen looking for someone serious for serious relationship wherever this blog is read.

 I am 6ft ''1 tall with 90kg (though am working out), I live and work in Dar es Salaam Tanzania. I would prefer my juliet to be 5ft "6 tall and above and at least less than 75kg. 

 I would love the responses to be channelled to my e-mail address ..nzagamba1975@gmail.com

Nimeamua kuleta ombi hili jamvini hapa maana katika kutafuta jiko unapaswa kua na macho mapana zaidi. Asanteni sana.

Mdau Nzagamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Hilo jiko unalotafuta la kuni,gas,mkaa,mchina au umeme??elezea vzr plz??na uangalie vzr cse utafungiwa mbuzi kwenye gunia....oooohhhh,

    ReplyDelete
  2. Watu hawatafuti majiko mitandaoni. Mke mwema mtu hupewa na Bwana. Omba Mungu halafu fungua macho ya kiroho na ya kimwili.

    ReplyDelete
  3. Have you been married before? if not why have you taken so long. 36 years?

    ReplyDelete
  4. Your BMI is more than 27. You are so overweight and you will soon become obese. Bila shaka magonjwa kama BP, kisukari nk vinakunyemelea. Take care of your health!

    ReplyDelete
  5. mdau wa pili acha kukatisha watu tamaa, na pia kuwa open-minded katika karne hii.
    Unaelewa nini maana ya mtandao??
    Hujui generation hii ni tofauti na ya kale? zamani watu ilibidi wakutane sehemu fulani tu, lakini sasa ni internet na digital age, watu ndiko hukutanika zaidi kirahisi na haraka zaidi.
    Au unamaanisha kuwa watu wanakuwa mitandaoni ni wa shetwani??
    Mbona tunatabia ya kujiona wema na bora kuliko wengine?? Thats very wrong.
    Hakuna binadamu aliye perfect isipokuwa MUNGU peke yake, tuwe wanyenyekevu.
    Mitandaoni kuna watu wa kila aina, hivyo mdau endelea na juhudi zako kutafuta mwenza wako kwa njia hii pia huwezi jua mola kakupangia utampata wapi na vipi.

    ReplyDelete
  6. masihara hayo!huyo mtu hata akikutumia hiyo e mail na picha kuhusu huo urefu mapaka hizo nnchi unazotaka utahakikisha vipi?

    ReplyDelete
  7. Sawa Mdau Nzagamba,

    Ombi lako litafuatiliwa na panapo uwezekano hata PASI au KROSI utapigiwa!

    Msimcheke au kumbeza Mdau kwa kuwa suala hili ni nyeti sana kwa muda wetu huu wa Zama hizi kwa kuwa wengi watauliza na watatoa kejeli kama:
    -Ohh muda wote huwo alikuwa wapi mpaka anafikisha 36?
    -Ohh mbona hatoi picha?
    -Ohh hajatoa undani wa historia na wasifu wake kama aliwahi kuoa kabla au amesha zaa watoto na mwaamke mwingine?
    -Ohh kwa nini asitafutie kwa watu wake wa karibu?

    Ukweli ni kuwa usihoji sana, kila aliye katika hali hii ana sababu zake za msingi kabisa, kama unaweza toa Ushirikiano ili yeye afikie lengo lake!

    ReplyDelete
  8. Mimi nina sifa zote but nimeachika mara 5....nipo nakaa kwa mtogole...
    email yangu ni khanga1@hotmail.com
    nitakupenda mpaka ushangae

    ReplyDelete
  9. Mdau wa MaguJanuary 28, 2012

    Wewe mchangiaji wa pili Huyo mungu unamjua wewe. Achana na vitu vyakufikirika.Kabla ya ukoloni wa kizungu na kiarabu na ukristu na uislamu wao watu walimwomba nani mke mwema? Tembea duniani uone diversity katika imani hapa ulimwenguni. Mwanawane Nzagamba hii ndio chagulaga ya kileo, endelea kusaka mke vyovyote vile. Kupata mke au mme mwema ni kama pata potea. Waungwana wameambulia wenza vimeo makanisani na misikitini. Hapa bongo tutaanzisha dini yetu sisi maa Atheist ndo mtanyooka.

    ReplyDelete
  10. Ila bwana Mkubwa Mdau Nzagamba, mashariti yako ni mengi na ni magumu kwa idadi ya wanawake wengi!

    Licha ya vigezo vingine muhimu vya sifa za Mwanamke anayefaa,

    UZITO:
    Idadi kubwa na Wanawakw wana ile hulka ya kula kula tena lishe ni Chipsi mayai hivyo hata ukute Mwanamke Kimbau mbau ni vigumu kupata mtu wa uzito chini ya 75kg.

    UREFU:
    Wanawake wengi ni Vibushuti/ Emolo/Vijeba au Wafupi.
    Wanawake wenye urefu wa Futi 5 na nchi 6 ni wachache,wengi wao wamesha hodhiwa na Wadau wa Mitindo na Masaluni kwa biashara zao, hivyo mwanamke wa aina hiyo kwanza anajiona Miss (Mrembo) atakusumbua sana!

    Sikukatishi tamaa cha msingi, Zaidi ya sifa zingine za Mwanamke jaribu kuzunguka na vitu viwili mkononi (i)Mizani (ii)Kipima urefu, ili ujaribu bahati yako na ufikie Lengo!

    ReplyDelete
  11. ujue i am tired na watu ambao bado wana fikira eti mitandaoni watu sio real....kwani wewe ulipo mtandaoni ni mwendawazimu?watu need to wake up and realise mitandaoni unaweza kumpata mtu ambaye bora zaidi na Mungu aliye kupangia....Mungu doesnt have limitations if you are trust God..He is the Almighty He can make things happen when you expect the least at a place and time you never expect...remember THIS is a digital age!!i understand its somehow risky so does even mitaani....the only thing is to be careful and take time even if mtu ukampata mitandaoni au porini au mitaani etc..so wake up!!i only date online and trust me i get the best women on earth,...educated God fearing family based......anything is possible acheni ugiligili wabongo..Mdau CA

    ReplyDelete
  12. ungejieleza kidogo kaka mambo muhimu kama dini, kazi na hata kabila. sasa mtu atavutiwa na umbo lako na uzito?

    ReplyDelete
  13. Mdau namba mbili ni heri umwambie, mke mwema mtu hupewa na Mungu haijalishi ni mrefu au ni mfupi ni mweusi au ni mweupe, ameajiriwa au hajaariliwa, mm huwa nashangaa sana watu vigezo vyao wanapo tafuta mke/mume. Kumbuka kwamba anachokupa Mungu utainjoy sana na hata kukiwa na tatizo utamwendea yeye aliyekupa. Natamani niweke ushuhuda wa jinsi nilivyompata mume wangu lakini nadhani sio mahali pake. Ubarikiwe mdau unayetafuta mke

    ReplyDelete
  14. nyie wote mnaojifanya wa kileo kama mnavyojieleza mimi kwa ninasema nyie ni wajinga lakini hamjijui huu wakati na vyombo vya kisasa kama mnavyoita kuna maana nyingi sana kwa waelewa swali moja lakini samahani sana mama zetu walipatikana mitandaoni?....kuweni makini sana.Mwanamume aliyetimia hatafuti mwanamke mtandaoni.

    ReplyDelete
  15. Kijana mimi nilishawatafuta sana hapa mtandaoni na sikumpata hata mmoja.Ila kimsingi wanawake wa hapa mtandandaoni wanalichukulia suala hili kama ubishoo na lisilo na tija kwao.
    Nakushauri umtafute unayempenda kupitia njia nyingine siyo mtandaoni.Muombe Mungu atakupa unayemtaka bila kikwazo chochote.

    ReplyDelete
  16. yaonekana unatafuta miss, huo urefu wanawake wengi hawana. mie watu wananiona mrefu sana na niko 5ft 4inches.

    ReplyDelete
  17. kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  18. Uwee mbwanee Nzagamba msongu uduma ku intaneti nee?? Nenda kukaa ku Lyamba kwaso asongu akolee aza ibee.

    ReplyDelete
  19. Vipi una ndevu au hauna? eee!

    ReplyDelete
  20. We mwenyewe una 90 kg halafu unasisitiza kupata asiye zidi 75kg,that is why you are still single, and if you are not going to change your altitude you will die a lonely heart man !

    ReplyDelete
  21. Uwee mbwanee Nzagamba, msongu akole kukaa kwasho ku lyamba.
    Sasa fanya ufunge safari ukachukue mmoja.

    ReplyDelete
  22. PICTURE PLEASE!

    ReplyDelete
  23. kwani tangazo ilikuwa lazima liwe kwa kuzungu? Introduction na conclussion kwa kiswahili, ujumbe kwa kizungu........ au ni copy and paste?
    kaazi kweli

    ReplyDelete
  24. wewe kafanye mazoezi punguza uzito wako,ukifikia kwenye 70kg utapata mke.

    ReplyDelete
  25. Mhh muacheni jamani kupanga ni kuchagua!

    ReplyDelete
  26. Mnhhh utakuwa mvivu ktk sita kwa sita na mara nyingi utataka ukae juu!!!,,,kwa uzito wako wa Kilo 90 na mimi niwe na kilo 75,,,lohhhh usije ukanifia Kifuani mwana wa mwenzio !

    ReplyDelete
  27. JE UNA KITAMBI, UNAKUNYWA POMBE? UNAVUTA SIGARA? UNAFUGA NYWELE (RASTA)UNA KIPARA AU UMENYOA STAILI YA UNGA? JIELEZE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...