MWALIKO WA WADAU KUTOA MAONI KATIKA MUSWADA WA SHERIA MBALIMBALI ZA BIASHARA "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011"
(PUBLIC HEARING)

Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara inawaalika wadau wote kwenye mdahalo wa kupokea maoni kuhusu Muswada wa Sheria Mbalimbali za Biashara "THE BUSINESS LAWS (MISCELLANEOUS AMENDMENTS) ACT, 2011". Kikao hicho kitafanyika kesho tarehe 26/01/2012 katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam kuanzia saa 4.00 asubuhi. Lengo la Muswada huu ni kufanya marekebisho katika Sheria mbalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania. Sheria zinazopendekezwa kurekebishwa ni:


1. Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara (Sura ya 213)
2. Sheria ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Sura ya 155)
3. Sheria ya Makampuni (Sura ya 212)
4. Sheria ya Bidhaa ya Biashara (Sura ya 85) na
5. Sheria ya Mipango Miji (Sura ya 355)

Nakala za Muswada husika zinapatikana Ofisi ya Bunge iliyopo Mtaa wa Shaaban Robert, Jijini Dar es Salaam, na wahusika wamuone Ndg. Kaboneka (Simu 0755-362852).
Karibuni nyote ili tuweze kuboresha Muswada huu .
Imetolewa na Idara ya Habari,

Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimatifa

DAR ES SALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. BINAFSI NASHUKURU SANA KWA MWALIKO, ILA NI VIZURI KWA OFISI KUBWA KAMA BUNGE, KUZINGATIA MAENDELEO YA KITEKNOLOJIA KATIKA KUWAHUSISHA WATANZANIA, TUNAOMBA NAKALA YA MUSWADA HUU IWEKWE KATIKA TOVUTI ILI WALE WASIOWEZA KUFIKA HAPO OFISI ZA BUNGE WAPATE PIA NAFASI YA KUUONA NA KUTOA MAONI YAO.

    ReplyDelete
  2. Mumezungumzia vitu ambavyo mtazungumzia hapo lakini kitu kimoja muhimu ambacho kitawafanya wafanya biashara wengi kuwa na moyo wakufanya biashara zao kwa amani ambacho nikumulika Rushwa za TRA ambazo zinaangusha watanzania wengi na ningeomba kama Diaspora wako na mwakilishi wao tanzania asikose kwenye mkutano huo nimuhimu kwa watanzania walioko nje!

    ReplyDelete
  3. Linus RweikizaJanuary 25, 2012

    Bw. Simime ameniwahi. Nami naungana nae kwamba draft iwe linked kwenye tovuti kadhaa ambazo watu wengi wanazifikia mara kwa mara ili michango mingi ipatikane. Otherwise, nawapongeza sana kwa juhudi hizi za kuwahusisha wananchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...