Mzee Yusuf (kulia) akiwa na mdau wa New York Shaban wakipata picha ya mara Mzee wa kurambisha alipotembelea Ofisi za Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa New York. 
 Mzee Yusuf (shoto) akipata picha ya pamoja na mashabiki wake na Afisa Ubalozi
 Mzee Yusuf (kati) akipata picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi.
 Mzee Yusuf akipata picha ya pamoja na mmoja ya wafanyakazi wa Ubalozi.
 Mzee Yusuf akipata picha ya pamoja na mmoja ya wafanyakazi wa Ubalozi.
 Mzee wa kurambisha akipata picha ya kumbukumbu Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Kimataifa, New York.
Mzee Yusuf (wa pili toka shoto) akipata picha ya pamoja na maafisa Ubalozi, Shaban (wa pili toka kulia) Mdau wa New York na Maporomota wake, Mao Luangisa (shoto) na Tahir Gharib (kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Naona walimwandalia chupa ya kunyonya, hivi jamaa bado ananyonya?

    ReplyDelete
  2. Swadakta.. mmh! huyo binti aliyesimama na Mzee Yusuph mwenye blauz rangi ya machungwa ni mzuri jamani.. safi sana bibie!

    ReplyDelete
  3. SASA MZEE YUSUF NAYE HATA KAMA NI MSANII MAVAZI YAENDANE NA SEHEMU..CHENI ZA NINI SEHEMU KAMA HIZO..BALOZI MWANAIDI ALIKUWA HAKI KUSEMA YUPO BUSY,HAWEZI KUONANA NA WEWE...

    ReplyDelete
  4. Maporomota hahahahahahahah...

    ReplyDelete
  5. Mao!Umekuwa mkubwa hivyo!Ndugu zako wote hawajambo!Kina Rose,,,,Ni mimi Dada yako Hanifah,,Upanga Lugalo!

    ReplyDelete
  6. Maishani kila mtu na bahati yake.

    ReplyDelete
  7. mmmh mzee yusuf hiyo jeans haijachafuka? au ziko nyingi naona toka umeteremka bado imeganga mwilini tu!

    ReplyDelete
  8. Kwanini mnamuita mzee kijana wa watu.

    ReplyDelete
  9. kwa hiyo ,ulitaka avae sutu ?? angelikuwa 2 pack au Michael Jackson kwako ingelikuwa sahihi kupozi na chain au jeans ya kizazi kipya, badala ya kushangilia kwamba siku hizi hata muziki wetu wa taarabu utauzwa hadi marekani,na mzee Yusufu anapotajirika ni moja ya msaada kwetu maana atainvest hapa hapa tanzania, kama vile atanunua shamba au atajenga nyumba ya vyumba vinne ambayo mimi na wewe tutapanga. pamoja na hayo, please naomba kujua namna ya kuweka tangazo langu kwenye blog hii ,nina mashine za kukamua na kupeki juice kwenye mapakiti, ninatafuta aidha ubia au kuiuza ,ninapatikana kwenye email hii jacobmayillah@hotmail.ca

    ReplyDelete
  10. mzee yusuph mbona umeacha mdomo wazi??au huyo mrembo ulipozi naye kakufurahisha sana??

    ReplyDelete
  11. Maisha bora kwa kila Mtanzania!

    ReplyDelete
  12. Naona jamaa amevaa kibongo fleva.

    ReplyDelete
  13. Mimi nawapenda sana hawa wafanyakazi wa ubalozi wetu, yaani wao huwa wana muda tu...kazi kwako tu kuleta ishu. Safi sana, tupo pamoja!

    ReplyDelete
  14. neema maa nakuona unawaka wakaa kama nyota ya jaa uko juu mammaa nakufagilia.tahir mbona umezeeka mshikaji tatizo nini babaaaa eeeh au bado una miss mama watoto wako wa zamani

    ReplyDelete
  15. Acheni roho mbaya. Mzee Yusf kapendeza. Na hiyo jeans ni fresh na chain ni freshi. Avae suti kwani anaenda kufanyakazi ubalozi wa Tanzania? Viroho korosho tu? Mzee wa kurambisha furahia safari yako ndugu. Mziki wkao ni bomba sana tena sana. Wafuasi wako tuko wengi na kila siku nasikiliza nyimbo zako zinznichengua sana. Utunzi,uimbaji ni vipaji vyako. Achana na wenye roho za kutu! Aluta Continua! Ukirudi angusha kitu kingine! Albamu na video mpya!

    ReplyDelete
  16. hilo sweta la Mzee Yusuf ni kubwa sana.lol

    ReplyDelete
  17. Lakini Wabongo mna maneno jamani!Mimi nakufa mbavu kwa kucheka,,huyo mdau hapo juu,kamfagilia kwanza mzee yusuf kisha anaomba wamsaidie jinsi ya kutuma tangazo lake kwa Michuzi,,sasa mdau hueleweki,unataka kuuza Juice au kuiuza hiyo mashine?kama ukiwa tayali kwa chaguo moja,,,angalia pale kwa michuzi juu utaona Email yake..kama sikosei ni issamichuzi@gmail.com !!!!Ee mdau umenifurahisha sana,,Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  18. Kweli Mdau Ahlam,,,UK.

    Umetoa Ushauri wa Busara kwa Mdau wa MASHINE YA JUISI!!!

    Masuala binafsi ya Kibiashara ya namna hii ni bora angewasiliana na Ankal kwanza moja kwa moja kwa faragha akachambua mbivu na mbichi ili ajue naye atakalia wapi(si unjua mambo ya Panga au Ganji kuona?),,,halafu kwa vile Michuzi ni mtu wa Libeneke angeturushia sisi wengine!

    ReplyDelete
  19. Naomba namba ya simu au email ya huyo dada aliyependeza, naweza kujiua nisipoipata.

    ReplyDelete
  20. Wewe Anonymous wa Sat Jan 21,12:58:00 PM 2012 unaetaka namba ya simu au email ya dada aliyependeza nguo za Rangi ya Machungwa.

    Utamweza demu huyo?,,,enheee kizuri chajiuza, mtoto anafanya kazi yake nzuri Ubalozini Marekani ametulia tuliii ukiona mtu wa hivyo siyo Demu Mchaluko ni mtu ana heshima zake!

    Ya nini namba ya simu au email?,,,kama upo Marekani nenda zako moja kwa moja hadi Ubalozini ukamwage sera zako, na kama haupo huko fanya mipango ya kufika kwa Obama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...