Naibu waziri wa kazi na ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akipata maelekezo toka kwa mkuu wa kiwanda cha sukari cha TPC kilichopo mjini Moshi,pindi alipokitembelea kiwanda hicho hivi karibuni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho wakipanga mifuku ya Sukari.
Wafanyakazi wa kiwanda cha sukari TPC wakimsikiliza naibu waziri wa kazi na ajira Dkt.Makongoro Mahanga (hayuko pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao.
Naibu waziri wa kazi na ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha TPC (hawako pichani)
Mwenyekiti wa TASIWU tawi la TPC Juma Bilali akitoa kero za wafanyakazi kwa Naibu Waziri,Dkt. Makongoro Mahanga.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
Hao vijana picha pili kutoka juu,wapatiwe mavazi(au PPE) yanayoendana na hilo eneo wanalofanyia kazi(kiwandani)..Hilo ni eneo la kiwanda-ni hatari.Nazungumzia mambo ya usalama(Safety)
ReplyDeleteDavid V
Huyu Naibu WAziri mimi namshangaa sana sisi wakazi Jimbo la Segerea pia tunamshangaa wananchi wake wamepata na mafuriko kuanzia buguruni mapaka bonde la msimbazi pale vingunguti sijamsikia hata akisema anaenda kuwapa pole na ndio hao waliompa kura yetu dah wabunge wetu bwana, bora mimi nilimpa Mpendazoe japo Hakupita lakini kura yangu ilienda kihalali... nawapa pole wale waopelekwa pelekwana CCM, kura mmetoa matokeo yake ndio hayo...hasa wale wakazi wa Buguruni ndio waliogawa sana kura kwa huyu baba.................SIMPENDI KWA KUWA HAKUNA ALILOFANYA TOKA AWE MBUNGE..................usibanie comment
ReplyDeleteHuyo Naibu Waziri wa Kazi mbona amveaa helment ya mtoto mdogo
ReplyDeleteMbona huyo Mfanyakazi katika picha ya kwanza hana helmet na amevaa kofia ya karatasi. Kama kuingia katika hio sehemu inatakiwa uvae helmet, huyo mkuu wa kiwanda haoni kampuni yake ina vunja sheria ya usalama kwa wafanyakazi wake?
ReplyDeleteSAWA USALAM: MTU KUBEBA MFUKO WA SUKARI KICHWANI? INA MAANA HAKUNA VITENDEA KAZI? PENGINE HUO MFUKO NI KILO 100, NAJUA HICHO KIWANDA HAKISHINDWI KUNUNUA FOLKLIFT.
ReplyDeleteUSALAMA WA WATU KAZINI NI MUHIMU.