Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jijini leo DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati (Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje, (kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini leo kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia) , hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje.
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia),wakionyesha mikataba waliyoisaini wakati wa hafla hiyo iiliyofanyika leo jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje.
Mkurugenzi Mtendaji wa TDPC Bw, Yona Killagane akitoa maelezo mafupi Jan 24,2012 kabla ya kusain i mkataba wa utafiti wa mafuta nchini utaozishirikisha kampuni tatu kutoka nje, Kampuni hizo ni Petrobras, Heritage na Motherland Industries Limited.
Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw, Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafii wa mafuta kutoka kampuni za nje leo wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo jijiji Dar es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mh, nina shaka

    ReplyDelete
  2. wazanzibar tumekwisha sasa mafuta byee

    ReplyDelete
  3. mungu usitujaalie kuwa na mafuta nchi yakasababisha tukakosa amani kama wenzetu wa libya na kwengineko.

    ameen.

    ReplyDelete
  4. Mhe.Mmeusoma vizuri huo Mkataba??msije tu kutupeleka kulekule.

    ReplyDelete
  5. Mhe.umeusoma vizuri lakini??

    ReplyDelete
  6. Wahindi lini wakachimba mafuta,hao ni wezi tuu. Ningekuwa waziri nisinge ingia nao mkataba. Si mnajuwa tena wana uwezo hata wakunadi picha ya Rais mbele yake kujipatia point na je tumesahau hayo ya reli ya kati. Kwa nini sisi Watanzanaia tunawatukuza hawa Wahindi ingekuwa hata vizuri kuwapa hiyo mikataba Warusi kwani wana utaaramu wa hali ya juu. Tukiendelea hivyo sijuwi kama tutafika au sivyo Yesu atatukuta bado tupo njia panda!!!!

    ReplyDelete
  7. Mikataba ya Tanganyika tayari hiyo Jee ya Zanzibar itasainiwa lini??

    Kuuliza si ujinga!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Eti Bwana Sood kutoka India. Huyo kweli ni Muhindi hata wewe kwa akili zako ukimtazama?

    ReplyDelete
  9. he, hivi ngeleja bado ni waziri tu! na mikashfa yote hiyo! kweli bongo tambarale!

    ReplyDelete
  10. mnafikiri mtakuwa matajiri kama waarabu, hamna.

    mtakuwa kama naijeria, nayo ina mafuta.

    kama tumeshindwa kuwa matajiri kwa dhahabu, almasi, tznite n.k. itakuwaje mafuta?

    ReplyDelete
  11. Hivi haya Mafuta yanatafutwa milele.Serikali yetu kila kukicha inaingia mikataba ya kuchimba mafuta. Mara ya kwanza walikuja Waholanzi wakatafuta weee, hatukpata matokeo. Sijui wakaja Wamarekani nao hatukupata matokeo ya utafiti wao.Sasa Wabrazil nao wamekuja kujizolea pesa za wajinga wajinga.

    ReplyDelete
  12. Labda wanatoa 10%

    ReplyDelete
  13. Hii Mikataba ingefaa iwekwe HADHARANI KABLA YA KUSAINIWA!

    KWA NINI YALIYOMO IWE NI SIRI KATI YA WANAOSAINI TU?

    KUNA TATIZO GANI KAMA SUALA LINAWAHUSU WENGI (WANANCHI WOTE) LISIWEKWE HADHARANI KABLA HATA KWA NJIA YA MAGAZETI ILI WATU WENGINE WACHANGIE?

    ''NO ONE IS PERFECT BUT ONLY GOD'' yaani ''Hakuna aliye mkamilifu isipokuwa Mungu'' ni utamaduni mbaya sana Mtu au watu wachache kujiona kuwa Mawazo yao ndio sahihi zaidi kuliko wengine, kumbe kwa bahati mbaya wapo wengine wasio dhaniwa wanaweza kuwa na mawazo bora zaidi kuliko hao.

    INAKUWA WANAOSAINI NDIO WENYE AKILI, NA WATU WENGINE HAWANA AKILI VILE!

    ReplyDelete
  14. du nanyie mafuta sio kwa ajili yenu
    nadhani hamjaelewa, mafuta , zahabu tanzanite sio kwa ajili yenu kwanza hamjawa na uwezo huo wa kuchimba, tumewaachia maji lakini hamjaweza itakuwa zaabu na mafuta? jiulizeni hapo.

    ReplyDelete
  15. ngeleje tena?

    ReplyDelete
  16. Ni yaleyale tu hakuna jipya zaidi ya kutibia rasilimali zetu kwa ubinafsi wa viongozi wetu. Na hii haitakwisha mpaka Wadanganyika wenyewe tuseme bas!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...