Na Mary Ayo,Arusha

IMEELEZWA kuwa pamoja na kuwa asali inaingizia taifa zaidi ya bilioni 27 kwa mwaka lakini bado zao hilo la asali linakabiliwa na changamoto mbalimbali hali ambayo inafanya zao hilo kushindwa kukua katika viwango ambavyo vinahitajika kwa ajili ya ubora wa masoko mbalimbali hapa nchini.

Hayo yalisemwa na Bi Gladness Mkamba ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya nyuki hapa nchini wakati akiongea na viongozi mbalimbali wa mikoa ya kanda ya kaskazini mapema leo.

Bi Mkamba alieleza wastani wa tani 9000 za asali kwa mwaka huvunwa ambapo jumla ya bilioni 27 hupatikana hivyo endapo zao hili la asali kama litapewa kipaumbele katika ubora ambao unatakiwa ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika zao hilo la asali basi zao hilo litakuwa na faida hapa nchini.

Alitaja changamoto ambazo zinaikabili zao hilo la asali hapa nchini kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kurinia asali hali ambayo inafanya zao hilo kuvunwa kienyeji tofauti na kanuni bora kwa zao hilo katika masoko ya kimataifa.

Changamoto nyingine ambayo ameitaja ni pamoja na baadhi ya Wananchi kukosa mbinu bora za ujasiamali katika zao hilo hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa zao hilo kushindwa kusonga mbele zaidi.

Bi Mkamba aliongeza kuwa changamoto nyingine ambayo nayo inaikabili zao hilo la asali hapa nchini ni pamoja na kutokuwepo kwa wawekezaji wa kutosha katika zao hilo hali ambayo nayo inasababisha zao hilo kuwa na wafugaji wachache sana.

“unaweza kuona zao hili linavyokabiliwa na changamoto mbalimbali lakini kama zao hili likipewa kipaumbele cha kutosha hapa nchini basi linaweza kuingizia taifa faida kubwa sana huku ajira nazo zikionekana
kuongezeka”alisema Bi Mkamba.

Pia alieleza kuwa nayo sera ya nyuki hapa nchini inatakiwa kuimarishwa zaidi ili kuweza kutoa kipaumbele kwa wadau mbalimbali kuweza kuwekeza zaidi katika zao hilo ambalo lina faida kubwa sana hapa nchini.

Alimalizia kwa kusema kuwa nao wawekezaji, wafanyabiashara, wakulima wanatak iwa kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu ambazo ni bora sana katika kuweka na kuuza asali ili kuweza kuimarisha zaidi zao hilo hapa
nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani kiswahili kinaniwia kigumu hapa. Nilidhani zao lazima litokane na kilimo. Kwa fikra zangu na uzoefu wa matumizi ya hii luhga nilidhani kuwa chochote kinachotokana na ufugaji uwe wa nyuki au ng'ombe hakiwezi kuitwa zao. Sasa sitashangaa tena kesho nikisikia zao la maziwa ya ng'ombe au zao la ngozi.

    ReplyDelete
  2. Anon. wa Fri Jan 27, 12:38:00 PM 2012

    Sioni tatizo lolote la lugha hapo. Zao ni sawa na kusema product kwa kiingereza. Nyuki wanazalisha asali au wakulima wa asali au wazalishaji wa bidhaa inayoitwa asali yote yanaeleweka bayana.
    Unaposoma habari jaribu kutafuta kitu wanachoita "context" hawa wenye lugha ya kimombo. Naona kuwa muandishi ametujuza sawia kuwa kuna changamoto katika uzalishaji wa bidhaa hii ambayo inaingizia taifa mabilioni ya shilingi na hilo ndilo muhimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...