Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao katika Hoteli ya Sheraton Waldhuus, Mjini Davos, Uswisi, Viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani unaofanyika mjini Davos na mazungumzo yao yaliangaza dhamira ya Vodafone ya kuongeza uwekezaji katika kusaidia ustawi wa jamii nchini na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao katika Hoteli ya Sheraton Waldhuus, Mjini Davos, Uswisi, Viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani unaofanyika mjini Davos na mazungumzo yao yaliangaza dhamira ya Vodafone ya kuongeza uwekezaji katika kusaidia ustawi wa jamii nchini na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania.

Vodafone ndio wanahisa wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania.Bw Colao ambae anahudhuria mkutano wa Uchumi wa Ulimwengu – WEF mjini Davos kama ilivyo kwa Rais Kikwete walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo hayo katika hoteli ya Sheraton Waldhuus.

Mazungumzo hayo yaligusia mahusiano ya Vodafone na seriklai ya Tanzania na watu wake hususan katika uwekezaji katika jamii kusaidia kukuza,kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii nchini ikiwa ni utekelezaji wa azma na malengo makuu ya Vodafone ya kuchangia kubadili maisha ya watanzania.

Vodafone kupitia Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kiasi kikubwa cha fedha kusaidia na kuunga mkono miradi mbalimbali ya kijamii nchini ikiwemo maeneo makuu matano ya Elimu, Afya, Kuinua vipato vya wanawake, Mazingira na Michezo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo

Katika mazungumzo hayo mafupi Bw. Colao alimuhakikishia Rais Kikwete kwamba Vodafone itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii Tanzania hususan katika maeneo ya afya na elimu ambayo yanauhusiano wa moja kwa moja na wa karibu katika kuiwezesha jamii kuondokana na changamoto ambazo zinaweza kuathiri maendeleo ya watu na hivyo kushindwa au kupunguza kasi ya kubadili maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbona hapana kumuona kamanda wangu Prof. Ibrahim Lipumba. Yeye si ndiye mwenyekiti wa balaza la uchumi la dunia au nimekosea wadau??

    ReplyDelete
  2. Duh, kama Lipumba ni mwenyekiti kweli basi jamaa nitamkubali babake!

    ReplyDelete
  3. Ndio umekosea. Sio yeye hebu angalau u google kabla hujaandika kitu hapa kwenye blog ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...