Mtoto Adam Robert akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza. |
Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi linalofahamika kwa jina la Under the Same Sun limegharamia ticket za ndege ya za Mtoto Adam Robert, Mama yake Mzazi Sabina Saliboko na Daktari wake Dr. Patrick Bulugu ili kutokea Geita Mkoani Mwanza kuja Jijini Dar es Salaam ili kwenda hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Kitengo cha Tiba ya Mifupa – MOI kwa matibabu zaidi.
Japokuwa majeraha ya Adam ambaye alidhuliwa na Baba yake kutoka na imani za kishirikina yameanza kupona kwa nje, bado anahitaji matibabu zaidi kwa mikono yake yote miwili. Adam hawezi kutumia mikono hiyo hivyo inamlazimu Mama yake Mzazi awe ana mlisha wakati wote.
Under The Same Sun waliombwa na Adam mwenyewe na pia Mama yake, Sabina Saliboko wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,Peter Ash alipomtembelea Adam katika Hospitali ya Wilaya ya Geita mwezi Novemba 2011, kumsaidia mtoto huyo kwa matibabu kabla ya kumpeleka shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daktari wake aliyempokea na anayemsindikiza hadi Muhimbili Dar es Salaam, Dr. Bulugu alisema kuwa mkono wa Adam wa kushoto uliposhambuliwa kwa panga, nerves ziliathirika na hivyo kuufanya mkono huo uwe kama umepooza.
Na hivyo wataalamu wa Muhimbili wataliangalia hilo na pia kumfundisha Adam jinsi ya kutumia vidole vyake viwili vilivyobakia katika mkono wake wa kulia ili avitumie kuandika na katika shughuli zingine zote zitakazomfanya aache kumtegemea Mama yake Mzazi kama vile kuoga, kuvaa na shughuli zingine.
Hivyo kutokana na hali hiyo Under The Same Sun wameamua kugharamia matibabu ya Adam katika kitengo cha Fast Track pale Muhimbili hadi hapo madaktari watakaporidhika na matibabu hayo. Na endapo Adam ataendelea na matibabu ya nje,Under The Same Sun watagharimia pia.
Under The Same Sun wamekuwa wakitoa misaada mbali mbali yenye gharama ya zaidi ya Shilingi Laki Nane ili kukidhi mahitaji ya Adam tangu alipolazwa kwenye hospitali ya Geita ikiwa ni pamoja na nguo, viatu, vyombo vya chakula na fedha zilizotolewa kwa Mama Adam tangu mtoto huyo aliposhambuliwa.
Fedha hizo pamoja na vitu vingine vingi ziliwawezesha kununua chakula kwa wakati wote walipokuwa Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Kwa upande wa ushirikiano na TAS, UTSS wanashughulikia matibabu ya Adam na TAS wanashughulikia elimu ya Adam atakapomaliza matibabu yake na ndugu yake, Salum.
Kwa upande wa kaka yake Adam, Salum Robert, Chama cha Albino Tanzania – TAS kimesema kuwa kimepata shule jijini Dar es Salaam. Kwa hiyo gharama za kumsafirisha Salum zitatolewa na TAS.
Tunatoa wito kwa mashirika mengine katika jamii kushirikiana katika masuala kama haya na mengine mengi katika kuwasaidia ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi. Na hasa katika kuondokana na imani na mila potofu zinazochangia ukatili wa kila aina dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini.
Baba yake mzazi yuko wapi? Jela au ameshahukumiwa kunyongwa? because he don't deserve to live or better yet cut his fingers off as well.
ReplyDeleteJamani huyo baba anyongwe hadi. Kufa au apigwe mawe hadi afe manake akinyongwa atakufa kwa starehe hafai kuitwa binadamu
ReplyDeleteKwakeli kesho kwa mwenyezi mungu tuna mengi ya kujibu.Na hasa wale wenyekuendekeza huu uchawi kwakweli ndio mnaosababisha haya yote kutokea na kuwatesa hawa albino.Kama tunaweza kuacha tamaa na kutokwenda huko kwa hao wenyekujifanya wachawi basi tusingekuwa na wachawi na kila mtu angetafuta kazi ya kufanya kwa jasho lake.Kwakweli ingekuwa vizuri huyu baba akatwe vidole kabla hajafikishwa polisi ili aone uchungu wake "shwain"
ReplyDeleteyani inasikitisha sna,nakubaliana na anony hapo juu, huyo baba yuko wapi??
ReplyDeletehuu ni ukatili usioweza kuvumilika,
ReplyDeleteni ushetani wa kupindukia.
please serikali ifuatilie akamatwe makali ya sheria yamshughulikie.
Huyo baba yake anastahili kukatwa mikono aone adha ya kuishi bila mikono. Binadamu gani huyu anayezidiwa hata na wanyama. Wanyama wakizaa mtoto kilema ambaye hawezi kukimbia wakati wa hatari wanakimbia wanamwacha hawamwui kama alivyofanya huyu kumkata mikono mwanae. Kwanza yupo wapi huyu baba yake. Is he still at large? Serikali na mahakama zisiwe na huruma hata kidogo na binadamu wanyama kiasi hiki.
ReplyDeleteKaka Michuzi asante na hongera kwa kuhabarisha jamii. Mimi nina wazo moja. Hivyo vijidirisha vidogo katika blogu yako (leave your comment) yaani "Publish your comment" na "Preview" havionekani kiasi msomaji anapata shida. Nashauri ubadilishe backgroung colour. Wengine macho yameanza kuchoka sababu ya masaa mengi.
ReplyDeletehuyo baba si binadamu bali ni shetani mbaya. adhabu ya shetani ni kuangamizwa tu. astaili kuishi. nina mpa pole sana huyo mtoto na mungu atamuangalia. wananchi tuwe macho watu kama huyo baba wanaiabisha nchi yetu tuipendayo.
ReplyDeletejamani mtoto nakupa pole upone.huyu baba aliyefanya ukatili wa namna hii ni kumkata mapumbu na vidole vyake.fisi mkubwa wewe.
ReplyDelete