· Kampuni pekee ya kizalendo iliyoweza kuwasaidia watanzania waliotapeliwa na makampuni ya Kijapani lakini kwa msaada wetu wamepata haki zao.
· Kwa waliotapeliwa hela zao na hawakupata gari zao kuanzia mwaka 2008 mnakaribishwa mkiwa na vielelezo vyote vilivyotumika wakati wa mauziano.
· Ofisi zetu kwa Dar Es Salaam tunapatikana mikocheni, Kwa Japan tunapatikana Osaka.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa simu zifuatazo;
Tanzania: +255 713 335 474 / +255 757 714 410
Japan: +818037627895.
Karibuni sana.
Kampuni inaitwa nini? Website? Kwa nini email addresses zenu zimekaakaa ki-a.k.a.? Mikocheni sehemu gani? Si rahisi mkaaminiwa namna hii.
ReplyDeleteUkishaibiwa na mwizi mmoja, na wa pili anatafuta kukuibia kidogo ulichobaki nacho.
ReplyDeleteHiyo namba ya simu ya Japan ni mobile phone. Hawa nao watakuwa ndo walewale.
ReplyDeleteTutegemee nini kumpa chui atuvushie mbuzi wetu mtoni? Tuwe macho watanzania, wajanja watatumalizia hawa.
ReplyDeleteMsaada pekee ni kutumia kampuni za wanasheria waliopo huko huko japan.
ReplyDeleteHawa madalali wanaotafuta pesa ya Ugali hawana msaada wowote zaidi ya kuwaongezea watu hasara ya pesa zao.
Duh! wabongo kwa kutengeneza dili hawajambo.
ReplyDeleteHapa tusubili tu kusikia watu wameachwa solemba.
Bongo tambarare!!
Mambo vp mzee Mcheri? Nitafutie prado ya 97.
ReplyDeleteKama upo Bongo naomba unipigie.
Wambura wa Tabata.
Big Up Mcheri. Naona Lucus mnajitahidi sana kuuza magari. Ila haya mambo ya sheria umeanza lini kaka?
ReplyDeleteMichuzi inabidi uwe makini kuzihakiki taarifa unazopewa kabla ya kutuletea.. maana hizi namba za Tanzania zinazoanzia 0713 na 0757 ni mobile phone, sasa usalama upo hapa kweli??
ReplyDeleteTusiwaongezee matatizo waliopatwa na matatizo.
Hii dili imekaa kimtego mtego. Tujiandae kusikia watu wanalizwa mara ya pili. Wabongo bwana.. we acha tu!
ReplyDeleteSafi sana Papaa Mcheri mokili nakuaminia baba kwa ubunifu wa kuzisaka ngawila. Piga kazi kijana tuendelee kula bata kwa kwenda mbelee..
ReplyDeleteHongera sana. Nawaaminia sana hawa lucus japan kwa marketing strategies zao. Inabidi mzee jumanne utufundishe na sisi wabongo wenzako haya ma-techniques ya huko Osaka ili tunyanyue maendeleo ya Bongo.
ReplyDeletewabongo wa huko osaka na nagoya hawaachi tu longolongo zao. Namba za simu walizoandika za japan na bongo zote ni mobile phones. Jungu linalopikwa hapa ngoja tutege masikio.
ReplyDeleteMichuzi, hutakiwi kuweka tangazo kama hili. Linaonekana ni sanaa tupu....
ReplyDeleteMdau DC.
Michuzi ongeza basi taarifa za hao jamaa. Maana wengi tumeshaumizwa kwa kununua magari kwenye mtandao wa Tradecarview.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu tuchangamkie hii dili kuokoa pesa zetu. Tuwasiliane na hawa jamaa kwenye hizo namba zao za simu.
ReplyDeleteHaujaacha tu yale mambo yako papaa mcheri japanese. Grow up man.
ReplyDeleteLengo langu ni kuwasaidia watanzania wenzangu waliopoteza pesa zao pale kwenye mtandao wa tradecarview.
ReplyDeleteHivyo msione kama nataka kuwatapeli pesa zenu.
Ubalozi wa Japan hapa Tanzania na ule wa Tanzania kule Japan wameshindwa kutatua haya matatizo nyinyi ndo mtayaweza kwa kutumia hizo ofisi zenu za kwenye mobile phone? Acheni utoto jamani kwenye mambo serious kama haya. Michuzi vp kaka unashusha hadhi ya blog yako kwa kupost upuuzi kama huu.
ReplyDeleteHebu toeni pumba zenu za kitapeli
ReplyDeleteGrow up mokili
ReplyDeleteHongera sana vijana wa nagoya kwa ubunifu wa sanaa za kipigaji.
ReplyDeleterecession inayoendelea huko japan, wabongo waliopo huko watatoana macho kwa michoro kama hii ya maji taka. ajira hakuna biashara zimedoda. mrudi tu huku nyumbani muanze upya.
ReplyDeleteHawa wahuni wenye hii post wananikumbusha.. wimbo wa profesa J.. "Aliyeuza cheni kapewa fedha bandia na aliyununua kapewa cheni feki. Hapo ni ngoma draw ndani ya bongo darisalamu"
ReplyDeleteWazee wa Azam Takeaway pale mtaa wa jumhuri wameadvance shughuli zao mpaka kwenye michuzi blogu!! Si mchezo, kwa mtego huu watawapiga vipofu wengi.
ReplyDeleteSegerea inawaita hawa wenye hizi mobile numbers. Siku hizi simu zote ziko registered sijui watakimbilia wapi hawa wasanii.
ReplyDelete............... Papaa Mcheri, tupe gharama za huduma hii !
ReplyDelete...... Ankal weka angalizo kuwa "Blog yako haitahusika kwa njia yeyote na sanaa hii, Buyer be......"
Hawa ni LUCUS T (LTD)wako opposite shoppers, nawapongeza kwa ubunifu wenu...ila mmeshafanya research ya kutosha ya mnachokiadvertise?
ReplyDeleteNawajua mko vizuri kweny biashara ya magari kwa kuwa nimeshafanya nanyi biashara...ila kwa hili sina hakika.
WAAGIZA MAGARI WAKOME SASA:
ReplyDeleteUnakuta mtu ana pesa ya kuunganisha, labda amewazima wenzie ktk dili, amedunduliza ameuza bidhaa za jumla,msimu wa mauzo wa mazao, amekopa Saccos, ana pesa ya ngama labda mafao baada ya kumaliza mkataba wa kazi,analipwa Mil. 10 yake,,,huyo anaingia ktk mtandao anatuma hela yote kuagiza gari!
Badala ya pesa hiyo ya bahati Mil.10 kufungua hata genge la bamia na dagaaa linalozungusha vizuri kwa Mil. 2.5 hivi na zingine Mil.7.5 akaweka akiba benki!
WATANZANIA KWA KUPENDA KIJIKO, MUONEKANO, UMAARUFU NA SIFA SISI HATUJAMBO!
Lakini biashara ya genge , ndiyo biashara salama kwa mstaafu, nayo ataliwa tu, tofauti atakuwa anatafunwa mtaji wake taratibu bila yeye kujijua. Taabu yetu, watanzania ni kusubiri hadi ustaafu ndiyo ufanye, kama mtu anaweza biashara ya genge au yoyote kwani usianze ukiwa kazini?? Matokeo ya kutoanza mapema, ndio mtu anapamia mambo oh ngoja niagize gari Japan, huko nako anakuta matapeli na kuliwa.
ReplyDeleteTuwatumie watanzania wenzetu kutushauri katika mambo mengi na usione hasara kumlipa mtu kidogo ukaookoa hasara kubwa mbeleni.
Janja wewe iko!
ReplyDeleteJe unaujua mwimbo wa watoto..
Buibui kasema kwa nzi karibu ndani
Nimepamba nyumba yangu.....
Ndio ndio wenye hamu ya kulizwa acha waendelee na mtoto akililia wembe mpe ili ukimkata ndipo atatia akili.
ReplyDeleteHawa wanaotangaza kusaidia waliotapeliwa magari Japan halafu anwani waliyotoa ni simu za kiganjani, ndiyo wale wale walioenda kwenye msiba wakaiba majamvi. Jamani muangakie msije mkalia mara ya pili.
ReplyDelete