Na Nafisa Madai - Maelezo,Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibari Mustafa Aboud Jumbe amesema shirika lake hivi sasa linakabiliwa na hujma kubwa ya wizi na uvamizi wa maeneo yaliyopo karibu na minara ya kuongozea meli.
Amesema wapo baadhi ya wananchi ambao huvamia maeneo hayo na kujenga nyumba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu ambapo alisema wapo baadhi ya vijana wanaojishughulisha na uuzaji wa vyuma chakavu hung’oa vyuma katika minara hiyo na kuuza.
Mkurugenzi Mkuu ameyasema hayo wakati alipofanya ziara na Bodi mpya ya shirika hilo kwenye vitengo mbali mbali vya shirika hilo na jinsi vinavyofanya kazi.
Ameongeza kuwa uvamizi huo unaweza ukasababisha ajali wakati wowote kwani meli kubwa za kigeni zinashindwa kuzitambua kwa urahisi alama za baharini pale wanapotaka kuingia katika milango ya Bandari Kuu ya Malindi Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu ameyasema hayo wakati alipofanya ziara na Bodi mpya ya shirika hilo kwenye vitengo mbali mbali vya shirika hilo na jinsi vinavyofanya kazi.
Akizungumzia Miradi ya Bandari Mkurugenzi Mkuuhu amesema hivi sasa shirika lake kupita serikali na wafadhili limo mbioni kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa bandari mpya ambayo itakuwa ya kisasa na kukidhi mahitaji ya watumiaji ya bandari hiyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi Salmin Senga, amesema wakati umefika kwa wafanyakazi wa shirika hilo kutumia zana za kisasa ili waweze kwenda sambasamba na ukuwaji wa sayansi na teknologia.
Alishauri uongozi wa shirika hilo kukaa pamoja ili kuweza kufanya tathmini ya vifaa vinavyohitajika na kupeleka mapendekezo yao serikali kuu ili kununua vifaa vipya vinavyokwenda na wakati hasa katika sehemu ya kupindia plate za kutengenezea meli ambapo utaalam unaotumika umepitwa na wakati.
Nao wafanyakazi wa kitengo hicho kwa niaba ya fundi mkuu Suleiman Nassor waliomba wapatiwe mashine za kisasa ili waweze kufanya kazi zao kwa wepesi zaidi.
Ziara ya viongozi hao ilianzia eneo la kuhifandia mafuta Malindi,kituo cha Ujenzi ya Miundombinu ya Bandari,Chelezo cha Malindi,kituo cha kutengenezea gesi ya kuongozea minara na kutembelea minara ya Maruhubi, Betras na Mwangapwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...