Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akizungumza na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali,wizara na wadau kutoka nchi wahisani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao unaojadili mabadiliko ya Tabia nchi na mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
Mshauri wa masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID) nchini Tanzania Bi. Magdalena Banasiak (kushoto) akizungumzia athari za mabadiliko ya Tabia nchi duniani na mchango wa wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa athari za mabadiliko ya tabia nchi zilizoanza kujitokeza zinadhibitiwa.
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira,Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiwasilisha mada kuhusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na ripoti ya tafiti ya athari za kimazingira iliyofanyika katika baadhi ya maeneo yakiwemo Zanzbar, Mbeya, Tanga, Manyara, Shinyanga na Mwanza leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Mazingira kutoka ndani na nje nchi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano wa wadau wa mazingira kuhusu mkakati wa kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.
Wadau wa Mazingira kutoka, Taasisi mbalimbali,wizara na wadau wa mazingira kutoka nchi wahisani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano unaojadili Mkakati wa Kitaifa kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Kuanzishwa kwa mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi kutaiwezesha na kuiongezea uwezo nchi ya Tanzania kushirikiana na mataifa mbalimbali katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchini yanayoendelea kuikumba dunia.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi wakati akifungua mkutano wa wadau wa mazingira kujadili mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi.

Amesema hivi sasa mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari kubwa duniani ikiwemo ongezeko la gesi joto angani jambo ambalo linahitaji juhudi za mtu mmoja mmoja, vikundi, Taasisi na Jumuiya za kimataifa kushirikiana kwa pamoja kuinusuru dunia kutokana na athari za mabadiliko hayo.

“ Tanzania na watanzania wote kwa ujumla watapata fursa ya kushiriki katika fursa za miradi ya kupunguza gesi joto kupitia sekta binasfi hasa fursa za miradi ya kupunguza gesi joto inayoanzishwa nchini na kuwawezesha watanzania kupata fedha huku wakiendelea kufanya shughuli zao za kila siku”

Amefafanua kuwa mkakati huo wa kitaifa wa mabadiliko ya Tabia nchi utaisaidia nchi ya Tanzania kushiriki katika masuala mbalimbali ya kimataifa na kuiwezesha kuwa na msimamo kama nchi kupinga vitendo vyote vinavyofanywa na mataifa mbalimbali yaliyoendelea kiviwanda ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la gesi joto duniani.

Pia amefafanua kuwa licha ya mkakakati huo kuanzishwa kwa mara ya kwanza kwanza nchini utaiwezesha Tanzania kuwa ushirikiano na nchi nyingine za Afrika, jumuiya mbalimbali za kimatifa ndani na nje ya bara la Afrika na kuongeza kuwa ukamilishwaji wa mkakati huo utaiwezesha nchi kupanga na kuamua masuala mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya Tabia nchi.

Aidha amefafanua kuwa sanjari na kuwepo mkakati huo ambao ni mkubwa masuala ya mazingira yataendelea kuongozwa na mkakati wa kitaifa wa mwaka 2006 na ule wa 2007 unaotoa mwongozo kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira yakiwemo uzuiaji wa uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito na uharibifu wa misitu na mazingira.

Kwa upande wake mshiriki wa mkutano huo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Prof. Richard Kangalawe amefafanua kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanendelea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wan chi yetu na hata kutishia maisha ya kila siku.

Amezitaja baadhi ya changamoto ambazo Tanzania kwa sasa inakabiliana nazo kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi kuwa ni pamoja na ukame katika baadhi ya maeneo, mafuriko yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini kutokana na mvua zinazonyesha kwa muda mfupi na ongezeko la magonjwa mbalimbali.

“Kama tunavyoona kuna dalili mbalimbali ambazo zinaonyesha kuwa hali ya mabadiliko ya tabia nchi imekuwa kubwa sana tofauti na miaka 30 iliyopita na inaliathiri taifa hasa baadhi ya matukio mbalimbali yaliyotokea hivi karibuni ikiwemo mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha madhara makubwa katika jiji la Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wao hao hao ndiyo wanaharibu mazingira harafu wanakuja vacation, ati ooh mazingira tabia. Ujibga huu au ujanja

    ReplyDelete
  2. Hii mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi inayokuja kufanyika dunia ya tatu ni kupoteza fedha na muda kwani viwanda vilivyochangia kuharibika kwa tabia nchi vipo huko dunia ya kwanza (nchi zilizoendelea kiviwanda) ambako hawataki kutekeleza makubaliano ya Kyoto. Wamekutana Afrika Kusini mwaka 2011 bila mafanikio sasa wameanza kutembelea nchi moja moja kwenda wakizishawishi zisaidie kudhibiti mabadiliko hayo. Tanzania viwanda vipo vingapi vya kuharibu tabia nchi. Nchi kama Canada ilijitoa kwenye makubaliano ya Afrika Kusini kwa sababu waliona uchumi wao utadorora. Pamoja na kujitoa kwa Canada nchi za Ulaya na Marekani wamekuwa bubu. Ingekuwa nchi ya dunia ya tatu imejitoa, ingefutiwa misaada na vikwazo vya kiuchumi. Hiki wanachofanya ni kuendeleza ukoloni mamboleo. Hawa watu wa Ulaya wanataka nchi za dunia ya tatu zibaki omba omba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...