Wafanyakazi wa kampuni ya Facebook wakimhoji Mama Adriana Huffington, mwanalibeneke mkongwe anayeendesha blogu kubwa kuliko zote duniani ijulikanayo kama http://www.huffingtonpost.com/, kwenye mkutano wa dunia wa uchumi mjini Davos, Uswisi
ankal kila konozzz na Mama Ariana Huffington, mwanalibeneke mkongwe anayeendesha blogu kubwa kuliko zote duniani ijulikanayo kama http://www.huffingtonpost.com/, kwenye mkutano wa dunia wa uchumi mjini Davos, Uswisi. kumbe libeneke la Globu ya Jamii analijua vizuri tu, na maongezi yamefanyika kuanzisha ushirikiani wa kikazi. Libeneke Oye!
BOFYA HAPA: KUSOMA HABARI ZA HUYU MAMA
BOFYA HAPA: KUSOMA HABARI ZA HUYU MAMA
Wafanykazi wa kampuni ya libeneke ya Facebook wakifuatilia na kutangaza laivu kongamano la uchumi la dunia mjini Davos.
Ankali hapo hapo kwa mamaa Adriana Huffington ndio pa kufunga kamba yetu na sisi tupae vilevile,,,Hakikisha unachukua contact zake kabisaaa,
ReplyDeleteLibeneke Oyeeeeeee!
IS LIBENEKE A NEW WORD FOR ONLINE MEDIA? OR BLOGGING?
ReplyDeleteAriana na Ankal! Wow! Wanalibeneke wa kimataifa.
ReplyDeletemichuzi huffington post sio blog hiyo ni website iliyojaa habari nyingi za kiuchunguzi na za maana.hapa usa wiki majuzi kuna judge aliamua kuwa blog sio vyombo vya habari na wana blog hawaruhusiwi kupata taarifa kama walivyo wandishi wa habari.
ReplyDeleteSamahani napenda kufafanua vizuri jinsi ya Anonymous wa Thu Jan 26, 08:25:00 PM 2012, alivyoandika. Jaji mmoja wa Marekani katika kesi za wana blogs. Alisema ya kwamba; waandishi wa blog hawawezi kupewa haki ya kufichwa kisheria kama ilivyo waandishi wa habari wengine tuliyowazoea, kwa mfano(radio,tv, magazeti na nk. lakIni siyo blogs) Tuseme pale wanapodokezwa siri na mtu fulani lakini hawasemi nani kawaambia na habari inakuwa ya kuaminika kwa sababu ya wanajulikana kama waandishi na sheria ya habari ina walinda. Siyo kama ulivyosema, "blog sio vyombo vya habari na wana blog hawaruhusiwi kupata taarifa kama walivyo wandishi wa habari". Na mjadala huu ingawa huyu jaji amemua lakini bado unaendelea, labda utapelekwa mahakama ya rufaa, au mahakama kuu(Supreme Court) Hapo ndipo tutajua wanablogs wana haki gani. Kwa sasa bado sheria haileweki ingawa huyu jaji anaona kama anavyoona yeye.
ReplyDeleteBlog kubwa kuliko zote Duniani ni; Hii yetu ya Libeneke letu (BLOG YA JAMII) hakuna nyingine.
ReplyDeleteLibeneke oyeeeeeee...!!!!!
Ankali Assalamu Alaykum zako kwa kweli!,,,yaani hilo koti ulilovaa unang'ara sana huku ukiwa na huyo mamaa wa Libeneke mwenzio Adriana Huffington,,,inabidi tukupe hadhi ya UBUNGE au UBALOZI!!!
ReplyDeleteAnkal hizo faranga zote unazopata kwenye misafara hii hebu tenga kidogo siku moja utuite wadau wako tuje kunywa japo soda tu, tujuane ila tusitajane majina atakae mtambua mwenzake siri yake - think of that we like and love you man.
ReplyDeleteLibeneke oyeeeeeeeeeeeeeee
Naungana na Mdau wa 8 hapo juu Anonymous Fri Jan 27,09:22:00 AM 2012
ReplyDeleteAnkal hizo faragha zote unazopata kwenye misafara hii hebu tenga kidogo siku moja utuite wadau wako tuje kunywa japo soda tu,,,,,
NI KWELI ''MKATE HUO ULIOUSHIKILIA ANKAL'' NI WA KUTUMEGEA NA SISI WADAU WAKO HATA ANGALAU UPUKUPUKU WA CHENGA ZAKE MAANA MKATE HAUKOSI ANGALAU CHENGA!