Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Ruvuma idara ya ardhi na miundombinu,Bw. Severin Tossi akiongea wakati wa sherehe ya kuwaaga watumishi ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria hivi karibuni.
Katibu tawala msaidizi mipango mkoani Ruvuma,Bi. Vestina Nguruse akitoa nasaha zake katika sherehe za kuwaaga watumishi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa huo.kushoto ni katibu wa Mkuu wa mkoa huo,Bw. Joel Mbewa na kulia ni mke wa katibu tawala wa mkoa Mama Tarimo.
Afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma,Bi. Paulina Mkonongo (kushoto) akimpa zawadi aliyekuwa katibu muhutasi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa huo,Bi. Hermana Mapunda,kwenye sherehe ya kuwaaga waliokuwa watumishi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa huo.
Mama Vestina Nguruse akiwaongoza akina mama wenzake kwenda kutoa zawadi kwa waliokuwa wafanyakazi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa ruvuma ambao wamestaafu utumishi wa ummma hivi karibuni.
Baadhi ya akina mama kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma wakiwa na zawadi zao kwa ajili ya kuwazawadia wanawake wenzao (hawapo pichani) waliokuwa watumishi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma ambao wamestaafu katika utumishi wa umma.
wafanyakazi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma wakicheza muziki katika sherehe za kuwaaga watumishi wenzao watatu waliostaafu hivi karibuni.
Katibu tawala msaidizi idara ya ardhi na miwa mkoa wa Ruvuma,Sevelin Tossi katikati akiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa watumishi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa huo bi Dorolosa Komba wa kwanza kushoto,Bi Moshi Mwakilisha wa pili kushoto na Bi Hermana Komba wa pili kutoka kulia. PICHA NA MUHIDIN AMRI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ila msije kumtupa Jongoo na mti wake, baada ya kuwaaga kwa kustaafu muwe na mwenendo wa kuwatazama tazama makwao Mtaani ambako ni kugumu saaana,,,kama mjuavyo hio ni njia yenu nyote na ninyi mtafika muda wa kustaafu!

    ReplyDelete
  2. Ukisikia fainali uzeeni ndiyo hiyoo, hapo mziki ndio kwanza unaanza we cheki kina mama walivokuwa na sura za wasiwasi maana kuwa nje ya kazi na kama hujajiandaa kuzoea maisha mapya baada ya kustaafu si kitu rahisi jamani.

    ReplyDelete
  3. Hao wastaafu wana migahawa au?

    ReplyDelete
  4. Nadhani hao akina mama waliostaafu wanaenda kujiajiri kuwa akina mama lishe maana hizo zawadi za masufuria zitatumika kwa shughuli hiyo.Hongereni akina mama mliotoa zawadi kwa kuwapatia mtaji wenzenu waliostaafu ili wasipate tabu ya kujua wapi pa kuanzia maisha mapya.

    ReplyDelete
  5. hivi umri wa kustaafu govt employeees ni miaka mingapi? 55, 60 or 65??

    ReplyDelete
  6. Ukistaafu inakuwa imetoka. Ukifanya kazi fanya kwa kujiaga kila siku, jifanyie sherehe n.k. Siku hizi waajiri hawana habari na wastaafu wao. Si waajiri tu, hata watoto ulozaa mwenyewe siku hizi ukushachoka hageuki nyuma kukujali, ndio kwanza anaomba ufe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...