Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mawaziri na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya kufungua mkutano wa tatu wa mazungumzo ya mwaka juu ya sera ya Taifa ili kuendelea kuimarisha juhudi za kupunguza umaskini na kukuza uchumi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Ubungo plaza jijini Dar es Salaam unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa tatu wa mazungumzo ya mwaka juu ya sera ya Taifa ili kuendelea kuimarisha juhudi za kupunguza umaskini na kukuza uchumi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Ubungo plaza jijini Dar es Salaam unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo mara baada ya kumaliza kufungua mkutano wa tatu wa mazungumzo ya mwaka kuhusu sera ya Taifa ili kuendelea kuimarisha juhudi za kupunguza umaskini na kukuza uchumi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Ubungo plaza jijini Dar es Salaam unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu Waziri wa Fedha Gregory Theu (kulia) pamoja na mabalozi wakimsikiliza waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa tatu wa mazungumzo ya mwaka kuhusu sera ya Taifa. Mkutano huo wa siku mbili unafanyanyika katika Hoteli ya Ubungo plaza jijini Dar es Salaam unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Katibu Mkuu ofisi ya waziri Mkuu Peniel Lyimo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizaya ya Fedha Dk. Servacius Likwelile (kulia) wakimsikiliza waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa tatu wa mazungumzo ya mwaka kuhusu sera ya Taifa. Mkutano huo wa siku mbili unafanyanyika katika Hoteli ya Ubungo plaza jijini Dar es Salaam unahudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Nategenmea katika mjadala huo watasema serikali inafuata nini MKUKUTA au Mpango wa maendeleo wa miaka 5 ? Maana Rais naye kajichanganya kwa kusaini mipango yote na kila mtendaji anajigamba kuwa anafuata maelekezo toka juu. Je bajeti ya mwaka ujao na maandiko mbalimbali yanayoenda kuomba fedha yataje mpango upi?
ReplyDelete