Aliyekuwa Refa wa Kimataifa hapa nchini, Gratian Hemans Matovu (pichani), amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.

Kwa kujibu wa taarifa zilizoifikia Globu ya Jamii, kutoka kwa mtoto wake Bw. Stephen Matovu, Mzee Matovu amefariki leo majira ya saa 6 mchana huko nyumbani kwa kwake Mbezi Beach (Makonde) na taratibu za mazishi zinaendelea hapo hapo nyumbani kwake.

Mzee Gratian Matovu alianza kuwa refarii wa kimataifa tokea miaka ya 1964 na aliendelea na shughuli hiyo hadi miaka ya 1970 na hadi Mwaka 2006 alikuwa bado katika Kamati ya Marefarii Tanzania.

HISTORIA FUPI

Mzee Matovu alipata Diploma ya Urefarii kunako miaka ya 1956 na akaja kuwa refarii Daraja la Kwanza mnamo Mwaka 1961. Miaka Mitatu baadae alipata Beji ya FIFA.


Mzee Matovu alipata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Chama cha Marefarii Tanzania.

Kwa Taaria zaidi za wasiliana na STEPHEN MATOVU 0713576666

Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Babu....Mshukuruni Mungu kwa kila jambo!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana Stephen, George na familia yote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...