KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa akizungumza katika maulidi ya harusi ya mkazi mmoja wa mtaa wa Togo, Kinondoni, Dar es Salaam. Maulidi hiyo ilikuwa ikifanyika karibu na eneo ambalo kiongozi huyo alifika kwa ajili ya kufungua Ofisi za Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), ambapo mbali ya kupata fursa ya kutoa salaam za heri kwa maharusi, yeye pamoja na viongozi wa chama hicho alioandamana nao katika msafara wake walitoa sadaka .
Home
Unlabelled
dkt slaa ahudhuria maulid ya harusi mtaa wa togo jijini dar es salaam
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wanaekti kama si wadini vile ngoja watake wanachokitafuta sera yao itakuwa UKRISTO KWANZA..!mi nasema chadema ni chama cha kikristo bisheni...!!!! sijui nani kawaalika...ahah..kumbe waliomba wenyewe...natonywa na mdau hapa..! wanajipendekeza!!muislam mwenye kujielewa hadanganyiki..na hao chadema.!
ReplyDeleteNashangaa hii cancer ya udini imetoka wapi? Nina umri zaid ya miaka 50 sasa, nashangaa udini umeota mizizi, kila kitu kinachofanyika tunakiona katika picha ya udini. Tulipokuwa watoto mambo hayakuwa hivyo, tuliishi sote pamoja, familia moja kuna wakristo, waislamu n.k. Lakini siku hizi!!
ReplyDeleteMaoni kama haya yashajeruhi hisia zangu
ReplyDeleteMdau wa kwanza kuchangia ndio mdini. Mbona tupo waislamu kibao huku tunaikubali chadema? Au wewe umeridhika saaana na hali ya nchi ya sasa? Labda kuna kitu unapata toka kwa mafisadi. Au wewe haupo Bongo nini? Kama ni mwana CUF huko nako unaona nini uhalisia wake! Kusema watu kama Prof. Safari, Zitto Kabwe n.k hawajielewi ni kushindwa kupambambanua siasa ni ipi na dini ni ipi. Anyway, tunatofautiana katika uelewa.
ReplyDeleteMaoni ya mchangiaji wa kwanza kimeo. Nahisi hata 'relijeni' yenyewe haielewi. Chuuuuuuuuki tuuuuuuu!!!!!
ReplyDeleteAnonymous wa Sun Feb 26, 09:54:00 AM. Eti mtu kamtonya kwamba waliomba wenyewe CDM. Jamani UONGO ni dhambi!
ReplyDeleteMdau wa kwanza nadhani sio muislamu kwani humu kwenye blog kuna mengi jamani. Au ametoa hayo maneno makusudi tu, lakini hamaanishi. Kwani uislam ni ustaarabu
ReplyDeleteMajid, H. wa Uturuki
na CUF ni cha watu gani??
ReplyDeleteHata Nyerere alishambuliwa kwa udini, leo liko wapi...kazi ilipigwa na wala hakukuwa na udini. Hata huo udini anaosakamwa nao JK wala siuoni. Just be fair and get your blessings.
ReplyDeleteuungwana ni kuheshimu jirani zako pamoja na mila na taratibu zao. cdm si chama chenye udini na matukio kama haya yanadhihirisha ukweli huo. watanzania tunataka kuishi pamoja kwa amani na upendo bila kubaguana.
ReplyDeleteAcheni, Waislamu ndio ambao hawana udini maana wao ndio waliowakaribisha wakristo na wakawavumilia na kuwakaribisha kwao hapa pwani na visiwani. Nyie mkikaribishwa kichwa mnaingia wazimawazima katika hema na kuchukua nafasi yote kishwa kuwapiga teke wenyeji na ndicho kilichotokea na ndicho kitakachotokea. Hatudanganyiki tena. Waacheni kina Zitto na Safari wana maslahi yao lakini sisi wengine tunasema basi ena........Kama wewe muislamu umeamua kuwa chadema basi uwe na usilazimishe kila mwislamu awe chadema. CHADEMA ni chama cha KIKRISRO period,
ReplyDeleteHakuna chama cha kikristo wala kiislamu, ni hisia za mtu binafsi ndio zina count. Acheni jazba kwa kila jambo wanangu.
ReplyDeleteTatizo letu sisi vijana wa siku hizi ni kuropoka bila kupima uzito na ukweli wa kauli zetu. Uvivu wa fikra ni tatizo la sasa na litakuwa na madhara siku za usoni kama hatuta badili mienendo yetu.
ReplyDeleteMtoa hoja ya udini ingekuwa vyema apambanue au atueleze vyama vya kidini ni vipi hapa nchini.... na pia ni kwanini anafikiri ni vya kidini. Halafu atueleze ni vipi visivyo vya kidini na atueleze kwa nini anafikiri hivyo. Hapo tutaweza kumuheshimu na kuchangia hoja yake. Lakini hisia tu aziwezi kutufanya tumuamini."Feelings are not supposed to be logical. Dangerous is the man who has rationalized his emotions."- (David Borenstein)
Napenda kutoa hoja kuwa watu wengi waliofilisika kimawazo au kiuchumi upenda kukimbilia mambo ya kikabila,ukanda na udini wakidhani ukombozi wao utapatikana na matabaka hayo. Napenda kupongeza kitendo hiki cha kiungwana alichofanya Dk. Slaa kwa sababu kilitokea katika hali ya kutopanga/ accidentally. Napenda pia kutumia fursa hii kumpongeza shekhe mkuu wa Mkoa wa Dar-es- Salaam na viongozi wenzake walio nyuma yake kwa kuwa na uelewa mkubwa wa dini ya kiislamu na mahubiri yake mazuri kuhusu kushusu amani kiasi cha kunifanya niipende dini hii na kuanza kujifunza undani wake.
We are so often caught up in our destination that we forget to appreciate the journey, especially the goodness of the people we meet on the way. Appreciation is a wonderful feeling, don't overlook it.
Ndungu mtoa hoja za udini hapo juu ....napenda kukumbusha kuwa............." Great spirits have always encountered violent opposition from mediocre minds"-(Albert Einstein).
Hakuna kingine hizi ni harakati kuelekea Uchaguzi 2015!
ReplyDeleteAssalama Leko kwa Mpigo Bwa Sheee ,Meku?
TUNAOMBA KURA ZETU WOOOTE KTK MAULIDI YA HARUSI, TAFADHALI!
Jamano SiLAHA mbona koti linamvaa??? maana tumbo lote limeisha , halafu festi ledi mtarajiwa ameshajifungua??
ReplyDeleteAnkal,kuna mdau humu aliwahi kutoa maoni kwamba sisi ni wadini.Nadhani kuna ukweli kwa sababu mtu mmoja akiongelea suala la udini basi maoni kibao yanaanza kuporomoka.Wakati kuna mada nzuri humu kwenye blog za kuelimisha hakuna anayechangia.Ebu acheni udini wenu huko
ReplyDeleteDavid V
Hahahahahahahaha!!!! Nyie hamjaenda mkutano wa kamati Jumapili nini????
ReplyDeletejamani nyie acheni akonde alishasahau ulezi sasa kasheshe za mtoto mchezo lazima ukonde.
ReplyDeleteUkiona Magwanda ya Kaki kwenye Mkusanyiko ni dalili kuwa MGAMBO WA MANISPAA WAMEVAMIA ktk Maulidi ili kuona kama Waandaaji wa Shughuli waliomba Kibali cha Ofisi ya Serikali za Mitaa au la?
ReplyDelete