Habari yako mzee.

Naomba uniwekee taarifa hii kwenye Blogu ya yetu ya Jamii.

usiku wa Jumamosi ya tarehe 5 Februari, 2012 Maeneo ya Sinza Makaburini Dar es salaam, wezi wasiojulikana waliiba gari yangu hii (pichani) aina ya TOYOTA COROLLA FIELDER yenye namba za usajiri T541BTE, rangi ya "Silver". 

Tafadhali kwa mtu yeyote atakayeiona gari hii awasiliane nami kwa namba 0715-561048, 0713-171775, 0762-561048, au kituo chochote cha polisi cha karibu. 

Zawadi itatolewa kwa atakayefanikisha taarifa hizi.

Mdau wako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Aise pole sana.Inauma kweli +/-10M.Sasa mimi nadhani ongeza maelezo zaidi kidogo kiongozi(filters) ni manual au automatic,ina diff?.Rangi na vibao haviwezi kusaidia sana hawa jamaa ni washenzi wanabadilisha rangi na vibao hivyo,chasis namba nasikia zinabadilishwa.Hapo Sinza kuna wezi wa magari sana hey?

    David V

    ReplyDelete
  2. duh wizi wa magari umeshaanza balaa pole dau , dah inabidi na mimi nipige picha gari yangu kabisa maana hata sina picha ya gari , ikiibiwa itakuwa balaa zaidi...

    ReplyDelete
  3. Jamani this is too much now, pale sinza makaburi(mwika social hall) wizi wamagari umezidi haswa kwa wale wanao hudhuria harusi, sendoff nk. jihadhari na magari yenu jamani kuna wizi mkubwa na wale wanaokwenda kunywa au kula pembeni yake kazi munayo. Kwanza hakuna parking yakutosha halafu nashangaa kuna walinzi lakini watu wanaibiwa magari yao. Polisi fanyeni uchungui na hao walinzi wa hapo nadhani watakuwa wako wote na hao wezi tuu!!

    ReplyDelete
  4. gari imeibwa na si kuibiwa mdau, hata hivyo ujumbe umefika ingawa hatukitendei haki kiswahili ambayo ndo lugha yetu rasmi ya taifa...pole sana mdau

    ReplyDelete
  5. Wezi wa Magari ni moja ya Wahalifu wenye mtandao mpana sana Duniani kama walivyo wafanya biashara ya Madawa.

    Ni jambo la kawaida kukuta gari inaibiwa Tanzania inasafirishwa na kuuzwa Kenya, au Uganda bila wasi wasi.

    Tatizo wezi wa magari wapo vizuri, hata ki fedha,ki uenezi ni Wajanja wajanja, wanaweza pita sehemu nyingi za vizuizi bila tabu na pia muonekano wao ni wa Ki u Bosi hivyo sio rahisi kuwatambua!

    ReplyDelete
  6. Imeibiwa nini tairi au side mirror? Au imeibwa? Kiswahili gongano hapo kwenye kichwa cha habari ankal!

    ReplyDelete
  7. Toa taarifa polisi. Kutoa taarifa kwa Michuzi haisaidii.

    ReplyDelete
  8. Mbona siku kibao zimepita tayari ndio tangazo. Jamaa wako fit sana. kama ilikuwa ni usiku inaweza kukupita asubuhi yake na ukawa huijui tena, wanabadilisha namba na kukwangua kila alama unayoweza kusema ndio hii. Jitahidi kuitafuta kwa msaada wa Polisi utaipata tu maana hata pale mlipani city zimeibiwa nyingi na nyingi kati ya hizo zimepatikana. Pole sana mdau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...