Baadhi ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimuhudumia mmoja wa wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika wadi namba sita kwenye Jengo la Mwaisela kwenye hospitali hiyo.Madaktari hao ambao walikuwa kwenye mgomo kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo,leo wameanza tena kazi mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda jana na kuzungumza nae na kuafikiana kutekelezewa yale waliyoyahitaji.
Madaktari wa Muhimbili wakimfanyia matibabu mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo leo.
Baadhi ya Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa wamekaa nje ya eneo ya huduma ya matibabu ya haraka wakisubiria wagonjwa wanaoletwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Wauguzi wa Muhimbili wakimtoa mgonjwa MOI na kupempeleka kwenye wadi iliopo kwenye jengo la Mwaisela.
Mgonjwa alipokelewa na wauguzi wa kitengo cha Huduma ya Haraka kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Pamoja na Kwamba Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamaliza Mgomo wao na kuanza kazi rasmi leo,wagonjwa wengi sasa hivi hawapo hospitalini hapo kama inayoonekana pichani.
Sehemu ya Kinamama wenye watoto wakiwa kwenye maeneo ya Hospitali hiyo na wamekuwa ni wenye furaha kwa kuona huduma zimerudi kama ilivyokuwa hapo awali hospitalini hapo.














AIBU YETU AIBU YAO?
ReplyDeletemichuzi si kila mwenye koti jeupe ni daktari tayari hata kama wana muangalia mgonjwa wengine ni wanafunzi bado wako ktk somo na dk mkuu wao
ReplyDeleteAhsanteni SANA!
ReplyDeleteTujaribu kubadilisha mwenendo na kuthamini kazi za watu kulingana na mazingira na Ugumu wa kazi.
Isiwe Mabilioni ya Shilingi fedha za Umma yanaibiwa na Wezi hukooo Halmashauri za Wilaya, huku tukiwaacha Madakitari katika kazi yao hatarishi ya maambukizi ya maradhi na masaa mengi ya kazi!
Ni process fupi na rahisi sana,,,ni kiasi cha kuchomoa mirija inayotiririsha Mabilioni ya Fedha za Umma kuelekea mikononi mwa WEZI na kuirudisha mipira kwenye mishipa ya wastahiki na wastahili kama MADAKITARI na wengineo!
ReplyDeleteMa Dr. mmefanikiwa BUT mmeuwa sana wasio na hatia nawahakikishieni mna DHAMBI iliyo kubwa sana kwa Mola na fedha mlizoongezewa ni haki yenu bali zitabaki daima kuwa fedha za DAMU!
ReplyDeleteKwa Serikali mmesababisha maafa ambayo hayakustaili hata kidogo! Ni ubabe tu na ulevi wa madaraka ndio uliowapa KIBURI hadi mkasababisha MAAFA haya!
Hakya mama, mnastahili kupelekwa the Hugue mkajibu tuhuma! Ebo!
Inauma sana sana
Kweli we Mkibosh
ReplyDeleteNimesikitishwa sana na moja ya madai ya madaktari ,kweli wasomi wanalilia mkopo wa magari?Kwa nini wasimwambie waziri tunaomba mikopo au kujengewa nyumba .Akili ni MALI
ReplyDeletemdau Muhimbili
sio kwamba waliosoma wote wana akili, kuna akili ya kusoma na common sense ambao hawa madaktari hawana kabisaaaaaa. Ule msemo unaosema Akili nyingi huondoa maarifa ni kweli. Watoto wetu wa siku hizi wanataka utajiri wa haraka haraka hata kama ni kwa kuuwa, Badala ya kuanza chini mshahara wao wanataka waanze juu. Akishasoma, basi anataka anunue gari, nyumba shamba na aoe mwaka huo huo. Hii kweli ni akili. Waacheni na wao si siku moja watashika nyadhifa halafu watoto wao watawafanyia fujo hizi.
ReplyDeleteSihukumu...bali mlichikifanya madaktari kitabakia kuwa dhambi yenu...Mwaweza kudhani mmefanikiwa, lakini hakika pesa haitakuja kutosha siku moja...je mtarudi kuua wengine mtakapohisi pesa haitoshi!? Mmeua wengi wasio na hatia! inasikitisha! Kama kugoma ni haki...kuuwa nayo ni haki!!!??? DAMU MLIZOMWAGA ZITAENDELEA KUWALILIA NINYI NA VIZAZI VYENU! Mwenyezi MUNGU awasaidie kila mtakapokumbuka Muungame!
ReplyDeleteEddy
Vancouver
KWA NDUGU WOTE WALIOTOA HOJA ZAO HAPA, HOJA ZENU NI ZA KWELI NA NAZIHESHIMU KWANI KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE KWENYE KILA JAMBO, NDIO MAANA WAHENGA WAKASEMA KUWA AKILI NI NYWELE- KILA MTU NA ZAKE, LAKINI NAONA HOJA NYINGI ZIMEJAA JAZBA NI SAWA KABISA MAANA HII SERIKALI NDIO INAPELEKEA WATU KUONGEA KWA JAZBA KUTOKANA NA DHARAU ZAO, WAMEONA MAISHA YA WATU YAMEPOTE NA KELELE ZA WANANCHI ZIMEZIDI NDIO WANASTUKA, MIMI KWA MTIZAMO WANGU SERIKALI NDIO IMESABABISHA HAYA YOTE, UKIANGALIA WATU WENYE MATUMBO MAKUBWA WANASINZIA BUNGENI ZAWADI YAO NI KUONGEZWA POSHO WAKATI MADKTARI WANAFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU ZAWADI YAO NI VIRUNGU VYA FFU, NA KWAKO MTANI WANGU MKIBOSHO HAWA MADAKTARI HAWANA DAMU YA MTU YEYOTE KWANI HAWAKUKURUPUKA TU KUGOMA, WAMELIA SIKU NYINGI LAKINI WALIDHARAULIWA, WAO PIA WANA MAHITAJI YA KILA SIKU NA WANA FAMILIA ZA KUZIHUDUMIA NA MAHITAJI MENGINE, WENYEWE WANAPELEKANA INDIA KWA MATIBABU TENA YANAYOWEZA KUTIBIKA HAPA NCHINI WAKATI DAKTARI AKIUGUA SERIKALI HAIMTAMBUI JE NI SAWA? HIZO PESA ZINAZOENDA INDIA KWANINI ZISITUMIKE KUKIDHI MADAI YA MADKTARI? HUU UNAKUA UITO WA AINA GANI? HAKUNA KAZI YA UITO HATA PADRI NA SHEIKH WANAKULA SADAKA, KWA HIYO DAMU IKO MIKONI MWA SERIKALI. NA KUHUSU MAMBO YA KUJENGA AU KUNUNUA GARI HUO NI UTASHI WA MTU MWENYEWE MRADI HAKI YAKE APEWE ATAKAVYO TUMIA ATAJUA MWENYWE.
ReplyDeleteBravo bravo madaktari mmeonyesha kwamba mnajua umuhimu ya taaluma yenu, mnaowaponda madaktari mbona nyie hamjawa madokta yani mnapenda wawe na kipato sawa na na makonda wa daladala, ukitaka kudai haki yako dai hata kama kwa kuua na mtu yoyote nayeisjhi na kujua ananyimwa haki yake anatenda dhambi.
ReplyDeleteNDUGU MSANGI UMENENA, NAKUUNGA MIKONO YOTE MIWILI, HEE IMEKUWA TENA HADITH YA PUNDA???? SHARTI KWA KIBOKO, WATU WAMEPOTEZA MAISHA KWA UZEMBE WA SERIKALI HALAFU WANALAUMU MADKTARI WAO WAKALE WAPI??? WAMEDHARAULIWA SIKU NYINGI SANA NAKUMBUKA KABLA SIJAHAMA TZ KULIKUWA NA MGOMO WA MADKTARI SI SAWA KUTAJA MAJINNA LAKINI NAKUMBUKA SANA KUNA DR MMOJA AKIITWA DR NGOMA ALITAJWA SANA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUWA NI MKOROFI ALIFUKUZWA KABISA, MASIKINI SIJUI YUKO WAPI SASA HIVI. HIYO ILIKUWA NADHANI MIAKA YA THEMANINI AU TISINI MWANZONI, KWA HIYO KILIO CHAO CHA SIKU NYINGI SANA, UGHAIBUNI MADKTARI, MANESI, WAALIMU, POLICE NA WAHUDUMU WOTE WA TAIFA WANAITWA KEY WORKERS WANAHESHIMIWA SANA, BASI HATA MANENO MAZURI HAKUNA ILA VIRUNGU TU, JAMANI SERIKALI HII ITAWAAMSHA WALIOLALA.
ReplyDeleteMadai na migomo kwa kuua watu mnaisifu kweli tufika pabaya sana.Fedha inatawala nyoyo za watu.
ReplyDeleteHivi madaktari hawa mnapna wanadhiki sana kuzidi walimu wetu!Wacheni hoja za kudai utajiri.Kama ni posho watumishi wote hazitoshi si madaktari tu.Sote tunavumilia kwani uwezo wa serikali yetu si mkubwa kama manvyofikiri wasomi wetu.
Hapa naona tamaa imetangilia mno mbele.Tujali na maisha ya watu tunaowahudumia.Kumbe udaktari siku hizi si witu tena bali ni biashara!
Tunazo hoja kweli lakini chonde chonde twende nazo polepole tusitafute tu ushindi wa sifa.
Watu wa intern na ma nurse kwa ukweli kote duniani wanfanyakazi kulikomadaktari mahospitalini.Huu ndo ukweli na madaktari wanajua hilo.Anayekataa ukweli huoni mshabiki na hajui undani wa hili.
Kuna mtu anasema kwa nini mlishindwa kusoma udaktari huyu ndo mbumbumbu kweli.Yeye anadhani wote ambao hawakusoma udaktari hawakuwa na uwezo!Pole sana kwa uelewa mdogo.
Kila mtu aliamua kusoma anachokitaka na kuwa kile atakacho atafanya kwa moyo na upendo kwa wanotaka huduma yake.Hatukusomea kitu fulani ili tusipolipwa vizuri tuwakomoa walaji au tuwaue.
Tudai haki zetu si kwa kuua au kuharibu au kuvunja mali.Tukipata haki hizo kuna vitu twaweza kuvijenga tene lakini kunvingine hatoweza kurejesha kama roho za watu.
Hao wanaodai maoesa yote hayo wao mahitaji yao wana nunua wapi?
ReplyDeleteHeeee!Mikopo ya magari,mishahara mamilioni,posho kibao.
Magari mnayo lakini mbona bado mnachelewa kazini?Kwenda kwenye supu muda mwingi wakati wagonjwa wamelala kwenye mabenchi wakisubiri foleni.Wengine mnawa refer kwenye clinic zenu binafsi.
Mkilipwa zote hizo mtaacha kwenda part time Hindu mandal!Aghakan!Maana tunaona majina kwenye maboard huko.Manesi wakiwaita usiku watu wakiziwa majibu ni je yukomahututi?Kama sivo nitamuona kesho mpe asprin.
Tudai madai kweli na ni haki zetu lakini tusizidi kipimo,na kazi tufanye kweli kwa moyo na upendo wa kidaktari kama mafundisho yavyosemaTuache U mungu mtu pahali pa kazi.
Maana wenye tamaa wanafurahia sana migomo na vurugu,na wengi wao ndo wavivu ile mbaya.
Anaye kataa ukweli huu hazijiu kabisa hospitali zetu na baadhi ya madaktari wa hivyo hajawaona anasimuliwa tu.Nendeni mukaone ndipo mtoe hoja.
Si wote madaktari wako hivyo.Wapo wanaokula hela kwa haki na Mungu anawaona.Matendo yao Mungu atawasimamia.Lakini kundi kubwa wapo kwa maslahi na ni mingu watu.Maslahi wantaka na rushwa wanataka.
Tuseme ukweli tu jamani,tusikae tu kuiandama serikali.Viongozi wakazi hospitalini wanjua ukweli huu,manesi wanajua ukweli huo,madaktari wnafyunzi nao wanajua ukweli huo,na wananchi tuanjua ukweli huo.Serikali nanyi nendeni mukaone ukweli huo.
Kweli tuongeze posho na kzai tusimamie.